Polisi wanavyokaa kimya wanaset negative precedent, matokeo yake wananchi wataanza kujichukulia sheria mkononi kwa mtu yoyote wanayemtilia shaka.
Ukisikiliza scene zote za utekaji unaona tu watu walikuja kiraia wakambeba mtu , huku watu wakibaki wanaangalia.
Mfano huyo waliomteka kwenye basi kama wananchi wangeamua kufunga basi na kusema hakuna kumchukua mtu je hao watekaji 4 wangeweza kumudu kuua watu wote 50+ kwa mkupuo?
Au polisi kutokana na kuchukua failures wengi ndio akili zimedumaa kabisa?
Kulaumu Polisi kwa ujumla, hapana...
Tatizo la Jeshi la polisi lipo kwa ma - Commanding Officers wao au maafisa wa juu wa Jeshi la Polisi IGP, MA - RPC nk ambao ndio wenye mamlaka na watoa amri na maelekezo kwa hawa walio chini.....
Hawa ndio wameoza kwa kuwa wamenunuliwa na kuwekwa kwenye mikono ya genge la wanasiasa walio madarakani kiasi cha maamuzi yao ku - abuse sheria na Katiba ya nchi. Mfano ni tukio la Mbeya juzi kwa polisi kupambana na vijana wa CHADEMA ktk mazingira ya uonevu kabisa na aliyeongoza Operesheni hiyo ni afisa mkubwa wa polisi Awadhi Haji....
Ukiona serikali ya nchi imejaa wizi na ufisadi wa fedha na Mali ya umma, jua kuwa fedha inayoibwa inakwenda ku - consolidate madaraka ya viongozi vya kisiasa walio madarakani kwa kuhonga na kuunda vikundi vya kigaidi na kuvifadhili Ili viteke na kuua wapinzani wa mabwana zao....!
Genge hili la wanasiasa hawa wa CCM walio madarakani mission yao kuu ni ya kisiasa - kuhakikisha kila aliye kinyume nao na anahatarisha uwepo wao madarakani anakwenda chini, anakufa......
Genge hili liko polisi, mahakamani, magerezani, bungeni....
Ukipigwa nje na kujifanya unaenda mahakamani, huko nako utawaluta na kamwe huwezi kupata haki yoyote...
Njia pekee iliyobaki kwa Sasa ni kumlilia na kumwomba Mungu wetu muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo atumie nguvu na mamlaka yake kupambana na watu hawa waovu waliokubali kutumiwa na shetani kutesa na kuua binadamu wenzao....
Alifanya hivyo kule Misri ya kale, Urumi ya kale, Babeli (Babylon) ya kale dhidi ya watu wa Mungu....
Hata Tanganyika anaweza....