Dar: Conrad Agonza Kayoza aliyeshambuliwa na Trafiki, kufikishwa mahakama ya Kinondoni leo

Dar: Conrad Agonza Kayoza aliyeshambuliwa na Trafiki, kufikishwa mahakama ya Kinondoni leo

Ila kina Bishanga kwa mataizi?? Hapa ilibidi tujue daktari ni jirani yako bush 😂😂
Huo ni mtazamo wako tu hatuwezi kuupinga make akili dhaifu udeal na kujadili mambo kama Yako hayo.
Ila nilitaka kumuelezea tu ndg aliyesema Dr anaenda kuozea jela nikajaribu kumcholea hali ya maisha pale kwao sio mtu wa kuozea jela. Sasa kama namfahamu nisiseme jamani.

wewe kama una mtazamo huo ni jambo jema. Na nakuongezea na wewe ana kaka yake anaitwa Dr (PhD) Bravius Kahyoza ni mchambuzi wa uchumi pale azam TV napo vimba upasuke
 
Comment yangu hii moja ndio imekupa taswira nina akili dhaifu bojo? Acha ushamba hatujuani nyuma ya keyboard usichukulie poa
 
Akishafikishwa Mahakamani tutajua anasomewa mashitaka gani. Litakuwa shitaka la shambulio na atapewa dhamana. Sema kapigwa sana kituoni na kaumizwa sehemu mbalimbali. Je, waliompiga watamlipa? Sababu hawakuwepo sehemu ya tukio
Mbona kwenye video hatumuoni na majeraha?
 
Atafungua dispensary yake, sio lazima aajiriwe. Kila mtu anajua athari za kujitoa muhanga lakini haya mamno ili yaishe lazima wachache wakubali hizo shuruba. Bila shaka hata huyu trafiki hawezi tena kurudia tabia yake ya kufokea watu wazima kama watoto na kuchomoa funguo ya gari. Polisi nao wajue binadamu sisi kama walivyo wanyama wengine. Tukifika mwisho wa uvumilivu akili ina-activate jungle mood.

Kingine cha kukiangalia hapa ni wabongo wanavyosogea hatua kwa hatua kukata ile dhana uliyoaminika kwamba ni waoga. Tulianza na maandamano. Wabongo kunguru hakuna atakaetoka watu walitoka. Wakapigwa risasi. Sasa hivi yakiitishwa maandamano polisi wanatumika kutoa vitisho. Dokta kagoa somo hawa jamaa 1 vs 1 hawana kitu. Imebaki hatua moja tu, nayo ni raia kupata silaha za moto

hata mimi ni pro maandamano niko tayari hata kesho, nimechoka na kuchoshwa kabisa na ccm na ningependa iondoke hata leo hii kwanza nikisikia imejiuzulu sasa hivi hiyo furaha siwezi kuilezea lkn pia hilo bado haliniondolei uwezo wa kuangalia mambo kiuhalisia zaidi klk jazba, jazba huondoa uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.

hakupaswa kumshambulia na kumpiga trafiki hilo ni kosa kisheria na hata ukiacha mambo ya trafiki kuchukua tu uamuzi kumpiga mtu mwingine bado tu kosa kisheria, hata tu wanaoipiga wake zao bado wanavunja sheria na wanaweza pia kukamatwa kwa kosa la kumpiga mke wake kwa maana hairuhusiwi kupiga binadamu mwingine.

ndiyo maana nashindwa kuelewa iweje watu ambao wanalilia haki na utawala wa sheria kila siku hata waki-demand katiba mpya (nikiwemo kwenye kundi la wanaotaka katiba mpya) wakimtetea mtu kama huyu, sielewi kwa kweli ...
 
Nilijua mpaka huyo Conrad kafikia hatua ya kumpiga askafi kwa Tz hii, basi hayupo kinyonge mfukoni au familia yake.
Screenshot_20260910-170600.png

Kuna chawa wameumia hapo,hawajui tu mfumo uliopo unawabeba walio nacho,unakuta chawa povu linamtoka sababu ya buku 7 ya posho,dr mfumo umembeba sababu ya elimu yake ila hii ni haki ya kila raia,lile tukio angefanya mtu hoe hoe saa hizi tushamsahsu
 
he is done, anaenda jela kwa ujinga tu, tanzagiza kila mtu anataka kupiga, kama alikuwa na familia ndiyo hivyo tena.

next time hata wewe yanaweza kukuta, usijukulie sheria mkononi hata kama tanzagiza tunaishi kwa mazoea lkn sheria zipo, kosa kubwa sana kumshambulia na kumpiga law enforcement akiwa kazini kutekeleza majukumu yake, hakuna jinsi anaweza kuchomoka, swali linabakia was it worth it?

