#COVID19 Dar: Askofu Ruwai’chi aagiza mapadri wote kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19

Kiunyenyekevu angetoa wito au ushauri mapadre wachanje sio Agizo! HAPANA!
 
Hawa jamaa ndiyo weupee hawana nguvu ya Mungu ujanja2 tu. Sijui kwanini wanaitwa baba!
 
Sawa, hongera kwa hilo ila chanjo ni hiari.
 
Wewe Muumini wa Father Nkwera tulia
 
Sema tu ni maagizo Toka Roma.
Wewe mwenyewe unajua ukweli hata ukichanjwa Corona itakuua tu.

Wafanyabiashara maarufu waliokufa karibuni kwa nature ya kazi zao,ni ukweli usiopingika kuwa walichanjwa lakini Israel amewapitia.
 
Uko disappointed wewe mwenyewe. Ruwaichi msimamo wake dhidhi ya Corona aliuweka wazi, Mpaka JPM akamnanga Kiaina.. Jamaa alishahimiza sana Tahadhari dhidhi ya covid kitambo.. Huu ni muendelezo
Usibishane na huyo mfuasi wa Kayafa Jiwe,anaendeleza upumbuvu wa Mwendazake.
 
Usilazimishe lisilokuhusu. Hapo anaongea na vijana wake. Yeye.kahamasisha na hajamsema mtu au hajamlazimisha mtu kuchanjwa. Mapadre ni waelewa sio wapenda sifa na ligi kuona Nani mshindi. Neno acha utoto maana yake ni umri ambao binadamu anaupenda sana. Ukiambiwa utoto unakasirika ujana unakasirika, uzee unakasirika, Sasa upo hatua gani mzee baba? Au upo hatua ya Masters katika hatua ya ukuaji.

Kwanza wanakushangaa kauli zako za kichochezi. Huwezi kugombanisha hii nyumba ni ngumu sana. Ogopa anaekusikiliza huku ameinamisha kichwa, akinyanyua kichwa na kukuangalia usoni utafute shimo haraka lakujificha.

Tusaidiane katika kumwondoa huyu mdudu atoweke.
 
Now, this is HUGE!
 
Anajua anayemtumikia, naye hanaga hiari bali lazima...neno linasema, ataonekana kama kondoo lakini anaongea kama joka...
Hakika tutawajua kwa matunda yao kama kweli kweli imo ndani yao. Binafsi nimeshangazwa na agizo hili. Lakini sitashangaa sana kutokana na matendo mengine ya nyuma, huu ni mwendelezo tu.
 
Reactions: Ame
katumwa huyo
 
🤣 🤣 🤣 🤣Mbona mnateseka sana mkisikia watu wanachanjwa? Wewe ni padri? Hili agizo linakuhusu?
 
Ukisikia kanisa la wasomi, kanisa la kweli ndilo hili sasa. Siyo hivi vibushuti vya kuokoteza vinavyojipachika uaskofu vinavyodanganya watu wakichanjwa watageuzwa ndondocha. Askofu ni kiongozi wa kanisa na ameshuhudi kwa macho yake jinsi mapadri wake waliathirika na UVIKO. Chanjo imekuja anawahimiza kuchanja, kuna ubaya huko ng'ambo kwenu?
 
ndio maana najua muda wowote nasepa ina kutegemea kwamba ukichanjwa ndio umekata tiketi ya kuishi huo ni use...nge wa kiwango cha rami
Nani alikudanganya ukichoma chanjo ya corona hufi?
 
Mapadre na watumishi wengi wa Kanisa, wapo katika kundi linalohudumia mamia ya watu.

Ni uamuzi mzuri na wa busara sana kama Mapadre watafuata muongozo wa Baba Askofu.
 
Kiunyenyekevu angetoa wito au ushauri mapadre wachanje sio Agizo! HAPANA!
Wewe hujui chochote kuhusu Kanisa katoliki. Toka lini askofu wa jimbo husika akatoa ushauri kwa mapadre wa jimbo lake. Siku zote askofu huwa anatoa 'maagizo' na sio 'ushauri' kwa walio chini yake.
Na kamwe haiwezi tokea wala haitokaa itokee chini ya jua akatokea 'Padre wa Kanisa katoliki' akampinga 'Askofu wa kanisa katoliki' HADHARANI.
Narudia haijawah tokea na wala haitokaa itokee padre ampinge Askofu wa jimbo lake. Ndivyo ilivyo na itabaki kuwa hivyo. Wamefunzwa nidhamu ya hali ya juu miaka yao yote wakiwa seminari ndogo mpaka seminari kuu.
Migogoro itabaki ndani ya madhehebu madogo madogo au taasisi nyingine lakini si ndani ya Kanisa Katoliki. Askofu Awe amekosea au awe hajakosea itabaki kuwa maoni kwako na kwa wengineo ila kwa Mapdre watatii amri yake na maisha yataendelea. Hutokaa usikie malumbano au mgogoro wa aina yoyote ile kwa kanisa katoliki. Ndo imetoka hiyo. Ni suala la nidhamu. Agizo limetoka na litatekelezwa na Mapadre wote walio chini yake. Malumbano yatabaki kwa kina Gwajima lakini si kwa Kanisa katoliki
 
Fuatilia mambo mkuu.

Papa alishashauri na alishasisititiza watu wachanjwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…