Dalili za mvua ni mawingu: Mradi wa SGR hautakamilika wote ndani ya utawala wa Magufuli

Pole sana Mkuu. Hauko peke yako kwani wako wengi wakiwemo Kampuni za Ulinzi wameporwa malindo na kupewa SUMA JKT. Cha kusikitisha ni kwamba nado wanasakamwa na Serikali hii hii wakati walishawapora Wateja.
Hakuna sekta ambayo haijaguswa awamu hii.

Sekta binafsi huzalisha ajira mara dufu kuliko Serikali ifanyavyo.

Sasa sekta binafsi imekufa ndiyo sasa unasikia kilio cha ukosefu wa ajira kila kona
 
[emoji23][emoji23][emoji23] dah mkuu, ndio sababu wanazotoa za kumuongezea muda kana kwamba huyu mtu akifa leo hii nchi nayo ndio inakufa.
Kawaida ukishakutana na watu ambao kazi yao ni kuitikia kiitikio, hawajui mashairi ya wimbo yanasemaje

Utasikia tu

Kwetu mwanza Nyegezi
Nyege nyege nyegezi

Hawajui kama huko ndani kuna masuala ya ambaruth wala nini
 
Hizo hesabu zako za uchumi za wapi? Ati pesa imepotela huko, kwa maana hakuna kinachofanyika hela imepotea. Tumejenga Kibiti Lindi kwa awamu tatu za Uongozi wa nchi kwako ilikuwa ni ni kupoteza pesa? vibanda vyetu wenyewe tunajenga kwamkuunga unga hatimae tunamaliza na kuhamia, huko ni kupoteza pesa? Maendeleo ni mchakato mnafeli wapi?
 
Hizo hesabu zako za uchumi za wapi? Ati pesa imepotela huko, kwa maana hakuna kinachofanyika. Tumejenga Kibiti Lindi kwa awamu tatu za Uongozi wa nchi kwako ilikuwa ni kazi bure? Maendeleo ni mchakato mnafeli wapi?
Kwani ahadi ya kukamilisha Sgr Dar to Moro ni awamu tatu za uongozi?
 
Hizo hesabu zako za uchumi za wapi? Ati pesa imepotela huko, kwa maana hakuna kinachofanyika.
Ninaposema pesa zimepotelea huko namaanisha sekta zingine zina starve, hii siyo serikali ya kwanza nchi hii.

Kama ni miradi ya reli, barabara, viwanda na hata ununuzi wa ndege haijaanza awamu hii. Na mambo mengine kama elimu, afya, maji, ajira, kilimo, umeme nk yalifanyika pia kwa pamoja na miradi hiyo.

Sasa awamu hii inayojificha kwenye hiyo miradi ya kimkakati kunyanyasa watu wake ndio unataka tuisifie?
 
Iyo train ya umeme unayosubiri mfano umeme ukikatika mtakuwa abiria mnashuka mnaisukuma au mnasubiri hadi umeme urudi?
 
Hata usipokamilika ndani ya muda wake sisi hatuna shida watakuja kufaidi wajukuu zetu kwani shida iko wapi?Marekani anapanga mipango ya miaka 50 namna nchi yao itakuwaje sembuse sisi?
 
Tofauti na watangulizi wake, yeye yote hayo anafanya kwa wakati mmoja. Ndiyo maana nchi nzima ni miradi na amefanya kwa kiwango kikubwa kuliko awamu zote zilizo mtangulia. Utapenda au hupendi ndio ukweli.
 
Umesahau na daraja la Busisi mkoani Mwanza?
 
Tuna bahati mbaya kuwa na uongozi kama huu.
 
Shida yenu mmekaririshwa kuwa watu wanawachukia ama kuwaonea wivu.

Hivi hiyo miradi ikifanikiwa me kama mtanzania sitanufaika nayo? Tunaposhauri ama kutoa mawazo tuna maana ya kujenga ama kuboresha. Kama ambavyo ikifanikiwa nasi tunanufaika vivyo hivyo ikifeli nasi tunaathirika.

Kuna haja gani ya kufanya miradi yote hiyo kwa mara moja wakati fedha zenyewe hatunazo? Tusipokuwa makini tutajikuta tuna miradi mingi ambayo haijakamilika na imetumia fedha zetu nyingi.

Dalili za awali kuwa uwezo wetu wa kuifanya hii miradi kwa pamoja ni mdogo tayari zimejiweka wazi ikiwemo rais mwenyewe kutamka wazi kuwa kuna mambo hayawezekani hadi tumalize miradi kwanza, mambo ambayo ni ya msingi na mengine ni stahiki za watu tena kwa mujibu wa sheria.

Tumenunua mandege ya masafa marefu bila kuwa na mpango kazi matokeo yamepaki tu na bado tunaambiwa zingine zitaagizwa hali ya kuwa hizi zilizopo hazileti tija yoyote.
Tofauti na watangulizi wake, yeye yote hayo anafanya kwa wakati mmoja. Ndiyo maana nchi nzima ni miradi na amefanya kwa kiwango kikubwa kuliko awamu zote zilizo mtangulia. Utapenda au hupendi ndio ukweli.
 
Sio ahadi unajenga kulingana na uwezo wako. Kumbuka hii sio pesa ya mkopo

Nilidhani hata unajua lolote kumbe hujui lolote, mpaka sasa serikali imeshakopa zaidi ya 1.5b sawa na 3.t. inaonekana hiki kitendo cha vyombo vya habari kuminywa hamjui lolote ndio maana mkianza kutetea watu wanawashangaa.
 
Kusema kwamba ukamilishaji wa mradi unachelewa kutokana na uchapaji kazi wa mkandarasiwa Kituriki na kwamba ingekuwa Wachina wangekamilisha kwa wakati si kweli.

Kama ni hivyo serikali inashindwaje kumuonya mkandarasi au kuvunja kabisa mkataba kama tunavyoona kwa miradi mingine ya ujenzi?

Kwa maoni yangu tatizo linaweza kuwa ni pesa.
 
Tofauti na watangulizi wake, yeye yote hayo anafanya kwa wakati mmoja. Ndiyo maana nchi nzima ni miradi na amefanya kwa kiwango kikubwa kuliko awamu zote zilizo mtangulia. Utapenda au hupendi ndio ukweli.
Uko sahihi sana, Sasa ukipata nafasi kapitie deni la taifa baina ya hao marais wengine na huyu, kisha uje na mrejesho.
 
Nilidhani hata unajua lolote kumbe hujui lolote, mpaka sasa serikali imeshakopa zaidi ya 1.5b sawa na 3.t. inaonekana hiki kitendo cha vyombo vya habari kuminywa hamjui lolote ndio maana mkianza kutetea watu wanawashangaa.
Mradi una phase tatu, mleta mada anazungumzia phase1 Dar to Moro na ndiyo ameambiwa na msiri wake haitakamilika kwa kipindi cha awamu hii, wewe unazungumzia phase gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…