Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ccm na act ni mtu na mwanawe lakini,so hapo kuna kamchezo kanachezwa.
 
Dhambi ya kuteka, kutesa na kuua watu ikikolea hata wanaoifanya sasa watafanyiwa!
 
Hii si kazi ya Samia. Mzanzibar yyt akiwa na cheo chcht huku bara anakuwa na mipaka ya utendaji wake.

kuna wenye nchi. Ni tabaka moja tu tokea uhuru.

Usalama wa nchi hii kwanza ni kuwatoa wahalifu kama sehemu ya watendaji wa serikali.

Hilo linawezekana iwapo tutaweza kuuondoa mfumo wa serikali kuu. Kwa kuchagua vyama vinavyopigania mfumo wa serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Hili zitto halikubali. Kwa kuwa kanyang'anywa akili. Kwa kudhani wakichukua maamuzi haya sahihi, anaungana na cdm. Kwake ni bora kujilinganisha ccm na si chadema. Kwa hiyo tuendelee tu kuona matukio haya wakiendelea. Kwa
 
Pingu na simu ya mtekaji vimeokotwa eneo la tukio ni uzembe hata Kama ni mission hii Sasa ni hamna kitu unaangusha vitendea kazi kweli Polisi ccm
 
Huwezi kumtisha kwa mawe adui ALIYE SHIKA BUNDUKI.

QUOTED FROM FID Q
Kwahiyo nikija na mguu wa kuku utaliwa kiboga kisa bastola tena umati mkubwa Stendi.....

Unakuja na SMG nakupimia YADI TATU.... gari linapigwa jabari la nguvu ukigeuka tu niko na wewe kama UMERUKIWA na Chuwi hiyo SMG itakohowa mpaKA jiji LITKISIKE

Piteni piteni hata Goma na Kisangani mara moyamoya hata mafunzo ya Mgambo
 
Watanzania hacheni ujinga Mtu anatekwa alafu mnakazi ya kupost tu
 

Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu

====

UPDATE

JamiiForums imewasiliana na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT Wazalendo Shangwe Ayo ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza Nondo alikuwa ametokea Kigoma baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika, ambapo wakati anashuka kwenye basi Stendi ya Magufuli watu wasiyojulikana watatu walimfuata kukawa na purukushani Nondo akijitahidi kujinasua lakini walifanikiwa kumchukua na kuangusha pingu walizokuwa wameenda nazo pamoja na begi alilokuwanalo Nondo

Matukio mengine ya utekaji kuwahi kufanyika nchini haya hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Shangwe ameeleza pia gari lililomteka Nondo ni Land Cruiser nyeupe yenye namba za usajili T 249 EMV. Taarifa za awali walizitoa kwa mashuhuda ambao walikuwa wanamfagamu Nondo, baada ya kufungua begi lake kulikuwa na note book ambayo nayo ilithibisha kumilikiwa na Abdul Nondo

Pia shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema gari hilo lililokuja kumteka Abdul Nondo lilikuwa na watu 4, wawili wakiwa na bunduki na wawili wakiwa mikono mitupu, watu walipoenda kuangalia kuna nini na kujaribu kuhoji waliwanyooshea bastola na hivyo watu kubaki wanaangalia tukio hilo likitokea na Abdul Nondo akawa ametekwa! Katika purukushani hizo kwa maelezo ya shuhuda mbali na pingu na bengi la Nondo, ilianguka pia inadaiwa simu ya moja ya watekaji ambavyo vyote vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Magufuli.
Kama mmekabizi pingu na simu kwa police Sina Cha kuwasaidia hiyo pingu ingewafukuzisha kazi Wengi na simu tungeitumia kufuatilia waarifu hapo MMEFANYA USHENZI FUTENI LIUZI LENU
 
1. Milishindwa kupiga picha wahusika?
2. Mlishindwa kupiga picha gari lao?
3. Hakuna alie weza hata kuchukua video ya tukio?
4. Walikua na silaha za moto?
5. Walikua wangapi?
6. Mlishindwa kuwahoji?
7. Mlishimdwa kuwazuwia wasimchukue?
Dar es salaam na Wanaume wao mdebwedo mdebwedo wapuz tu
 
Simba mmoja anavamia kundi kuuuuubwa la nyumbu takribani nyumbu 600 anajichagulia mmoja wengine 559 wanasimama pembeni na kushuhudia mwenzao akitafunwa.

1. Milishindwa kupiga picha wahusika?
2. Mlishindwa kupiga picha gari lao?
3. Hakuna alie weza hata kuchukua video ya tukio?
4. Walikua na silaha za moto?
5. Walikua wangapi?
6. Mlishindwa kuwahoji?
7. Mlishimdwa kuwazuwia wasimchukue

Nawaza tu askari anawezaje kusahau Pingu

Kwa Sababu huwa anaifungua wakati mtuhumiwa ameshanyoosha Mikono baada ya kutaitiwa

Sisi wengine ni akina Tomaso 😂
Si askari wote wana nidhamu , smart ni wachache sana wengine ni kutumia nguvu, matokeo ndio haya yanayo onekana
 
Back
Top Bottom