DAR: Barabara 9 kufungwa kwa siku sita kupisha mkutano wa madini chini ya Viongozi kadhaa wa Afrika

DAR: Barabara 9 kufungwa kwa siku sita kupisha mkutano wa madini chini ya Viongozi kadhaa wa Afrika

Njia badala zipo nyingi wangefunga behewa za kutosha kwenye treni kwa kipindi hiki, njia ambazo hazitumiki mara kwa mara zikisawazishwa wasio zijua watazijua
 
Kwa lugha nyingine wangesema tu CBD imefungwa maana kwa barabara walizozitaja ni kama kuingia mjini na magari itakuwa haiwezekani ikichukulia kuna njia nyingine za kuingia mjini zimeshafungwa sababu ya ujenzi wa BRT...

Nashauri tu mtu kama una ndinga na unataka kufika mjini, tafuta parking maeneo ya jirani kama Upanga, Lumumba then uingie town kwa ama mwendokasi au kutembea...
 
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam imetangaza kuwa Barabara tisa Jijini Dar es Salaam, zimefungwa kwa siku sita kuanzia leo Januari 25 hadi Januari 30, 2025 ili kupisha misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati Afrika.

Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Januari 25,2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema Mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi Januari 28, 2025, unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya marais 25 na mawaziri 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo pia bajaji na bodaboba hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji katika kipindi chote ambacho mkutano huo utakuwa ukifanyika.

Barabara zitakazofungwa ni pamoja na Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu; Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo

Zingine ni Barabara ya Bibi Titi kutokea makutano ya barabara za Ohio na Ally Hassan Mwinyi kwenda Hoteli ya Crowne; Barabara ya Azikiwe kwenda Hoteli ya Four Points, Hoteli ya Golden Tulip City Center na Hoteli ya Holiday Inn; Barabara ya Morogoro kutokea Sokoine kwenda Hoteli ya Tiffany No. 1; Barabara ya Makunganya kutokea Azikiwe kwenda Hoteli ya Tiffany No. 2 na Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC.

sisi wa Mandela na Kawawa tuendelee kugonga glass🥂

#KitengeUpdates
 

Attachments

  • 20250107_214111.jpg
    20250107_214111.jpg
    139 KB · Views: 1
Nchi masikini ni masikini tu, hivi wamefikiria adha tutakayoipata wananchi? Barabara kuu zifungwe kwa siku 9? Sitaki kuamini ninachokisoma.
Kuna mtu humu ndani aliwahi kusema kwenye zile evolution of man, Mtanzania alikomea kwenye hatua moja kabla ya kuwa binadamu kamili.

Ni maneno makali ila ukiyatafakari na yanayoendelea hapa nchi unaweza ukakubaliana nae.
 
Na huyu Dogo atakuwepo?
 

Attachments

  • Burkina-Faso-apres-avoir-suspendu-Air-France-Ibrahim-Traore-frappe-fort-et-fait-une-annonce-re...jpg
    Burkina-Faso-apres-avoir-suspendu-Air-France-Ibrahim-Traore-frappe-fort-et-fait-une-annonce-re...jpg
    62.3 KB · Views: 2
Kifupi shuka kariakoo tembea kwenda ofcn kwko,,kumbuka kubeba kitambulisho Cha kazi na Cha NIDA
Mpaka unafika kariakoo utakuwa umetumia usafiri gani? Maana foleni ya kuingia kariakoo Kwa hizo barabara Ambazo zitafungwa zipo karibu yake...
Kwa Sisi wabangaizaji tutaingia kariakoo SAA 5 na tutaondoka usiku Sana kuanzia SAA 3, poleni nyie wa maofisini
 
Mpaka unafika kariakoo utakuwa umetumia usafiri gani? Maana foleni ya kuingia kariakoo Kwa hizo barabara Ambazo zitafungwa zipo karibu yake...
Kwa Sisi wabangaizaji tutaingia kariakoo SAA 5 na tutaondoka usiku Sana kuanzia SAA 3, poleni nyie wa maofisini
We utajua utumie usafiri Gani kufika ofcn kwako
 
Na kitu wanachoenda ongelea eti waTanzania 8.5M, JPM aliwezesha watu kupata umeme uko vijijini na hakuna kukatika, ukikatika Manager husika na wewe unakatika, bila mkutano wa wakuu wa nchi umeme ulienea, naweza kusema kijijini Kwetu tulikuwa wanufaika wa mpango huu.

Kutoka Airport Kwa Sasa kuna njia ya Mwendo kasi iliyo kamilika Kwa karibu 95% Kwa nini wasitumie hiyo na waweke vizuizi kuhakikisha hakuna gari binafsi linapita huko hasa hizi zenye namba PT, STK, SU, RAC, DFP, JW, STN, na wale waajiriwa kutoka hizo ofisi, maana ndio magwiji wa kuvunja Sheria za barabarani Kwa kisingizio Cha maagizo ya boss.

Naamini kwanza viongozi wote wa juu magari yao yanausalama wa hariali ya juu kabisa. Wewe ukiwa na gobore lako utapiteq mapema tu.
 
Back
Top Bottom