#COVID19 Dar: Askofu Ruwai’chi aagiza mapadri wote kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19

#COVID19 Dar: Askofu Ruwai’chi aagiza mapadri wote kupata chanjo dhidi ya UVIKO-19

Kwanini unafikiri napinga chanjo? Wewe kachanje, mimi ni kama waberoya ...kama huwajui nenda kafatilie walipokeaje imani! Sifati ulimwengu kiboya.
Sasa ndo uanataka mapadre wafate uboya wako ambao hauko guided na wisdom?
 
huyo wa mabatini ana PHD ww apo ni LY ..

ma askofu wanaongoza kuwa ingilia watoto wadogo na kuficha watoto....Sioni askofu alosoma apo , anaongea utumbo na ww unaongea mavi
PhD ya uzinifu na utapeli labda!! Usimfananishe Ruwai'chi na vitu vya kijinga
 
Kwani Papa akisema inabidi nifate? Kasome vizuri katekisimu ili ujue Papa akisema nini unapaswa kufata, sembuse Askofu!
Nimemzungumzia Pope kwa sababu wewe ulikuwa unamwingiza kwenye argument zako za kijinga,argument yoyote ambayo ni unfounded ni ya kijinga.
 
View attachment 1906131
PICHA: Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi

Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Tadheus Ruwai’chi ameagiza mapadri wote wa jimbo hilo kupata chanjo dhidi ya Uviko 19 kwa kuwa ugonjwa huo unaumiza na kuondoa uhai.

Ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 24, 2021 katika adhimisho la Misa Takatifu ya kumuombea Padri Paul Haule aliyekuwa Paroko Msaidizi katika Parokia ya Mtakatifu Petro na Mkurugenzi wa Tumaini Media.

Ruwai’chi amesema mwaka 2020 wakati wa awamu ya kwanza ya janga la Uviko-19 watu walimuomba Mungu ajaalie kupatikana kwa chanjo, ambayo sasa imepatikana.

“Tulimuomba Mungu ajaalie kupatikana kwa chanjo sasa imepatikana badala ya kutumika watu wameingia katika malumbano ya kusema haya na yale dhidi ya chanjo,” amesema.

“Tusingojee hadi mambo haya yatutinge, tutumie vizuri fursa alizotupa Mungu kujikinga na kujihami na kwa sababu hiyo, sijui ni mapdri wangapi ambao mmeshachanjwa, lakini leo naomba nitoe agizo, kila padre akachanjwe, kila padre akachanjwe, tusifanye utoto, tusifanye lelemama, hii uviko 19 haina mjomba na shemeji na inatuondolea uhai,” amesema Ruwai’chi

Amesema ni utashi wa Mungu kwa watu wawe hai na kuwa na uhai tele hivyo ni vyema kuujali uhai waliopewa.

“Tujihami na tuendelee kumuomba Mungu, atuhurumie na tujihami na atuondolee hili janga,” amesema Ruwai’chi.

Mwananchi

Amekula maharage ya wapi huyu?

Chanjo ni hiari ya mtu na hana mamlaka ya kuwalazimisha ila kuwasihi waone umuhimu wa kuchanjwa kama sehemu ya kuwalinda wengine.
 
Usiaminishe watu ujinga
The Vatican is taking Pope Francis’ pro-vaccine stance very seriously: Any Vatican employee who refuses to get a coronavirus shot without a valid medical reason risks being fired.

A Feb. 8 decree signed by the governor of the Vatican city-state says that employees who opt out of vaccination without a proven medical reason could be subject to a sanction up to and including “the interruption of the relationship of employment.”

The directive cited the need to protect Vatican employees in the workplace, as well as guidelines issued by Francis’ advisory COVID-19 commission, which said individuals have a moral responsibility to get vaccinated “given that refusing a vaccine can constitute a risk for others.”
Mtu akigoma kuchanja atafukuzwa kazi lakini si kufungiwa sakramenti! Kwahiyo hizo hadithi haziwezi kunifanya niamini Vatican ndio utakatifu wenyewe. Tunalijua Kanisa ndio maana pamoja na makandokando yake tumebakia imara.

