Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Safi kabisa haki hudaiwa kwa haki. Hata hivyo hilo soko ni la manispaa sio lap hata hiyo haki hawana.

Hii nchi Kuna group la watu wanahisi wao ndio was maana sana. Machinga wanajiona wao ni special group wasikilizwe kila matakwa yao.

Sijui wenye viwanda nao wagome halafu uone nani anasikilizwa?
Sasa Jana waziri alikuwepo walikuwa kila wanachoambiwa wanapiga makofi,na akatoa siku 7 za uchunguzi,leo wanaandamana nn sasa
 
CCM mbele kwa mbele,,,mpaka kufika 2025 medula zitakuwa zimetusogea..
 
Swali fikirishi Sana.
Eneo la breweries lile

Enzi za makamba,walipokuwa wanawatoa wamachinga kko,wakapepelekwa pale

Zamani breweries walikuwa wanapatumiaaaa
Wanapaki magari yao,wanafanya shuguli zao
Biashara zilikuwepo sema za kiuzushi syo za kudumu

Ova
 
Sasa Jana waziri alikuwepo walikuwa kila wanachoambiwa wanapiga makofi,na akatoa siku 7 za uchunguzi,leo wanaandamana nn sasa
Hapo ndio utashangaa, na ndio maana nimesema hao walioandamana leo unaweza kukuta ni wahuni tu hawana hata kibanda pale Ila wanataka wafunguliwe ili wajigawie mapema maeneo ya kuwapangisha wengine.

Hapo Kuna Vita ya waliokuwepo versus wanaotaka kuingia kwa upenyo huo. Wanalaumu serikali lakini aliyechoma Moto ni wao kwa wao wanaondoana wanajua wakiruhusiwa kujenga na ndio wanataka eti wajijengee wenyewe hii ni kutaka maeneo .

Mtu anakamata eneo anapangisha hata meza tano halafu yeye hauzi hata mitumba anakula hela ya pango na ndio wanajifanya wapewe eneo lao, nani amesema kuna aneo la mwananchi??? Maeneo yote yapo chini ya Rais.
 
Ukisikia GSM kakabidhiwa hapo wala usishangae. Soko dogo la Kariakooza chini chini zinadai tayari kashakabidhiwa. Yale madai ya kuwa rimoti ameshikilia msoga naanza kuyaamini.
 
Ukisikia GSM kakabidhiwa hapo wala usishangae. Soko dogo la Kariakooza chini chini zinadai tayari kashakabidhiwa. Yale madai ya kuwa rimoti ameshikilia msoga naanza kuyaamini.
Gsm wapi eneo hilo ni la breweries
Fatilieni historia la eneo hilo

Ova
 
Mbona bado mapema sana kwa mama yetu au wenye stress ya 2025 bado wapo au wamachinga wenyewe baadhi yao wanawahujumu we zao ili wawatoe wale wazawa wa karume wakae wakuja kutoka kariakoo shimoni .😦

Kuna nini nyuma ya panzia ni bora nami niweke maneno ya akiba niasome maoni ya we zangu naweza nikapata jibu nachokifikiria
 
Kiukweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.

Wanasiasa hebu wasaidieni hawa wamachinga wanapita katika kipindi kigumu sana.

Hali niliyoishuhudia leo pale Karume ilinikumbusha zile vurugu za wale Imani kali pale Mwembechai enzi za Augustino Lyatonga Mrema

Mungu wa mbinguni wape busara viongozi wetu.
 
kabisa yani, hapo utakuta wote ni ccm na hata wanaoonekana kulaumu wanatupia lawama kwa awamu hii na kusema ingeluwa awamu iliyopita haya yasingetokea

Yani kiufupi hawajaona tatizo la kuongozwa na ccm
Kumbe ccm ni wengi kiasi hicho?

Sasa mbona mkipigwa kwenye uchaguzi huwa mnalalamika?
 
Kiukweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.

Wanasiasa hebu wasaidieni hawa wamachinga wanapita katika kipindi kigumu sana.

Hali niliyoishuhudia leo pale Karume ilinikumbusha zile vurugu za wale Imani kali pale Mwembechai enzi za Augustino Lyatonga Mrema

Mungu wa mbinguni wape busara viongozi wetu.

John alikuaga mjanja sana alijua akicheza vizuri na hilo kundi atatawala vizuri ndicho alichofanya ili msala abaki nao ataemfuata na ndio hivo, kwa sababu nchi ya watu milioni karibu 60 ajira rasmi hazizidi milioni 2 ina maana kuna watu lazima wawe wachuuzi, machinga na kadhalika na idadi yao ni kubwa sababu hata wasio na ajira kwa nchi kama yetu hawana security yoyote hata ya chakula au mlo mmoja kwa siku tofauti na nchi kama south ambapo jobless japo serikali inawapa chochote kitu mwisho wa mwezi, sasa kuhandle issue ya machinga inataka kutumia busara ya hali ya juu sana
 
Mama anajitoa ufahamu
Katoka kwao visiwani kaja kuwa rais
 
Back
Top Bottom