TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Duh

Mtu mmoja mwenye haki alisababisha mabadiliko makubwa Misri na Tunisia 🐼
 
Hata hili litapita kama mengine sisi tugoje yetu tu. Huu ndiyo mfumo tulio amua twende naa kwa sasa, tutauzoea tu, mbona nchi za wenzetu hivi vitu ni kawaida tu. Wewe ukiamka salama mshukuru Mungu nenda kazini kama utabahatika kurudi salama nyumbani shukuru Mungu. Mfa maji haishi kutapa tapa
Huwezi kuwa na furaha wewe uko hai na salama lakini nduguzo na jirani zako wanaomboleza misiba inayosababishwa na binadamu wenzao...

Nimekushangaa kidogo kusema "kuuana ni mambo ya kawaida......" Na kwamba nchi za wenzetu ni ya kawaida tu....

Bila shaka siku mwanao kapitiwa na ukaenda kuokota maiti yake huko shimoni ndiyo utakuja kujua kuwa Mungu hajapenda kauli yako ya "....shukuru Mungu wewe ni mzima pamoja na kuwa nduguzo na jirani zako wanaomboleza vilio tokana na vifo vya kusababishwa na binadamu wenzako..."

Biblia Neno la Mungu inasema;

"...Lieni na waliao, ombolezeni na wanaomboleza na furahini na wanaofurahi..."

Cha ajabu wewe uko kinyume na kauli ya Mungu. Why? Are you among the killers...?
 
Sio jambo jipya watu kufanya mauji huko mitaani tunapoishi kama Kuna watu wapo tayari kukuua sababu yakunyang'anya simu tu sasa mtu kama huyu ukimpa posho nzuri na maisha yakufurahia hapa duniani kuua itakuwa ni jambo dogo

Kama mnavyosikia habari za watu kupotea ni wengi sana lakini zinazolipotiwa ni zile tu za watu wenye nyazifa fulani kwenye tukio

Maono yangu nazani Kuna uwezekano mkubwa kwenye hii plan hawa wazee wa tinted nyeusi hawakujua wanayekuja kumkamata mpaka wamekuja kudedisha walijua ni raia wa kawaida lakini ndio hivyo mtu wa watu alikuwa mtu wa dini wamejikuta wanajichanganya maiti huwa zinatupwa polni Leo hii tumeiona ununio
Mungu akiamua kukuumbua juu ya muumba wake hashindwi
 
Inawezekana serikali INAHUJUMIWA....

Iko siku hili litathibitika....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app

Serikali ina mkono mrefu sana ,tukio kama lile la watu waliojiamini kuteka basi na kuja kumtoa abiria ndani na mitutu kisha wakaondoka naye kwenda kumuua unadhani ni raia wa wakawaida? Unafikiri wangekuwa raia wa kawaida wangefika hata bahari beach bila kukamatwa?
 
Hili suala watu wangu wa ndani wananiambia si suala la muungano.
Ukitaka kuikosoa serikali vuka maji nenda zako Zanzibar.
Huku hamna mtu anayeguswa hata kidogo.
Huku wakosoaji hadi tunapewa Internet ya bure, asubuhi pia tunakunywa uni wa bure maeneo ya mnazi mmoja.
Akili mtu wangu.
 
kwanini haya yote yanafanyika kipindi hiki cha uchaguzi wa ndani wa chadema tu?

na kwanini wahusika wa songombingo ya kabokamchizi ni kwa watu wa chadema pekee?

nafasi ya mtoa taarifa hizi wa Chadema ni ipi hasa hata aonekane kama vile alikuepo wakati wa utekaji, lakini pia yupo kama vile alikua akishuhudia mwisho wa tukio na matokeo ya utekaji?

na mbona matukio haya yanaongezeka zaidi wakati wa uchaguzi wa ngazi ya juu chadema?🐒

Kwa hali hii,
kuna anaempinga mwezake chadema alie salama kweli?

