Dar: Dunstan Daudi Mutajura adaiwa kutekwa eneo la Buza

Dar: Dunstan Daudi Mutajura adaiwa kutekwa eneo la Buza

Tanzania hakuna utekaji wa kutaka ransom, ni watu wa TISS na kitengo maalum ndani ya polisi ndiyo huusika na utekaji. The 'protected' motherfvckers na ndiyo maana huwa wanateka openly kwa kujiamini sana, wangeshambuliwa na kuuawa ungesikia ni TRA or anything else similar to that kwamba waliowauwa wakamatwe(na wangekamatwa tu) na blah blah blah blahs kibao kuhalalisha utekaji na uuaji.
100% TRUE.

This Topic should be closed!
 
Kipindi cha nyuma humu nilishawahi kusema,haya mambo ya utekaji yanayofanywa na watu wa mfumo...kuna watu nao wataanza kupita na upepo wake
Nao watatumia njia hizo hizo kuteka

Ova
Watekaji wakiwa ni watu wa nje ya 'system' polisi watapiga kelele mpaka msemaji wa polisi ataitisha press conference possibly hata mkuu wa polisi wa kanda maalum ataongea na viongozi wa serikali wanaweza kupaza sauti pia, ila kama ni wao linapita kimyakimya.
 
Awamu ya Nne . Rejea kwa Ulimboka .
Ubinafsi ,uchu wa madaraka na kutafuta mali kupitia madaraka na teuzi ni kamba ya kunyongwa watu wema katika nchi hii.

JPM alikua Mzalendo wa kweli .Uadui dhidi yake ulikua ndani na nje ya nchi .
Kwa hiyo wakati mwingine alikua anapotoshwa kuwa fulani ni adui tuachie tumshughulikie . Kumbe WATU wanatafuta maslahi yao.

Yote kwa yote tunahitaji kiongozi atakayesimamia sheria zetu kwa haki.
Kama mtu ni mhalifu basi akamatwe kisheria na afikishwe mahakamani kama ni kunyongwa anyongwe lakini sio kutafutia WATU dhambi za kuua watu wasio na hatia . Magenge yote ya watekaji yanapaswa kuondolewa na kuchunguzwa hata mali wanazomiliki kwa sababu wakati mwingine ni maslahi binafsi ya kunyanganya WATU pesa zao kwa nguvu.

Ni wazi tunahitaji kiongozi anayeamini katika utawala wa Haki na kufuata sheria na atakayekemea wale wote wanaokiuka sheria iwe ni watawala au wananchi .
Huyu sio mwingine ni Tundu Antipas Lisu.

Lisu kamwe hawezi kukubaliana na watu kujichukulia sheria mikononi .
How do you know that au wewe ni 'mfalme njozi'?.
 
Tanzania hakuna utekaji wa kutaka ransom, ni watu wa TISS na kitengo maalum ndani ya polisi ndiyo huusika na utekaji. The 'protected' motherfvckers na ndiyo maana huwa wanateka openly kwa kujiamini sana, wangeshambuliwa na kuuawa ungesikia ni TRA or anything else similar to that kwamba waliowauwa wakamatwe(na wangekamatwa tu) na blah blah blah blahs kibao kuhalalisha utekaji na uuaji.
Unakumbuka alilekwa yule binti wa kiarabu msasani peninsula
Waliyomteka walitaka hela kutoka kwa mzee wake ,na ili9nesha kama mzee wa hyo binti alikuwa ana daiwa hela na mmoja wa watekaji,ila mwisho wa siku alipatikana na jamaa walidakwa

Utekaji ambao upo sahv ni wa watu kudhulumiana,hata watu wakijuwa una mpunga umepiga dili una hela watu wanakutimbia
Watu wanapita na upepo huo huo wa watu wa mfumo kuteka

Ova
 
Watekaji wakiwa ni watu wa nje ya 'system' polisi watapiga kelele mpaka msemaji wa polisi ataitisha press conference possibly hata mkuu wa polisi wa kanda maalum ataongea na viongozi wa serikali wanaweza kupaza sauti pia, ila kama ni wao linapita kimyakimya.
100% True.

