Dar: Dunstan Daudi Mutajura adaiwa kutekwa eneo la Buza

Dar: Dunstan Daudi Mutajura adaiwa kutekwa eneo la Buza

Jana niliona hizi taarifa nikasema nianze kuchimba kumtafuta huyu bwana…Kwanza Hakuna alot of information kumuhusu ila nikaenda sehemu ingine nikapata kuwa aliwahi kuteuliwa mwaka 2022 kama Non executive director kuiwakilisha GOT kwenye mradi wa uchumbaji madini Mahenge. CV yake wakati anateuliwa ni kama ufuatavyo.

Danstan Mtajura Daud - Government Appointed Director Link : Black Rock Mining Limited – An emerging Tanzanian/Australian graphite miner

——————
Eng. Danstan Mtajura Daud holds a in Mineral Processing Engineering (Metallurgist) from MRI and Diplomatic in Protocol and Public Relations from Mozambique/Tanzania Centre for Foreign Relation (CRF). He is Currently Serving as a Mining Analyst and Advisor in President's Office and Monitoring and Coordinator of All Strategic Government Negotiations Team including Special Presidential Government Negotiations Team (SPGNT).
 
Attachments

  • IMG_2480.PNG
    IMG_2480.PNG
    872.3 KB · Views: 7

Asante sana mwnyewe jana kwenye search results zilikuwa zinatokea taarifa zake tu za kupotea.
 
Jana niliona hizi taarifa nikasema nianze kuchimba kumtafuta huyu bwana…Kwanza Hakuna alot of information kumuhusu ila nikaenda sehemu ingine nikapata kuwa aliwahi kuteuliwa mwaka kama Non executive director kuiwakilisha GOT kwenye mradi wa uchumbaji madini Mahenge. CV yake wakati anateuliwa ni kama ufuatavyo.

Danstan Mtajura Daud - Government Appointed Director Link : Black Rock Mining Limited – An emerging Tanzanian/Australian graphite miner

——————
Eng. Danstan Mtajura Daud holds a in Mineral Processing Engineering (Metallurgist) from MRI and Diplomatic in Protocol and Public Relations from Mozambique/Tanzania Centre for Foreign Relation (CRF). He is Currently Serving as a Mining Analyst and Advisor in President's Office and Monitoring and Coordinator of All Strategic Government Negotiations Team including Special Presidential Government Negotiations Team (SPGNT).
 
Huko mbeleni mtu akija na kitabu cha kuhusu samia na mambo yanayoendelea watu wasishangae, Rais kashindwa kabisa kukemea maswala ya utekaji
Kuanzia mwezi wa 6 ataanza kukemea na kujiweka mbali, watu waseme " Jamani raisi naye hapendi haya mambo";"Kuna watu wanamuangusha"; "anahujumiwa".

Mimi kwangu ni muhuni tu kama waliopita kabla yake.
 
Jiji la das-es laam ni la ajabu sana.. Mtu anatekwa mchana kweupe wanamuangalia tu., 🤒🤒🤒
Mara nyingi Kama sio zoteee ""MTOA. MSAADA NDIE HUWAGA ANAUMIA""

Utapigwa risasi au kujumuishwa kwenye mbanga ZAO.

Ningekua Mimi ningefanya Kama MDUDE CHADEMA

Au yule bonge wa kiluvyaa ninge dinda na huu MWILI wangu bonge labda ninge pigwa na kupoteza fahamu na nisinge kubali ningejaza watu.
 
Tanzania hakuna utekaji wa kutaka ransom, ni watu wa TISS na kitengo maalum ndani ya polisi ndiyo huusika na utekaji. The 'protected' motherfvckers na ndiyo maana huwa wanateka openly kwa kujiamini sana, wangeshambuliwa na kuuawa ungesikia ni TRA or anything else similar to that kwamba waliowauwa wakamatwe(na wangekamatwa tu) na blah blah blah blahs kibao kuhalalisha utekaji na uuaji.
Exactly!
 
1736181842023.jpeg

Kwa mujibu wa Taarifa ya kamanda wa Polisi kanda hiyo, SACP, Jumanne Muliro imesema "Januari 04,2025 majira ya saa 8 :00 mchana lilipokea taarifa toka kwa wananchi ya kuonekana kwa gari aina ya Mercedes Benz lenye namba za usajili T 109DVY likiwa limetelekezwa eneo la BUZA SIGARA".
 
