Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Dar es salaam limegeuka jiji la makelele, Serikali imelala?

Sasa kama hizo kelele zitakuwa hivyo hivyo kama ilivyo mchana hao wanaoishi K.koo wataweza kulala na kupata usingizi ??!
Hatari sana !
Zile nyumba ni zina sound proof ukiingia ndani husikii makelele ya nje kumbe hujawahi kuingia kwenye baadhi ya zile nyumba za kariakoo ndio wanaoishi zile nyumba kelele za nje hawazisikii kabisa ila ukitoka nje ndio unasikia
 
Jukumu la kuhakikisha jamii inaishi katika makazi bora ikiwemo udhibiti wa uzalishaji kelele mjini hasa Dar es salaam, lingeweza kufanywa na Serikali za mitaa ndani ya Halmashauri zetu kwa ufanisi mkubwa!

Badala yake Halmashauri hasa ya Ilala nao wanashiriki kikamilifu kuzalisha kelele kwa matangazo yao ya kukumbushia leseni za biashara na Service levy.... Kelele za kutangaza kuvuna mahali ambapo hawajapanda !!.
 
Mkuu hujakaa karibu na ile misikiti ya "swalaa, swalaa, kitanda chako ndiyo kaburi, shuka ndiyo sanda yako, swalaa swalaaa" wanakupigia makelele saa nzima sala ya alfajiri, bila kujali una imani gani?

Maombi hayatambuliki kwa wote katika secular state. Maombi yenu ombeni kanisani kwenu msiwapigie kelele wengine wasioamini kama nyie.
Kuna mmoja mtaani kwetu kazi yale kupiga swalaa lakini chuma ulete hatari sana.
 
Ameomba lakini hajapata.
Basi awe mvumilivu huku akiendelea kupambana na uhamisho.
Uhamisho Ni haki ya Mtumishi kwa sababu mbalimbali:
  1. Kafanya kazi ktk eneo moja kwa muda mrefu.
  2. Ugonjwa WA Mfanyakazi. Hivyo, unaomba uhamisho kuwa Karibu na sehemu yenye uhakika na matibabu.
  3. Mazingira magumu ya unapofanyia kazi. Hivyo, inapelekea kushusha morali ya ufanyaji kazi Wako. Dawa Ni kuhama.
  4. Kuhama ili kuwa Karibu na wategemezi wanaokutegemea kwa kila Kitu. Mfano wazazi, n.k
  5. Kuwa Karibu na familia yako. Make/mme na watoto zako
 
3. Serikali ithibiti haya matangazo ya magari ambayo huzunguuka mitaani huku wamefungulia muzik kwa staili ya Disco.
Yale ma canter na wakata viuno ni hatari, wakipita mahali kama unaongea na simu au watu lazima kusitisha kwanza, maana ni makelele ya kuumiza masikio. Wakipiga kambi mahali hapakaliki
2. Serikali ipige marufuku kwa bodaboda kufunga speaker kwenye mabodaboda yao, kwanza haya mamiziki wanayofungulia ni hatari kwa usalama barabarani.
Hao bodaboda hata wakipigiwa honi hawasikii kwa ule ulimbukeni wa kelele za singeli
 
Yale ma canter na wakata viuno ni hatari, wakipita mahali kama unaongea na simu au watu lazima kusitisha kwanza, maana ni makelele ya kuumiza masikio. Wakipiga kambi mahali hapakaliki

Hao bodaboda hata wakipigiwa honi hawasikii kwa ule ulimbukeni wa kelele za singeli
Ni kweli na uzi ni kusaidia usalama wa bodaboda pia.
 
Ushaambiwa jiji la biashara then unalalamika kelele.
Hamia Mtwara/Lindi ambako kumetulia.
Dar ina wakazi 6M, wewe lonely ndo hupendi kelele.
Mkuu London ni Jiji la biashara pia lakini halizalishi kelele kama Dar !!.
Sema Dar hakuna mamlaka zinazojielewa na kusimamia sheria za miji na majiji kikamilifu. Uzalishaji kelele Dar hautofautiani na kiwango cha uzalishaji taka na vyote vinadhibitiwa na sheria.
 
Hahaaa. Ndiyo ubaya wa demokrasia huo mkuu. Ukitaka kuwagusa machinga unaogopa sababu watakunyima kura. Ukitaka kusema msijenge hapa, bodaboda ziwe na utaratibu huu, bajaji ziwe hivi nk nk huwezi sababu ya kuogopa kunyimwa kura. Ndiyo maana miji ya India haieleweki hata kidogo. Miji yetu nayo inafuata huko.
Kwakweli ndio maana wengine tunaona hii Demokrasia ni majanga tu !
 
Zile nyumba ni zina sound proof ukiingia ndani husikii makelele ya nje kumbe hujawahi kuingia kwenye baadhi ya zile nyumba za kariakoo ndio wanaoishi zile nyumba kelele za nje hawazisikii kabisa ila ukitoka nje ndio unasikia
Lakini bado zipo nyumba nyingi sana za kizamani ambazo hazina na hakuna namna yeyote ya kutengeneza hiyo sound proof !
 
Dar ni Jiji la biashara kuliko majiji kama Dubai na Tokyo?
Mbona huko hakuna hivyo vispika na makelele?

Kuna mdau huko juu amesema hali hiyo ya makelele na kupenda makelele ni dalili ya ujima na umasikini,nakubaliana nae kwa asilimia mia moja.
Bro wanaovitumia hawanazo wala wa mamlaka za local authority. kaka ukisogea kwenye vikelele huwezi kujua wanasema nini yaani ni kama mkusanyiko wa wadudu.
 
Back
Top Bottom