Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Hawana imani na kiongozi gani sasa?? Viongozi wao wamachinga au mkuu wa mkoa??

Labda awe kiongozi wao ila kama ni RC hawawez kumfanya chochote kwa utawala huu wa kulindana. Labda mwendazake angewasikiliza ila pia sio kwa bashite hapo angewatoa baru.

Kwa bahati mbaya hawa wamachinga wanateseka na nahisi wataendelea kuteseka bila ya kua na mtetezi si upinzani wala serikali. Wamebaki wao kama wao, waliemtegemea hayupo tena ni HUZUNI.
 
Hii ngoma kila mtu ataisoma kwa wakati wake. Hata Ndugai hakuwa hujua ipo siku atalala na viatu.

Katiba Mpya Katiba Mpya
 
Ni kweli wote walikenua meno? Nadhani tunasema uongo hapa, yani wafanyabiashara wote wa karume wawe ccm?
 
Kwahiyo unataka kusema
Anayebomoana Aliyechoma ni mtu mmoja?

Nchi ngumu hii
 
Kucheka na kulia huwa ni Kwa zamu kwenye haya maisha
 
Wana wazalendo wao huko ccm watawatetea.
 
Tatizo watz hatupendi mabadiliko, hapo hiyo ni nafasi ya Serikali kupajenga ni eneo zuri sana wamachinga walishajengewa ile machinga complex
 
kabisa yani, hapo utakuta wote ni ccm na hata wanaoonekana kulaumu wanatupia lawama kwa awamu hii na kusema ingeluwa awamu iliyopita haya yasingetokea

Yani kiufupi hawajaona tatizo la kuongozwa na ccm
Tatizo sio ccm weka chuki na siasa zako Pemben kwani JPM alikuwa ukawa? Yaani nyie wafia vyama ndio mnachelewesha maendeleo ya nchi hii mnaonekana kujali vyama kuliko nchi.
 
Uchunguzi ufanyike kwa Sikh Saba ama kumi na NNE watakuwa awakila wapi? Mtawapa hela? Uchunguzi hauwezi kufanyika huku machinga wakiendelea na biashara zao? Nina maswali kibao hapo....
 
Mwenyekiti wa machinga alikuwa anaambatana na mgombea wa CCM kila anapoenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…