MASHUHUDA WASIMULIA TUKIO LA UTEKAJI MUTAJURA' GARI NYEUSI ILIKUJA KELELE ZILIPIGWA WATU WALI...'

6 January 2025
Matukio ya watu kudaiwa kutekwa yameendelea kuripotiwa nchini, baada ya jana kudaiwa kutekwa kwa mkazi wa Dar es Salaam, Dastan Mutajura eneo la Buza -Sigara.

Taarifa za kutekwa kwa Mutajura zilisambaa mtandaoni, zilidai lilitokea wakati akienda kazini akitokea nyumbani kwake eneo la Kitunda. Kutokana na taarifa hiyo, asubuhi ya leo Jumapili, Januari 5, 2025 taarifa ya kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ilieleza kuwa wanafuatilia kupotea kwa mtu huyo.

Mwananchi limefika eneo lilipotokea tukio hilo na kuzungumza na mashuhuda walioeleza watu wasiojulikana wakiwa na bunduki walitekeleza utekaji uliowaacha wananchi na hofu, saa nne asubuhi ya Januari 4, 2025.

Mjumbe wa eneo hilo la Kwa Mchina, Selina Geay amesema tukio la kutekwa Mutajura halikuchukua dakika tano hadi kuondoka naye, kwani lilikuwa la haraka. "Nilikuwa nafanya usafi katika eneo langu hapa, tukaona gari nyeusi ilikuwa na mwendo wa kasi, lakini ilisimama ghafla baada ya kuvuka dimbwi la maji.

Tukamuona mwanaume anashuka kwenye hiyo gari, huku nyuma yake kukiwa na gari nyingine," amesema mjumbe wa mtaa Selina.

Amesema baada ya mwanaume huyo kushuka "Mutajura" alianza kupiga kelele akihitaji msaada na kudai anatekwa na watu asiowajua, jambo lililowashangaza watu waliokuwepo eneo hilo.

"Wakati anapiga kelele hizo tukaona watu wengine wameshuka na bunduki na kumfuata yule baba na kumpiga mdomoni na hakuendelea kupiga kelele.

Watu waliokuwa jirani na tukio katika kijiwe cha bodaboda walitaka kukimbia, lakini walitishiwa na kubaki eneo hilo," amesema.

Mjumbe Bi. Selina amesema bila kuchelewa walimkamata Mutajura na kumuweka kwenye gari walilokuja nalo, kisha kuondoka kwa mwendo wa haraka, huku gari nyeusi ikiwa limebaki eneo lilipotokea tukio hilo.

Amesema baada ya watu hao kuondoka, alipiga simu kituo cha polisi Buza kwa ajili ya kuwapa taarifa kwa tukio hilo na kuachwa kwa gari ambayo imepelekwa polisi na kutolewa taarifa.

Wakiwa katika maulizo na Jeshi la Polisi, amesema alijitokeza mwanamke akitokea njia ya Kitunda yalipokuwa yametokea magari hayo na kujitambulisha kuwa ni mke wa aliyetekwa (Matujura).

"Yule mwanamke alipofika alijitambulisha kwa polisi kuwa gari lililopo katika tukio ni la mumewe, hivyo alihitaji kujua yuko wapi lakini walimwambia waende kituoni kwa ajili ya maelezo zaidi," amesema.

Baada ya kuvutwa kwa gari hilo kupelekwa katika kituo cha polisi Buza, mkewe naye alifuata nyuma akiwa kwenye bodaboda ambayo alikwenda nayo eneo la tukio.

Amesema leo mkewe amefika tena eneo la tukio kuuliza mashuhuda namna mumewe alivyotekwa na walichokishuhudia hadi walivyoondoka naye.

"Leo mkewe amekuja tena maana jana hakutaka kuongea na mtu zaidi ya polisi, naona ili kupata usahihi wa taarifa amerudi ili kujua ilikuaje na kama walimdhuru wakati wanamchukua na sisi tumemueleza kile tulichokiona," amesema shuhuda mwingine ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

Amesema kilichotokea jana madereva wa bodaboda katika kijiwe lilipotoea tukio wameingiwa na uoga, baada ya kuona bunduki na kupewa amri za kutokwenda sehemu yoyote na kutofanya kitu chochote kwenye simu zao.

Source : Mwananchi digital
 
Back
Top Bottom