nadhani kuna haja ya uchunguzi yakinifu chadema 🐒


Hivyo una ushahidi Chadema ndiyo wameajiri usalama wa taifa kumteka kiongozi wao tena mzee😂😂🤔🤔 . Bora unyamaze maana unajishusha sana next time kama ndiyo kipaji chako hivi na uelewa wa chini basi nitakuomba usichangie topic zangu maana ni aibu
 
Tujaribu kumrudisha jela kwa miezi kama mitatu tuangalie hali ya utekaji itaendeleaje
 
Hakuna nguvu ya dola iliyowahi ishinda nguvu ya umma.

Kumalizwa hatabila kuandamana watakumaliza tu kwani hao waliouawa na kumalizwa waliandamana?

Leo mzee wetu, hatujui kesho ni nani? Inaweza kuwa wewe au mimi. Bila kupiga kelele, tutakuwa kama kondoo mbele ya Fisi mkuu.

Tanzania ni
Nashauri, tuchange Hela, yatafutwe magaidi ya alshababu na sisi tuanza kuwatungua hao watekaji na hao waliowatuma kimya kimya, hii ndio dawa Yao fire by fire
 
Polisi wanavyokaa kimya wanaset negative precedent, matokeo yake wananchi wataanza kujichukulia sheria mkononi kwa mtu yoyote wanayemtilia shaka.

Ukisikiliza scene zote za utekaji unaona tu watu walikuja kiraia wakambeba mtu , huku watu wakibaki wanaangalia.

Mfano huyo waliomteka kwenye basi kama wananchi wangeamua kufunga basi na kusema hakuna kumchukua mtu je hao watekaji 4 wangeweza kumudu kuua watu wote 50+ kwa mkupuo?

Au polisi kutokana na kuchukua failures wengi ndio akili zimedumaa kabisa?
Kulaumu Polisi kwa ujumla, hapana...

Tatizo la Jeshi la polisi lipo kwa ma - Commanding Officers wao au maafisa wa juu wa Jeshi la Polisi IGP, MA - RPC nk ambao ndio wenye mamlaka na watoa amri na maelekezo kwa hawa walio chini.....

Hawa ndio wameoza kwa kuwa wamenunuliwa na kuwekwa kwenye mikono ya genge la wanasiasa walio madarakani kiasi cha maamuzi yao ku - abuse sheria na Katiba ya nchi. Mfano ni tukio la Mbeya juzi kwa polisi kupambana na vijana wa CHADEMA ktk mazingira ya uonevu kabisa na aliyeongoza Operesheni hiyo ni afisa mkubwa wa polisi Awadhi Haji....

Ukiona serikali ya nchi imejaa wizi na ufisadi wa fedha na Mali ya umma, jua kuwa fedha inayoibwa inakwenda ku - consolidate madaraka ya viongozi vya kisiasa walio madarakani kwa kuhonga na kuunda vikundi vya kigaidi na kuvifadhili Ili viteke na kuua wapinzani wa mabwana zao....!

Genge hili la wanasiasa hawa wa CCM walio madarakani mission yao kuu ni ya kisiasa - kuhakikisha kila aliye kinyume nao na anahatarisha uwepo wao madarakani anakwenda chini, anakufa......

Genge hili liko polisi, mahakamani, magerezani, bungeni....

Ukipigwa nje na kujifanya unaenda mahakamani, huko nako utawaluta na kamwe huwezi kupata haki yoyote...

Njia pekee iliyobaki kwa Sasa ni kumlilia na kumwomba Mungu wetu muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo atumie nguvu na mamlaka yake kupambana na watu hawa waovu waliokubali kutumiwa na shetani kutesa na kuua binadamu wenzao....

Alifanya hivyo kule Misri ya kale, Urumi ya kale, Babeli (Babylon) ya kale dhidi ya watu wa Mungu....

Hata Tanganyika anaweza....
 
Back
Top Bottom