Hivi utaratibu wa kumkamata mtuhumiwa si uko wazi Kwa mujibu wa Sheria?
Huyo Nondo ni Katibu wa Chama, ina maana ana address yake kwamba anaishi wapi
Mnafika Kwa mjumbe wa nyumba 10 kwenye Mtaa anaoishi kisha mnaenda kumchukua.
Hiyo kumvizia stendi na kumkamata kama jambazi inazua taharuki kwamba huenda ni Wasiojulikana
Hebu Viongozi wa hayo makundi sijui ni Usalama ama Polisi Idara ya Usalama, warudie kusoma miongozo ya kazi zao.
Najua mnatekeleza majukumu yenu, lakini fuateni Sheria na taratibu za kazi zenu