John alikuaga mjanja sana alijua akicheza vizuri na hilo kundi atatawala vizuri ndicho alichofanya ili msala abaki nao ataemfuata na ndio hivo, kwa sababu nchi ya watu milioni karibu 60 ajira rasmi hazizidi milioni 2 ina maana kuna watu lazima wawe wachuuzi, machinga na kadhalika na idadi yao ni kubwa sababu hata wasio na ajira kwa nchi kama yetu hawana security yoyote hata ya chakula au mlo mmoja kwa siku tofauti na nchi kama south ambapo jobless japo serikali inawapa chochote kitu mwisho wa mwezi, sasa kuhandle issue ya machinga inataka kutumia busara ya hali ya juu sana