Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Watu kadhaa wanasadikiwa kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa, kufuatia ajali iliyotokea maeneo ya Mbezi Luguluni, ikihusisha Basi la kampuni ya Burudani, lililokuwa likitokeaa mkoani Tanga kuelekea Dar es Salaam, ambapo basi hilo linadaiwa kuwa lilikuwa kwenye mwendokasi, hivyo wakati likijaribu kulikwepa gari dogo lililokuwa linaingia barabarani, likapoteza mwelekeo na kuhamia upande wa pili wa barabara na kugonga daladala na bodaboda.