Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

2015 waasi walishika mpaka baadhi mitaa ya Dumasikas lakini bado wakashindwa.
Jeshi la Syria lilikuwa limelilax kwa sababu waliamini vita inaelekea kuisha kwa sababu ya makubaliano ya Astana Kazakhstan yaliyo sainiwa na Urusi Uturuki,na Iran hivyo hili shambulizi hawakulitegea kabisa.

Sasa Uturuki amewazunguka Urusi na Iran na kuwaamuru waasi kuanzisha mashambulizi kinyume na makubaliano.
Syria ni eneo muhimu sana kimkakati kwa Urusi na Iran watafanya kila aina ya mbinu kuhakikisha inabaki mikononi mwao.
 
Nimefuatilia comments zako nyingi inaonekana hii offensive ya waasi imekutouch sana aisee! Sometimes unajaribu kuleta habari za kujifariji hata za kupotosha lakini mwisho wa siku mambo kwa ground ndio hivo

Kwa nini umeumia hivi mkuu!?
Ww mbona Ukraine akipigwaga huwa unaumia wakati ww ni mmatumbi?
 
Tatizo la hao rebels IDF wanaweza kuwa wanawasaidia ila wakifanikiwa kumtoa Assad watamgeuka mu Israel
Huo muda hawatakuwa nao kwasababu wataanza kupigana wao kwa wao kwa muda mrefu, ndani ya hilo kundi la Waasi kuna wengine hawaelewani kuhusu misimamo.

Hilo Kundi ni Kokolo limejaza kila aina ya Wahuni.

Lakini Israel na US zitakuwa zimefanikisha kukata Line ya Ayatolah kwenda kwa Hezbola na Hamas.
 
Habari za hivi punde zinadai,Wapiganaji wa HTS ambao wanasadikika kuungwa mkono na nchi ya Uturuki, wameuzingira mji wa nne kwa ukubwa nchini Syria wa HAMA kusini Magharibi mwa nchi hiyo. Mji huo upo umbali wa Kilometa 210 kutoka mji mkuu wa Syria wa Damascus.

Ikumbukwe kuwa, Wiki iliyopita, Waasi hao walifanya mashambulizi ya kushitukiza na kuuteka mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria wa Aleppo.

Jeshi la anga la Syria (SAA) likisaidiwa na ndege za kivita za Urusi zilishambulia mji wa IDLIB ambao ulikuwa ngome kuu ya wapiganaji hao tangu mwaka 2015. Hata hivyo, Mashambulizi hayo yanaonesha kutowarudisha nyuma waasi hao.

Endapo mji wa HAMA utadhibitiwa na waasi hao,Basi watakuwa umbali wa Kilometa 78 kutoka mji wa tatu kwa ukubwa nchini Syria wa HOMS na umbali wa Kilometa 210 kutoka mji mkuu wa Syria wa DAMASCUS.

Hata hivyo,Waziri wa Mambo ya nje wa Iran ameilaani Marekani na Israel kwa kushambulia msafara wa Wapiganaji kutoka Iraq waliokuwa wanakwenda kuisaidia jeshi la Syria kupigana vita vya Ardhini na waasi hao.

Uturuki imeitaarifu Urusi kuacha kutumia ndege zake kuwashambulia Raia lasivyo Uturuki itapeleka Mifumo ya Ulinzi wa Anga Kasikazini mwa Syria ili Kuziangusha ndege za Urusi na Syria ambazo zinafanya mashambulizi hayo.

Source: Aljazeera
: Dw English
Kwani akina Ritz na yule bibi kule zenji wako wapi
 
DLLJYDFRQII67HJD4X5KEKWSCY_size-normalized.jpg
Silaha za Assad ni za Kale kama hichi kifaru cha Kirussi aina ya T50 kilichotekwa leo Mjini Hama.
 
BREAKING NEWS
Waasi wa HTS wameuteka mji wa nne kwa ukubwa nchini Syria wa HAMA. Jeshi la Syria limesema limeondoa wanajeshi wake 12,000 waliokuwa wamejidhatiti kuulinda mji huo. Hata hivyo,jeshi hilo limesema kwamba limejiondoa ili kuepusha vifo vya raia, kwa mapigano ya mjini ambayo yangelitokea( URBAN FIGHTING).

Msemaji wa jeshi la Israe,Daniel Hagar amesema kwamba bado wanafuatilia kwa ukaribu mapigano hayo na mienendo ya waasi hao. Hata hivyo amesema pia,Endapo waasi wataukamata mji mkuu wa DAMASCUS basi Israel itapeleka vikosi vyake katika Milima ya Golan kulinda Ardhi na uhuru wa Israel.


View: https://youtu.be/PGpRPWg6cW8?si=tirR3OBK22z-ZiRq

Israel ndio dawa ya magaidi.
 
Uturuki ipo vizuri kijeshi. Kumbuka kuwa jeshi la Uturuki lilikuwa jeshi la pili Duniani, baada ya Marekani, kuwa na uwezo wa ku-refuel ndege zao za kivita zikiwa angani.

Uturuki ndiyo nchi pekee ambayo wananchi wake wengi ( 98%l).ni waislam, ni nchi mwanachama wa NATO. Na kukubaliwa kwa Uturuki kuwa mwanachama wa NATO, haikuwa ni kutokana na upendo wa nchi za Magharibi, bali ni kutomana na uwezowakewa kivita.


The Turkish Armed Forces is the second largest standing military force in NATO, after the U.S. Armed Forces. Turkey is one of five NATO member states which are part of the nuclear sharing policy of the alliance, together with Belgium, Germany, Italy, and the Netherlands.
Edorgan leo anaipiga mkwara Iran na Russia? Kweli nimeamini middle East ni wehu.
Ki
 
TV za Nchi za Kiarabu za Kisunni zinashangilia kukombolewa kwa Mji wa Hama wa Syria Arab Republic.
 
Back
Top Bottom