Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

Katiba chakavu ndio chanzo cha haya yote.....ni sawa na kuvaa shati lililopauka wakati uwezo wa kununua shati jipya unao
 
Dangote ni mfanyi biashara hajishukuliki na siasa...amejenga refinery kwao na ameona faida kubwa sana katokana na huo refinery. Amefanya hesabu zake na ameona kunafaidi kubwa akijenga afrika mashariki
 
Mimi naombeni kuuliza tu mwenye hilo bomba ni total sasa wao ndio wawekeza hapo je watakubali kuwekewa hizo refinery sijui za kusafisha mafuta?
 
Kujengwa kwa refinery Mombasa hainamaanishi mafuta lazima itoke Uganda bali itanunuliwa kutoka soko ya dunia mahali bei iko chini. Mafuta ya Uganda kusafirishwa kw bomba la EACOP hadi Tanga itagharimu $12 kwa pipa na kutoka ughaibuni hadi mombasa ni $2. Tayari kuna shida kwa bei
 
Kwani Tanzania haiwezi kujenga kama nchi, tulikuwa na refinery kigamboni Tipper sio lazima kumtegemea Dangote.
Anataka ulinzi wa nini huu ni wakati wa soko huria.
 
Refinery ya Lagos inatoa mafuta yake kwa wingi kutoka US....
Nigeria ni Oil producer hawajampa mzawa? Kweli aisee nigeria ina extract 1.4million-18m barrels per day na refinery yake ina capacity ya kuchakata 650,000 barrels per day bado anachukua US and other suppliers!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…