Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kazi ya k
KAZI ya kiongozi aliyeko madarakani ni kulinda raia wake.
Bibi amefeli kabisa
Kama wananchi wenyewe hawajijali nani awajali zaidi? Uchaguzi umeporwa kwa mtutu na watu kuuawa lakini bado kuna makundi ya watu wamejitokeza na kusifia kuwa ulikuwa mzuri. Raia hao hao ndiyo walikuwa mbele kwenye kusaidia hujuma. Acha nchi ivune ilichopanda.
 
stendi yote hamna aliye record? mkewe hakuja kumpokea stand?
 
Ndio maana watu wanasema katekwa...

Lakini haya yote lawama ni kwa jeshi la Polisi, haya mautaratibu ya kunyakua watu wameyavumisha wao wenyewe...
Ni sahihi, nimeona hata taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nao kutojua nani hasa aliyemchukua huyo Abdul Nondo.

Kwa mujibu wa aliyetoa taarifa, wanasema Pingu zilianguka wakati wa Purukushani na hao wakamataji(watekaji).

Kwa mujibu wa Sheria, wanaoruhusiwa kutumia Pingu ni Askari Polisi, Magereza na Takukuru Kwa Uchache.

Kwahiyo ni obviously waliohusika katika utekaji huu ni Vyombo vya Usalama

Kwahiyo ndani ya Nchi moja lakini Vyombo vya Usalama havina mawasiliano.

Huu ni utekaji kama utekaji mwingine unaofanyika kwenye hii Nchi.

Tukifanya mchezo tutatekwa wote tuishe 🙌
 
Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu

====

UPDATE

JamiiForums imewasiliana na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT Wazalendo Shangwe Ayo ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza Nondo alikuwa ametokea Kigoma baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika, ambapo wakati anashuka kwenye basi Stendi ya Magufuli watu wasiyojulikana watatu walimfuata kukawa na purukushani Nondo akijitahidi kujinasua lakini walifanikiwa kumchukua na kuangusha pingu walizokuwa wameenda nazo pamoja na begi alilokuwanalo Nondo

Matukio mengine ya utekaji kuwahi kufanyika nchini haya hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Shangwe ameeleza pia gari lililomteka Nondo ni Land Cruiser nyeupe yenye namba za usajili T 249 EMV. Taarifa za awali walizitoa kwa mashuhuda ambao walikuwa wanamfagamu Nondo, baada ya kufungua begi lake kulikuwa na note book ambayo nayo ilithibisha kumilikiwa na Abdul Nondo

Pia shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema gari hilo lililokuja kumteka Abdul Nondo lilikuwa na watu 4, wawili wakiwa na bunduki na wawili wakiwa mikono mitupu, watu walipoenda kuangalia kuna nini na kujaribu kuhoji waliwanyooshea bastola na hivyo watu kubaki wanaangalia tukio hilo likitokea na Abdul Nondo akawa ametekwa! Katika purukushani hizo kwa maelezo ya shuhuda mbali na pingu na bengi la Nondo, ilianguka pia inadaiwa simu ya moja ya watekaji ambavyo vyote vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Magufuli.
Amechukuliwa na police au watu wasiojulikana???
Kuna watu hawajulikani dunia hii??
Hawajulikani hawana ndugu???
Hawajulikani hawajazaliwa na mama???
Nani anawalipa mishahara ilihali hawajulikani????
 
Watu ambao hawajitambulishi wanaweza kukupeleka kusiko julikana pia
 
Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu

====

UPDATE

JamiiForums imewasiliana na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT Wazalendo Shangwe Ayo ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza Nondo alikuwa ametokea Kigoma baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika, ambapo wakati anashuka kwenye basi Stendi ya Magufuli watu wasiyojulikana watatu walimfuata kukawa na purukushani Nondo akijitahidi kujinasua lakini walifanikiwa kumchukua na kuangusha pingu walizokuwa wameenda nazo pamoja na begi alilokuwanalo Nondo

