Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam imetangaza kuwa Barabara tisa Jijini Dar es Salaam, zimefungwa kwa siku sita kuanzia leo Januari 25 hadi Januari 30, 2025 ili kupisha misafara ya viongozi wanaokuja kutoka nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano wa Nishati Afrika.
Taarifa ya Polisi iliyotolewa leo Jumamosi Januari 25,2025 na Kamanda Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Jumanne Muliro, imesema Mkutano huo utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 27 hadi Januari 28, 2025, unatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya marais 25 na mawaziri 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo pia bajaji na bodaboba hazitaruhusiwa kuingia katikati ya Jiji katika kipindi chote ambacho mkutano huo utakuwa ukifanyika.
Barabara zitakazofungwa ni pamoja na Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu; Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena na Barabara ya Ghana kutokea barabara ya Ohio kwenda Hoteli ya Onomo
Zingine ni Barabara ya Bibi Titi kutokea makutano ya barabara za Ohio na Ally Hassan Mwinyi kwenda Hoteli ya Crowne; Barabara ya Azikiwe kwenda Hoteli ya Four Points, Hoteli ya Golden Tulip City Center na Hoteli ya Holiday Inn; Barabara ya Morogoro kutokea Sokoine kwenda Hoteli ya Tiffany No. 1; Barabara ya Makunganya kutokea Azikiwe kwenda Hoteli ya Tiffany No. 2 na Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun pamoja na Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNICC.
sisi wa Mandela na Kawawa tuendelee kugonga glass🥂
#KitengeUpdates
Dodoma hao wageni tuyawalaza wapi???Huu mkutano ulitakiwa ufanyikie Dodoma!
Dar itakuwa vurugu sana!
kwamba mantilie wa pale kigogo na mburahati nae atumie gas? labda serikali ipunguze kodiUtapunguza gharama ya gesi na kuuia kabisa matumizi ya kuni na mkaa kama nishati
tegemea nauli za daladala kuongezekaWatapitia Majumba 6 kwenda Tabata kisha Mandela Road, Ilala, n.k.
Ndio, sio mama Ntilie tu...hata mashuleni na majeshinikwamba mantilie wa pale kigogo na mburahati nae atumie gas? labda serikali ipunguze kodi
mara zote foleni hapa dar zinasabishwa na baadhi madereva kwa uzembe wao au kuharibika magari lkn endapo trafiki wakipangwa vyema hakutakua na folenDuh! Na huu mji ilivyo na foleni sasa hizo zikifungwa siitakuwa balaa
umeambiwa upite ile barabara ya vumbi inayotumika na mkandarasi wa rel ya sgrYaani hii moja tu ni tatizo. Watu wa Goms sijui wataendaje makazini.
Kuleni chuma hicho. Sisi tunalima mihogo huku mikutano yenu.Hawa jamaa kwanini wasiwe wanafanyia mikutano yao mikoani tena kwenye HOTEL zilizo Nje ya miji? Ya nini kuwaletea KERO watu?
Kuna mtu humu ndani aliwahi kusema kwenye zile evolution of man, Mtanzania alikomea kwenye hatua moja kabla ya kuwa binadamu kamili.Nchi masikini ni masikini tu, hivi wamefikiria adha tutakayoipata wananchi? Barabara kuu zifungwe kwa siku 9? Sitaki kuamini ninachokisoma.
Kabisaa mkuuAliyesema Dar ni Jiji, aliwadanganya!
Hakuna Jiji la aina hiyo Duniani
Mpaka unafika kariakoo utakuwa umetumia usafiri gani? Maana foleni ya kuingia kariakoo Kwa hizo barabara Ambazo zitafungwa zipo karibu yake...Kifupi shuka kariakoo tembea kwenda ofcn kwko,,kumbuka kubeba kitambulisho Cha kazi na Cha NIDA
We utajua utumie usafiri Gani kufika ofcn kwakoMpaka unafika kariakoo utakuwa umetumia usafiri gani? Maana foleni ya kuingia kariakoo Kwa hizo barabara Ambazo zitafungwa zipo karibu yake...
Kwa Sisi wabangaizaji tutaingia kariakoo SAA 5 na tutaondoka usiku Sana kuanzia SAA 3, poleni nyie wa maofisini