Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Naona wengi tunalaumu kwa nini watu hawakuingilia na kuwazuia watekaji.
Niwe mkweli,zaidi ya kujaribu kurekodi nisingeweza kutokea Front kuwazuia watekaji.
Sio kwamba Sina ujasiri wa kufanya hivyo,la hasha!
Kila mtu apambane na hali yake.
Nimeamua kuishi kama Fala sio kwamba Mimi mjinga,sitaki kelele Wala ugomvi na mtu.
Kama yeye ameamua kuishi kwenye spotlight Mimi ni nani mpaka nihatarishe Maisha yangu na future ya wanangu kwa sababu ya "Abdul nondo"!
Uislam huo Mimi Sina.
Nakupita tu kichwa changu chini na mikono yangu nyuma.
Bora nibaki Fala nipite salama hapa Duniani kuliko kujitafutia tabu kwa vitu vya kupita tu.
 
Hii serikali kuna mtu hana akili tuu. Huwezi kufanya matukio ya kipumbavu namna hii kila mara bila aibu.
Ila faiza foxy alisema akifanya muislam tumefanya wote, ngoja ninyamaze tuu.
 
Kama wangekuwa na chuma wangenidhuru ila sijui kama hawakuwa nayo maana wakati wawili wanapambana kumuingiza mchizi ndani kuna mmoja alikuwa kakaa mlangoni kwenye siti. Hawa jamaa wakija hawaogopi kabisa wanakuchukua katikati ya watu wanakuburuza wanasepa na wewe. Mimi nilikuja kutahamaki mchizi anapiga kelele huku anaburuzwa na mapingu wanakazana kumfunga. Sasa mimi niliwauliza nini shida? Hawanisemeshi wanakomaa tu na mchizi nikaona msinitanie maana najua mishe zenu. Nikaingia mzima tukawa wawili against wawili huku mmoja kakaa kwenye siti ya mlangoni. Baada ya kuona mambo yashakuwa mengi wakageuza gari haooo yan kama majizi kabisa huwezi amini eti ni watu wa usalama.
 
Ukifuatilia harakati za Abdul nondo na wote wa namna yake watakuambia wanawapigania watanzania!
Ukweli mchungu hizo harakati ni sehemu ya kazi zao za kuwapatia riziki kama alivyo fundi mjenzi dereva mwalimu na askari nk, sasa kila kutafuta riziki kuna changamoto zake ambazo mtu huzikabili na kusonga mbele.
Fundi umeme kuna wakati ana pigwa shoti na fundi bomba kuna wakati analowana maji na hakuna anaye jali kwa vile ni wajibu wake!
Sasa hao wasiasa na wanaharakati wanataka kila wanapo pata changamoto watanzania wote wasimame nao hali ni wajibu wao kuzikabili.
 
Kimtindo nimeipenda hii.
 

dah, hongera sana kwa ujasiri, binafsi siwezi risk maisha yangu kiasi hicho kwa ugomvi nisioujua sana sana kama kuna chochote ambacho ningefanya labda ningepiga picha au video tena kwa siri wasinione, lkn kama wanamfanyia hivyo mtu ninayemjua na kumpenda hapo nitajitolea liwalo na liwe lkn siyo kwa stranger kwa maana huo ugomvi siujui …
 
Kilichobaki ni wanafamilia kumteua mtu wa kupokea sh. Milioni tano.
 
Cha ajabu ni kwamba wamesoma na hiyo miongozo wanaijua vilivyo. Labda ni majambazi, yaani si watu wa usalama wa raia.
 
Pole sana ndugu yetu Abdul, mwenyezi Mungu akupiganie wakuachilie salama.

Lakini Abdul kwa level aliyofikia, alitakiwa awe hata na ka vitz jamani, sass watu wanakuja kukutekea stand, tena stendi ya mbezi shamba.
Kwani Bonge hakuwa na gari?
 
Inaonesha mole alipanda nae basi tangu wanatoka kigoma na walipokaribia stend mole aliwatonya kuwa ndio wanaingia stend hivyo watekaji wakajiandaa kumpokea nondo kwa bashasha, mole alipomaliza kazi yake huyo akashuka kwenye basi na kwenda kuendelea na majukumu yake stakishari.
 
ACT ni sehemu ya serikali Zanzibar ambayo ndiye mtawala wa Tanganyika. Naamini watamrudisha salama.
 
Mtu anatekwa watu waangalia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…