Wewe jaribu kufikiria, ni kwa nini wale watekaji waliojaribu kumteka yule Mfanyabiashara kule Kiluvya hadi leo hawajakamatwa na Wala Majina yao wale wahalifu hayawahi kutajwa hadharani mpaka leo licha ya kwamba picha zao zipo wazi kabisa zinaonyesha sura zao? Mfano huyu hapa kwenye picha hapa chini, kwa nini Jeshi la Polisi halitaki kuweka wazi utambulisho wa huyu mhalifu anayeonekana kwenye picha hapa chini?
 
Attachments

  • Screenshot_20241122-141705.png
    Screenshot_20241122-141705.png
    727.4 KB · Views: 4
100% True.

Wewe jaribu kufikiria, ni kwa nini wale watekaji waliojaribu kumteka yule Mfanyabiashara kule Kiluvya hadi leo hawajakamatwa na Wala Majina yao wale wahalifu hayawahi kutajwa hadharani mpaka leo licha ya kwamba picha zao zipo wazi kabisa zinaonyesha sura zao? Mfano huyu hapa kwenye picha hapa chini, kwa nini Jeshi la Polisi halitaki kuweka wazi utambulisho wa huyu mhalifu anayeonekana kwenye picha hapa chini?
Sasa yule jamaa wa kilivya syo mwanaharakati wala hajihusishi na siasa,lakini watu walitaka kumteka!ukweli anaujuwa yeye
Hata kesi yenyewe ukifatilia haielezi motive ya watekaji ni nini!
Ila kwa wenye jicho la tatu washajua kuwa ni masuala ya pesa tu

Yule jamaa Anaweza asiwe Mwanasiasa Active huko kwenye majukwaa ya kisiasa ya mihadhara ya watu, lakini Anaweza kuwa Mwanasiasa Machachari Sana kwenye ulingo wa siasa za ndani za chama au hata humu mtandaoni.

Kumbuka, humu mtandaoni wameweka mamluki wao wengi Sana ambao wanafuatilia mijadala ya kisiasa iliyopo humu. Watu wanaotakiwa kutekwa (Mateka Tarajali) wamekuwa recruited humu mitandaoni kila siku.

Aidha, Utawala wowote ule ambao upo mwishoni, utawala wowote ule ambao unakaribia kuanguka au utawala wowote ule ambao unakaribia kukata roho, mambo kama haya ya kuteka watu ni kawaida kabisa kufanyika kwenye nchi yenye utawala wa aina hiyo. Hii ni kutokana na sababu za Watawala kuchanganyikiwa, kushikwa na hofu au kupata kiwewe.
 
Tanzania hakuna utekaji wa kutaka ransom, ni watu wa TISS na kitengo maalum ndani ya polisi ndiyo huusika na utekaji. The 'protected' motherfvckers na ndiyo maana huwa wanateka openly kwa kujiamini sana, wangeshambuliwa na kuuawa ungesikia ni TRA or anything else similar to that kwamba waliowauwa wakamatwe(na wangekamatwa tu) na blah blah blah blahs kibao kuhalalisha utekaji na uuaji.
 
Nimepokea taarifa usiku huu kutoka kijijini Kishanje, Bugabo Bukoba, akitaarifu kutekwa kwa kijana Danstan Daudi Mutajura (pichani juu) anayefanya kazi Jijini Dar es Salaam.

Dastan ametekwa jana majira ya saa 4 asubuhi maeneo ya Sigara, TANESCO, Buza Jijini Dar es Salaam wakati akienda kazini kwake akitokea nyumbani kwake eneo la Kitunda, Jijini Dar es Salaam.

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Dastan ametekwa na WATU WASIOJUKIKANA baada ya gari alilokuwa akiendesha (T.109 DYV) aina ya Mercedes Benz C300 kuzuiwa kwa mbele na gari la watekaji.

Baadaye gari la Danstan liliokotwa na kupelekwa Kituo cha Kidogo cha Polisi cha Buza na kuandikishwa kama MALI YA KUOKOTWA RB NO. BZA/RB/53/2025

Madereva wa bodaboda walioshugudia tukio hilo wamesema Danstan alinyofolewa kutoka kwenye gari lake na kufungwa Kitambaa usoni akilalamika kuwa alikuwa akitekwa.