Matukio mengine ya utekaji kuwahi kufanyika nchini haya hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Shangwe ameeleza pia gari lililomteka Nondo ni Land Cruiser nyeupe yenye namba za usajili T 249 EMV. Taarifa za awali walizitoa kwa mashuhuda ambao walikuwa wanamfagamu Nondo, baada ya kufungua begi lake kulikuwa na note book ambayo nayo ilithibisha kumilikiwa na Abdul Nondo

Pia shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema gari hilo lililokuja kumteka Abdul Nondo lilikuwa na watu 4, wawili wakiwa na bunduki na wawili wakiwa mikono mitupu, watu walipoenda kuangalia kuna nini na kujaribu kuhoji waliwanyooshea bastola na hivyo watu kubaki wanaangalia tukio hilo likitokea na Abdul Nondo akawa ametekwa! Katika purukushani hizo kwa maelezo ya shuhuda mbali na pingu na bengi la Nondo, ilianguka pia inadaiwa simu ya moja ya watekaji ambavyo vyote vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Magufuli.
Mmmm! Haya Bhana Wajinga Ndio Wataendelea Kuumiza Kichwa Ngoja Kijana Atengeneze Umaarufu Ila Ni Mtu Wao
 
Watu ambao hawajitambulishi wanaweza kukupeleka kusiko julikana pia
Kama ni hivyo usemavyo basi nchi yetu tupo kwenye tatizo kubwa. Kwamba pembele ya polisi watu wasiojulikana wanawasaka tu wenye maoni pinzani na kuwapeleka kusikojulikana ambako wanateswa na kudhulumiwa uhai.
Kwamba mbele ya polisi watu wanakimbizwa na kumiminiwa risasi za moto na kuawa!
Sikiliza! Huo ujasiri hata waasi wa Congo DRC hawana!
Fikirisha akili yako
 
Hali tete,polisi nao hawajui Nondo amechukuliwa na nani?Tuombe Mungu arudishwe salama.
 
Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu

====

UPDATE

JamiiForums imewasiliana na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT Wazalendo Shangwe Ayo ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza Nondo alikuwa ametokea Kigoma baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika, ambapo wakati anashuka kwenye basi Stendi ya Magufuli watu wasiyojulikana watatu walimfuata kukawa na purukushani Nondo akijitahidi kujinasua lakini walifanikiwa kumchukua na kuangusha pingu walizokuwa wameenda nazo pamoja na begi alilokuwanalo Nondo

Matukio mengine ya utekaji kuwahi kufanyika nchini haya hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Shangwe ameeleza pia gari lililomteka Nondo ni Land Cruiser nyeupe yenye namba za usajili T 249 EMV. Taarifa za awali walizitoa kwa mashuhuda ambao walikuwa wanamfagamu Nondo, baada ya kufungua begi lake kulikuwa na note book ambayo nayo ilithibisha kumilikiwa na Abdul Nondo

Pia shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema gari hilo lililokuja kumteka Abdul Nondo lilikuwa na watu 4, wawili wakiwa na bunduki na wawili wakiwa mikono mitupu, watu walipoenda kuangalia kuna nini na kujaribu kuhoji waliwanyooshea bastola na hivyo watu kubaki wanaangalia tukio hilo likitokea na Abdul Nondo akawa ametekwa! Katika purukushani hizo kwa maelezo ya shuhuda mbali na pingu na bengi la Nondo, ilianguka pia inadaiwa simu ya moja ya watekaji ambavyo vyote vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Magufuli.
Hivi watanzania kwa umoja wetu tumeshindwaje kuunganisha nguvu zetu kuyaondoa haya majambazi madarakani?
 
Kama ni hivyo usemavyo basi nchi yetu tupo kwenye tatizo kubwa. Kwamba pembele ya polisi watu wasiojulikana wanawasaka tu wenye maoni pinzani na kuwapeleka kusikojulikana ambako wanateswa na kudhulumiwa uhai.
Kwamba mbele ya polisi watu wanakimbizwa na kumiminiwa risasi za moto na kuawa!
Sikiliza! Huo ujasiri hata waasi wa Congo DRC hawana!
Fikirisha akili yako
Watu wasiojulikana ni taasisi
 
Back
Top Bottom