Danguro jipya laibuka Mbezi Mwisho, wapangaji wahamishwa kupisha biashara

Danguro jipya laibuka Mbezi Mwisho, wapangaji wahamishwa kupisha biashara

Wakuu

Kwa sasa hili jiji la Dar kila kona hali imeharibika, biashara ya ukahaba imekithiri kwelikweli mpaka kwenye maeneo ambayo hayakufikirika kama siku moja kunaweza kuwa na danguro

Madanguro yanaota kama uyoga kila siku na wenye mamlaka wamekaa kimya as if haya madanguro hayaonekani, hii ni kero kubwa kwa wakazi wa maeneo husika hasa katika makuzi na malezi ya watoto kwani madanguro hayo yanapatikana katika makazi ya watu

Kwa sasa kuna DANGURO kuuubwa limetengezwa maeneo ya Mbezi Mwisho, wananchi na wapangaji wa eneo lile walipewa notsi kuachia vyumba vyao kupisha biashara ya ukahaba

Kwa sasa danguro limekuwa kubwa mno, baa ya lubumbashi na Kwa GOD zimekuwa chachu ya ukahaba huu

Imagine lile eneo lote kati ya kwa god na lubumbashi, zile nyumba za kati zote ni madanguro
Eneo lile saa 1 jioni tu makahaba yamejaa wala hayaogopi kitu

Serkali na jeshi la polisi tunaomba danguro hili lisambaratishwe
Wame target wasafiri wanaoshuka na kuondoka pale Magufuli Bus Terminal ?
 
Huwa wanalipa kabla kabisa ya kodi kuisha au wanalipia miezi mingi zaidi ili wasipewe notisi. Kuna jamaa yangu anakaa nyumba aliyokuwa anakaa Asha nani sijui yule aliyetafutwa na polisi miezi kama miwili iliyopita, yule mwenye tattoo ya ua mgongoni. Asha na wenzake walikuwa wanalipa kodi mapema kiasi kwamba mwenye nyumba mzee Msabato alipojua wanatafutwa na polisi kwa kesi hiyo akawa hana hela ya kuwarudishia awahamishe. Mzee alisaidiwa na mtu mwingine kuwarudishia hela
😆😆😆😆! Dah.
 
Mimi maoni yangu serikali ingeweza ndoa za muda mfupi kama siku 3 au week, mwezi, mwaka ili kupunguza wimbi kubwa la madanguro lakini hivi hivi ni ngumu na kwa sasa jiji la Dar es salaam kote pamechafuka akuna jipya naamini ndoa hizo zitapunguza ukahaba na ukienda guest bila cheti cha ndoa upesi room
Wew kweli Dikteta usiye na maono.
 
UFUNUO 2: 19-23

19 Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
21 Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
23 nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake
Hivi we mwanamke umetumwa au? Yani we ni kushusha maandiko tu!
 
Kwa hiyo wana mpango wowote wa kubadilisha jina hilo la kwa God?
 
Kwani maandiko yanakuumiza Mjuni Lwambo?
Pole mwaya😂😂😂
Sasa yataniumiza vipi wakati hayo ni maneno tu.... Nilitaka nimalizie kama ya kwenye kanga nikajua utachukia kwamba nadharau maandiko.
 
Halafu mleta uzi anaomba serikali iingilie kati..aje asome hii comment ndio ajue serikali yenyewe ina mlengo gani kuhusu hao malaya.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Umalaya ni biashara kama zingine huwezi kuikwepa tunajidanganya kupambana nayo ukweli inawasaidia watu wengi TU iwekewe mazingira mazuri Ili pande zote zifaidike ulaya ni biashara halali na Kodi wanalipa
 
Back
Top Bottom