TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Ajabu wote mlioko hapa mnaishia kulaani tu badala ya kutoa neno nini kifanyike kukomesha huu udhalimu;
Mimi ningependekeza ipangwe siku wananchi wote nchi nzima tuandamane kwenda kwenye ofisi za Serikali kulaani mauaji haya yanayoendelea.

Serikali itoa mwongozo na elimu kwa uwazi jinsi mtuhumiwa atakavyokamatwa na Polisi, na nje ya utaratibu huo, serikali itamke kuwa wananchi wajihami kwa namna yoyote ile kuhakikisha hakuna mtu anayetekwa.

Utaratibu huo usomwe kwenye mikusanyiko yoyote ile, iwe ni msikitini, kanisani, kwenye sherehe au mahali popote ambapo watu wanakusanyika.
 
Kuna haja ya kubadili Sheria za umiliki wa silaha ili Kila mwananchi mwenye akili timamu atembee na silaha kama ilivyo marekani ili kupambana na Hawa askari.Mzee kama huyu ambaye Hana madhara yeyote kiusalama wamemuua!yaani kosa tu kuwa mpinzani ndiyo unauliwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…