Dar: Basi la Burudani kutoka Korogwe Tanga, lapata ajali Mbezi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Watu kadhaa wanasadikiwa kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa, kufuatia ajali iliyotokea maeneo ya Mbezi Luguluni, ikihusisha Basi la kampuni ya Burudani, lililokuwa likitokeaa mkoani Tanga kuelekea Dar es Salaam, ambapo basi hilo linadaiwa kuwa lilikuwa kwenye mwendokasi, hivyo wakati likijaribu kulikwepa gari dogo lililokuwa linaingia barabarani, likapoteza mwelekeo na kuhamia upande wa pili wa barabara na kugonga daladala na bodaboda.
 
Watu wanapoteza maisha kwasababu ya uzembe na upumbavu wa madereva. Umeshafika Dar unakimbilia wapi??

Hii ni tabia ya madereva wengi wa mabasi. Na kwa bahati mbaya mengi ya makampuni ya mabasi yanamilikiwa na wanasiasa au marafiki wa wanasiasa, kwahiyo polisi wanawaogopa.

Enzi za JPM polisi wakifanya kazi yao kwa uhuru kwakuwa pale juu alikuwepo mtu asiyetaka mazoe ya kijinga. Kwasasa uswahiba umerudi.
 
Bila kujua chanzo wapumbavu wanaropoka
 

Wa daladala lazima wamefariki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…