Habari Wakuu
Leo tarehe 10.09.2026 majira mchana mtuhumiwa aliyeshambuliana na askari traffic maeneo ya Mwnge jijini Dar, atafikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kinondoni, Dar es Salaam.
Kumbuka Jeshi la Polisi Dar es Salaam linamshikilia Conrad Agonza Kayoza, miaka 35, kwa tuhuma za kumshambulia kwa ngumi na mateke Askari Polisi wa Usalama Barabarani, F. 8886 SGT Andrew, katika eneo la Lugalo, Kinondoni, Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea Septemba 8, 2026 majira ya saa 1:30 asubuhi kwenye Barabara ya Bagamoyo.
Kumbuka huyu Trafiki alichomoa ufunguo wa gari na kumzuia Daktari kuendelea na safari.
Mtuhumiwa alikuwa anawahi mufanyia Operation mgonjwa Hospitalini ila trafiki hakutaka kuelewa. Ndipo katika kunyang'anyana ufunguo, ugomvi ukatokea. Mmoja anataka Rushwa, mwingine anataka kuokoa uhai wa mtu.
Soma