DAR: Barabara 9 kufungwa kwa siku sita kupisha mkutano wa madini chini ya Viongozi kadhaa wa Afrika

DAR: Barabara 9 kufungwa kwa siku sita kupisha mkutano wa madini chini ya Viongozi kadhaa wa Afrika

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam imetangaza kuwa Barabara tisa Jijini Dar es Salaam, zimefungwa kwa siku sita kuanzia leo Januari 25 hadi Januari 30, 2025 ili kupisha misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati Afrika.

Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Januari 25,2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema Mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi Januari 28, 2025, unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya marais 25 na mawaziri 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo pia bajaji na bodaboba hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji katika kipindi chote ambacho mkutano huo utakuwa ukifanyika.

Barabara zitakazofungwa ni pamoja na Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu; Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo

Zingine ni Barabara ya Bibi Titi kutokea makutano ya barabara za Ohio na Ally Hassan Mwinyi kwenda Hoteli ya Crowne; Barabara ya Azikiwe kwenda Hoteli ya Four Points, Hoteli ya Golden Tulip City Center na Hoteli ya Holiday Inn; Barabara ya Morogoro kutokea Sokoine kwenda Hoteli ya Tiffany No. 1; Barabara ya Makunganya kutokea Azikiwe kwenda Hoteli ya Tiffany No. 2 na Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC.

sisi wa Mandela na Kawawa tuendelee kugonga glass🥂

#KitengeUpdates
Bora zote za hukohuko Posta
 
Tanzania inabidi waupange vizuri mji wa dodoma ufae kwa ajili ya mikutano ya kimataifa. Pawe na barabara nyingi zinazofaa kwa ajili ya mikutano. Pawe na airport kubwa, viwanja vipimwe vizuri na viuzwe kwa bei ndogo. Pawe na maeneo ya mahoteli na pawe na maeneo ya kumbi kama 5 au 10 za mikutano ya kimataifa



Dar ni mji mdogo na haujapangwa kwa ajili ya wageni wa kimataifa. Ndio maana barabara zinafungwa tu.
 
Nchi masikini ni masikini tu, hivi wamefikiria adha tutakayoipata wananchi? Barabara kuu zifungwe kwa siku 9? Sitaki kuamini ninachokisoma.
 

Attachments

  • 1728759764686.jpg
    1728759764686.jpg
    154.8 KB · Views: 1
Back
Top Bottom