T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Israel huwa ina solutions, alternative solutions na "bahati" za kutosha zilizopangwa.Tatizo la hao rebels IDF wanaweza kuwa wanawasaidia ila wakifanikiwa kumtoa Assad watamgeuka mu Israel
Hamas wamekurupuka kuua mamia ya Wayahudi, Israel inawadhibiti na kuingia Gaza kusafisha. Hezbollah wanaanzisha mashambulizi, Israel inawashambulia taratibu haiendi kwa fujo. Baadae inaonekana Iran inatishia sana itasaidiana na haya makundi mawili, Rais wa Iran anakufa kwa ajali "bahati mbaya".
Hamas inapigwa inaelekea ukingoni, Hezbollah inaanzishiwa lakini Iran wala haiisaidii maana Rais mkorofi hayupo tena. Hezbollah inapigwa inaanzisha mazungumzo ya amani hapohapo Syria ambapo inapitisha silaha waasi wanaanzisha mapigano.
Hivyo waasi hawa wakiiletea changamoto Israel, bado solutions za kutosha zipo mikononi mwa Israel. Ndio maana measure ya kwanza ni kupeleka majeshi Golan heights mpakani na Syria.
Kwenye mlinganyo huwezi ona msaada wa Israel kwa hao waasi ila Israel yenyewe inafanya vitu kwa hesabu inaenda mbele inarudi nyuma. Sasa hawa wakurupukaji wanashangilia tukio moja kumbe yenyewe iko na strategic responses.
Yani Israel inaweza ona inashambulia magaidi huku inalaumiwa na dunia, ikaomba mazungumzo yakafanyika huku ikijua wakurupukaji wataishambulia tena. Ikakaaa ikaandaa vifungu vya kuiruhusu kushambulia ikichokozwa, ikatulia kama mnyonge ikakusanya ushahidi na vithibitisho kuwa inavunjiwa amani. Alafu ikashambulia vikali kwa kisingizio sisi hatuna fujo tunajitetea tu.