Dar: Conrad Agonza Kayoza aliyeshambuliwa na Trafiki, kufikishwa mahakama ya Kinondoni leo

Tandika Dr!
 
Good! Na kwasababu wewe ni "akili kubwa" kumshambulia askari, kumpiga, kumjeruhi na kumfanya kushindwa kutekeleza majukumu yake ni sahihi kwasababu tu "the allegedly doctor" alikuwa anawahi mgonjwa hospitali sio?
Aliyemwambia achomoe funguo nani, tandika huyo!
 
Wanauzi Hawa traffic,siku Moja nipo na mgonjwa hoi,anaanza upuuzi puuzt!
 
Kuna sababu gani hasa ya kuwa na maaskari barabarani kwenye karne hii ya sayansi na teknolojia.

Ni njia ya ccm kuwafanyia polisi fadhila ili wapate mwanya wa kujiongezea kipato kwa njia ya kula rushwa mabarabarani wakishukuru kwa namna polisi wanavyowasaidia kuhujumu chaguzi.

Uwepo wa maaskari barabarani haupunguzi ajali ni kula rushwa tu kwa kwenda mbele.
 
Kwa nini mahabusu siku 3 na isiwe Kesho Yake au siku Ile Ile, au Kesi take ni ya ugaidi na kutaka kuchoma vituo vya Polisi
 
Hata wake Majaji Wanao Tanua kuwahi Mahakamani ni wazembe
 
Jazba ni kitu cha papo kwa hapo. Dokta hakutoka tu nyumbani kwake akiwa na lengo la kutembeza kichapo kwa trafiki atakaekutana nae barabarani. Alichokifanya dokta ni kama tu hayo maandamano unayosema unayaunga mkono. Kila mtu ana kikomo cha uvumilivu. Kila mtu ana insanity spot yake, ukii-trigger hatoangalia wewe ni nani. Polisi wafundishwe kazi pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…