Sasa wewe si unashabikia Vatican kusema chanjo lazima kwa wafanyakazi wake? Vipi ukipata dossiers za uchafu wa kutisha pale? Utaambatana na huo uchafu? Upo mstari kati ya mafundisho ya Kanisa na maamuzi ya kibinadamu. Nimepewa akili, swala la chanjo nimeamua kuwa kama Waberoya, hao hawakugomea imani bali waliikubali baada ya kuchunguza maandiko.
 
Kwanini unafikiri napinga chanjo? Wewe kachanje, mimi ni kama waberoya ...kama huwajui nenda kafatilie walipokeaje imani! Sifati ulimwengu kiboya.
Naona watu wanakushambulia na matusi juu!
Lakini kwa uzito wa hoja umewatupa mbali, hii inaonyesha tofauti ya uelewa ukichangiwa na ushabiki ndani yake.
 
Kanisa katoriki ni taasisi imara na inayoongozwa kwa weledi wa hali juu. Tuliosoma seminary tunafahamu hilo na ndio chombo pekee kilichoonesha msimamo wakati wa vituko vya awamu ya tano. Tuna shida sana kwenye educational program zetu zinatoa half cooked personnel. Haiwezekani na kituko cha dunia watu kuendeshwa na hisia kiasi kile yaani. It is impossible to move a mountain by say '' mountain go" haiwezi kutokea. Itoshe kusoma kongole kwa baba askofu na taasisi yako
Kabisa
 
PhD ya uzinifu na utapeli labda!! Usimfananishe Ruwai'chi na vitu vya kijinga
Tanzania imejaa ujinga tu, watu wanashindwa kung'amua mambo na kuwa na uelewa wa dunia inapoelekea-CORONA imeanza kuchukuliwa kama pandemic na hvyo haitaisha leo wala kesho,na hvyo nchi nyingi zimeshaanza kuifanya chanjo kama lazima na si hiyari-Hata china na ukomunisti wao-Nchini mwao huingii bila chanjo.Vatican yenyewe imepitisha decree inayowataka wafanyakazi wake wachanjwe-mtu asipochanjwa hana kazi.
 
Naunga mkono hoja
Kuna wakatoliki uchwara humu ndani wanakuja na kumuhusisha pope Francis ili kutetea ujinga,Kiufupi hata Pope francis kapitisha decree-kila mfanyakazi Vatican lazima achanje-usipochanja kazi hakuna.wanasema hakuna hiyari ya mtu kwenye kuambukiza wengine
 
Nimemzungumzia Pope kwa sababu wewe ulikuwa unamwingiza kwenye argument zako za kijinga,argument yoyote ambayo ni unfounded ni ya kijinga.
Hujaelewa ndugu, hilo ni agizo kwa wafanyakazi wa Vatican haina mahusiano na imani ndio maana hakuna agizo la kiulimwengu.

Ndio maana nimesema hotuba za Papa ni ushauri kwa waamini na macleri sio agizo. Tambua nafasi za papa akiwa Vatican.
 
Kuna wakatoliki uchwara humu ndani wanakuja na kumuhusisha pope Francis ili kutetea ujinga,Kiufupi hata Pope francis kapitisha decree-kila mfanyakazi Vatican lazima achanje-usipochanja kazi hakuna.wanasema hakuna hiyari ya mtu kwenye kuambukiza wengine
Nani aliyekuambia kwamba mtu akichanja hawezi kuambukiza wengine?...
 
Hujaelewa ndugu, hilo ni agizo kwa wafanyakazi wa Vatican haina mahusiano na imani ndio maana hakuna agizo la kiulimwengu.

Ndio maana nimesema hotuba za Papa ni ushauri kwa waamini na macleri sio agizo. Tambua nafasi za papa akiwa Vatican.
Kwa akili yako Mapadre,Makleri siyo watumishi wa kanisa?
 
Nani aliyekuambia kwamba mtu akichanja hawezi kuambukiza wengine?...
Science inasema mtu akiwa vaccinated anaweza ambukiza wengine-lakini ili kupunguza risks kwa jamii kiujimla na kuweza ku-contain huu ugonjwa-Ni lazima kuwe na international efforts za kuhakikisha watu wote wanakuwa vaccinated.Science inasema ni lazima tuchanje na pia tuvae barakoa for the mean time ambapo wengine wengi bado hawajachanja hasa wazee.
 
Back
Top Bottom