View attachment 3192960
Na unaamini Samia hawezi kumaliza utekaji?
Haya mambo yameanza tena?
Utawala wowote ule ambao upo mwishoni, utawala wowote ule ambao unakaribia kuanguka au utawala wowote ule ambao unakaribia kukata roho, mambo kama haya ya kuteka watu ni kawaida kabisa kufanyika kwenye nchi yenye utawala wa aina hiyo. Hii ni kutokana na sababu za Watawala kuchanganyikiwa, kushikwa na hofu au kupata kiwewe.
 
Yule jamaa Anaweza asiwe Mwanasiasa Active huko kwenye majukwaa ya kisiasa ya mihadhara ya watu, lakini Anaweza kuwa Mwanasiasa Machachari Sana kwenye ulingo wa siasa za ndani za chama au hata humu mtandaoni.

Kumbuka, humu mtandaoni wameweka mamluki wao wengi Sana ambao wanafuatilia mijadala ya kisiasa iliyopo humu. Watu wanaotakiwa kutekwa (Mateka Tarajali) wamekuwa recruited humu mitandaoni kila siku.

Aidha, Utawala wowote ule ambao upo mwishoni, utawala wowote ule ambao unakaribia kuanguka au utawala wowote ule ambao unakaribia kukata roho, mambo kama haya ya kuteka watu ni kawaida kabisa kufanyika kwenye nchi yenye utawala wa aina hiyo. Hii ni kutokana na sababu za Watawala kuchanganyikiwa, kushikwa na hofu au kupata kiwewe.
Point yangu ni syo anayetekwa basi ni mambo ya sisasa,
Kuna watekaji wanawateka watu kwa kutumwa kuwa teka watu
Kutokana na mambo ya kibiashara,kudhulumiana nk
Juna watu sahv wanapita na upepo huu wa kutekana tekana wanaoutumia watu wa mfumo na wao wanapita mule mule !

Ova
 
Yule jamaa Anaweza asiwe Mwanasiasa Active huko kwenye majukwaa ya kisiasa ya mihadhara ya watu, lakini Anaweza kuwa Mwanasiasa Machachari Sana kwenye ulingo wa siasa za ndani za chama au hata humu mtandaoni.

Kumbuka, humu mtandaoni wameweka mamluki wao wengi Sana ambao wanafuatilia mijadala ya kisiasa iliyopo humu. Watu wanaotakiwa kutekwa (Mateka Tarajali) wamekuwa recruited humu mitandaoni kila siku.

Aidha, Utawala wowote ule ambao upo mwishoni, utawala wowote ule ambao unakaribia kuanguka au utawala wowote ule ambao unakaribia kukata roho, mambo kama haya ya kuteka watu ni kawaida kabisa kufanyika kwenye nchi yenye utawala wa aina hiyo. Hii ni kutokana na sababu za Watawala kuchanganyikiwa, kushikwa na hofu au kupata kiwewe.
Na Ukishaona watu wanafikia kutekana basi hawaziamini tena vyombo vya sheria kama polisi,mahakama nk

Ova
 
Hii nchi ina mambo ya kijinga sana. Huu upumbavu wa kutekana na kuuana ulianzishwa na Magufuli.
Huu upunguani ndio unasababisha hilotatizo lisiishe.

Watu wamekua kama majuha, mtuanatekwa badala ya kupambana na current situation mnahangaika na mtualiekufa, pumbavu sana.

Hata hayo matekaji yanajua yakifanya huo ushetaniwao wanajua lawama mtampa marehemu.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Kwaiyo bado anaendeleza akiwa kaburini? Au bado Rais wa nchi ni yeye?
Au unataka kusema nchi haina Rais?

Swali zuri sana. Kwahiyo hawa waliopotea 2024 au waliouwawa nao alisababisha JPM? Kuna wakati nashindwa kuelewa huwa tunafikiri nini.
Tunaambiwa na baadhi ya watu alikuwa mtu muovu. Nilifikiri tungekuwa tumefanya tofauti, tungekuwa na haki ya kunyoosheana vidole.
Mbona kama vile......

Naangalia haya maandishi ya Biblia na kuyaamini ukweli wake, kutoka
Luka 6-41-45
Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako. Kwa maana hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
 
Back
Top Bottom