Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,912
- 12,904
Duh aisseDuh aiseee kutesa wananchi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh aisseDuh aiseee kutesa wananchi
Yaani hii moja tu ni tatizo. Watu wa Goms sijui wataendaje makazini.
Bora zote za hukohuko PostaJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam imetangaza kuwa Barabara tisa Jijini Dar es Salaam, zimefungwa kwa siku sita kuanzia leo Januari 25 hadi Januari 30, 2025 ili kupisha misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati Afrika.
Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Januari 25,2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema Mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi Januari 28, 2025, unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya marais 25 na mawaziri 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo pia bajaji na bodaboba hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji katika kipindi chote ambacho mkutano huo utakuwa ukifanyika.
Barabara zitakazofungwa ni pamoja na Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu; Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo
Zingine ni Barabara ya Bibi Titi kutokea makutano ya barabara za Ohio na Ally Hassan Mwinyi kwenda Hoteli ya Crowne; Barabara ya Azikiwe kwenda Hoteli ya Four Points, Hoteli ya Golden Tulip City Center na Hoteli ya Holiday Inn; Barabara ya Morogoro kutokea Sokoine kwenda Hoteli ya Tiffany No. 1; Barabara ya Makunganya kutokea Azikiwe kwenda Hoteli ya Tiffany No. 2 na Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC.
sisi wa Mandela na Kawawa tuendelee kugonga glass🥂
#KitengeUpdates
Utapunguza gharama ya gesi na kuuia kabisa matumizi ya kuni na mkaa kama nishatiHuo mkutano una tija gani kwa Taifa?
Upigaji tuHuo mkutano una tija gani kwa Taifa?
Yaani hii moja tu ni tatizo. Watu wa Goms sijui wataendaje makazini.
huruma😂😂Yaani hii moja tu ni tatizo. Watu wa Goms sijui wataendaje makazini.
Nchi masikini ni masikini tu, hivi wamefikiria adha tutakayoipata wananchi? Barabara kuu zifungwe kwa siku 9? Sitaki kuamini ninachokisoma.
mtu hata hajaamka mshapigwa foleniSasa hii ndo Tanzania.
Ndomaana hata msafara wa Kiongozi nchini, utakuta barabaraninafungwa Masaa matano ndo MTU anapita.