kuharibu career yako uliyoisotea kwa tabu na gharama kubwa and all came down to one moment ambapo angeweza kujizuia tu, sasa hata akija kutoka jela udaktari bingwa umeshayeyuka, hakuna atakayeweza kuajiri mtu aliyewahi kuhukumiwa na kufungwa jela, its sad lkn ndiyo hivyo, imeisha hiyo ...
Screenshot_20260910-170600.png

Chawa maumivu yake hapo ulipo ayaelezeki
 
View attachment 3667766
Chawa maumivu yake hapo ulipo ayaelezeki

oh nani sasa unamuita chawa? ishakuwa yanga vs simba sasa? kwa hiyo haturuhuswi kujadili mada na kutoa maoni yetu kwa jinsi tunavyoona bila ya kuwekwa upande na kupewa labels? kama amepata dhamana its good for him na nafikiri labda atatumia muda uliopo kufanya tafakari ya yalioyotokea kama ulikuwa ni uamuzi sahihi au la, sisi wengine tunaandika coments tu ...
 
Habari Wakuu

Leo tarehe 10.09.2026 majira mchana mtuhumiwa aliyeshambuliana na askari traffic maeneo ya Mwnge jijini Dar, atafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni, Dar es Salaam.

Kumbuka Jeshi la Polisi Dar es Salaam linamshikilia Conrad Agonza Kayoza, miaka 35, kwa tuhuma za kumshambulia kwa ngumi na mateke Askari Polisi wa Usalama Barabarani, F. 8886 SGT Andrew, katika eneo la Lugalo, Kinondoni, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea Septemba 8, 2026 majira ya saa 1:30 asubuhi kwenye Barabara ya Bagamoyo.

Kumbuka huyu Trafiki alichomoa ufunguo wa gari na kumzuia Daktari kuendelea na safari.

Mtuhumiwa alikuwa anawahi mufanyia Operation mgonjwa Hospitalini ila trafiki hakutaka kuelewa. Ndipo katika kunyang'anyana ufunguo, ugomvi ukatokea. Mmoja anataka Rushwa, mwingine anataka kuokoa uhai wa mtu.

Soma

Aliweza kumthibitishia Askari Traffic Andrew kuwa anamuwahi mgonjwa? Kama utanijibu, uzingatie kuwa alikuwa kwenye private car na alitakiwa kuzingatia kanuni zote za barabarani!
 
View attachment 3667745
Kuna chawa wameumia hapo,hawajui tu mfumo uliopo unawabeba walio nacho,unakuta chawa povu linamtoka sababu ya buku 7 ya posho,dr mfumo umembeba sababu ya elimu yake ila hii ni haki ya kila raia,lile tukio angefanya mtu hoe hoe saa hizi tushamsahsu
Wallah,asingetoka mtu,, maana mahakimu wa jf walisema mengi,mara atafutwa KAZI,mara atafungwa maneno kibao.
 
Ndio. Hata kabla hajafukishwa mahakamani nilimuona
Good! Na kwasababu wewe ni "akili kubwa" kumshambulia askari, kumpiga, kumjeruhi na kumfanya kushindwa kutekeleza majukumu yake ni sahihi kwasababu tu "the allegedly doctor" alikuwa anawahi mgonjwa hospitali sio?
 
Habari Wakuu

Leo tarehe 10.09.2026 majira mchana mtuhumiwa aliyeshambuliana na askari traffic maeneo ya Mwnge jijini Dar, atafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni, Dar es Salaam.

Kumbuka Jeshi la Polisi Dar es Salaam linamshikilia Conrad Agonza Kayoza, miaka 35, kwa tuhuma za kumshambulia kwa ngumi na mateke Askari Polisi wa Usalama Barabarani, F. 8886 SGT Andrew, katika eneo la Lugalo, Kinondoni, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea Septemba 8, 2026 majira ya saa 1:30 asubuhi kwenye Barabara ya Bagamoyo.

Kumbuka huyu Trafiki alichomoa ufunguo wa gari na kumzuia Daktari kuendelea na safari.

Mtuhumiwa alikuwa anawahi mufanyia Operation mgonjwa Hospitalini ila trafiki hakutaka kuelewa. Ndipo katika kunyang'anyana ufunguo, ugomvi ukatokea. Mmoja anataka Rushwa, mwingine anataka kuokoa uhai wa mtu.

Soma

CHADEMA tuichukue hii ni ajenda nzuri watanzania watatuelewa ,EU na USA mpaka kieleweke.
 
Back
Top Bottom