2. Umesema, kuna habari inaweza kuwa ni kubwa kwako kustahili front page, lakini kwa mwingine isiwe habari kabisa!. Huu ndio Uhuru wa habari.
Kaka P, hapa ndo umenisikitisha sana, na hasa ukizingatia wewe ni mwanahabari mbobevu..!! Mtoa mada, kataja matukio kadhaa ambayo hayo magazeti yanayoambiwa hajaandika popote ndani ya magazeti hayo.
- Hivi kwa hali ya utekaji ya sasa, unadhani hii si habari kubwa???
- Hivi unadhani habari kuwa kubwa ni kwa sababu ya maamuzi ya mtu fulani kuiona kuwa kubwa au habari yenyewe..!!???
- Hivi, kwenye huo uanahabari wako, HOW DO YOU DECIDE kwamba habari hii ni kubwa au ndogo?
Vile vile, habari kuwa kubwa kwa huyu lakini ndogo kwa mwingine, hilo si kigezo. habari zote zipo hivyo, inategemeana tu na interest ya mtu unayempelekea habari au impact ya habari hiyo kwa jamii au habari hiyo ina public inetrest kwa kiasi gani. Mfano, kuna wale wa 51mba na Yanga, ukianza kuwaambia habari za vitasa, wengine hawakuelewi. Kuna watu unavyoviandika wewe kwao havina maana, etc. Hivyo kuamua habari kama ni kubwa ua la, likiachwa kwa mtu binafsi badala ya impact ya habari husika kwa jamii, HAKUTAKUWA NA HABARI KUBWA WALA NDOGO.
CC
Kadhi Mkuu 1