Dar es Salaam ni mkoa uliojaa masikini wengi wanaojificha kwenye kivuli cha miundombinu tu

Dar es Salaam ni mkoa uliojaa masikini wengi wanaojificha kwenye kivuli cha miundombinu tu

Mkuu 😊🤓

Unaita binadamu watoto wa MUNGU mafukara..

Maisha ni gwaride Kuna wa mwisho na wa kwanza ikisikika nyuma geuka wa mwisho anakuwa wa kwanza..
Haiondoi ukweli kwamba Kuna mafukara ,ndio maisha yenyewe hayo.

By the way wengi wa mafukara wa Dar wamejitakia watoke huko waje kupambana Mkoani.
 
Dsm cha bure ni salamu tuu , hadi k u ,uma inauzwa tena unaikuta safi kabisa , wee kazi kubwa nikuuilipia tuuu 3k , 4k , 5k 10k plus then unakisisimua kichwa cha chini
 
ukipita kwenye vituo vya mwendokasi, watu wamenyong'onyeaaa wameshika tama, wamevunjika moyo unaona kabisa huyu anahitaji msaada hana furaha. ndio maana mnajazana kwenye makanisa ya kina mwamposa kuomba miujiza everyday,na hamnawahi kuipata. hivi tangu mwamposa aanze kuwauzia mafuta hawa watu, umasikini si ungekuwa umeisha Dar es salaam kama sio nabii wa uongo yule? angalia tu, wameona makanisa ya uongo ndio kimbilio kwenda kupunguza stress. fanyeni kazi au njooni mikoani mtafute mtaji mkirudi huko na mitaji mizuri mtafanya biashara kubwa na mtatoka haraka.
Hahaaa eti anahitaji msaada
 
Dar ndio sehemu pekee mtu anakuja kwa nauli ya kupewa na anaishi. Uko Dodoma kwenu nani aje vijijini Godegode, Kibakwe au Chololo bila connection na atoboe?

Dar mtu anakuja analala kwenye maboksi anaweka juhudi anapiga hatua kidogo kidogo. Mtu anaamka asubuhi hajui kazi ataipata wapi na atafanya nini ila ana uhakika wa kazi. Dar kila siku ni msimu, hakuna bidhaa utakosa hata iwe bei ghali. Nachingwea unapata maembe mwaka mzima? Sasa mtengeneza juisi Nachingwea kama hakuna msimu huwa anafanya nini vibarua au.

Labda kwa wafanyakazi wa serikali. Mwalimu wa Dar anaweza zidiwa na mwalimu wa Morogoro kama wote wana akili sawa za kujiongeza. Ila fundi ujenzi au mshona viatu sahau
You nailed it broo.

Binafsi sipapendi DSM kwa sababu ya kazia ya Hari ya hewa na Usafiri. Ila nje ya hayo mambo dar ni jiji la opportunity kila unachotaka kufanya DSM ni biashara tofauti ni mkoani Value chain ni ndogo sana.

Imagine mtu anauza miguu tu ya kuku na anauhakika wa kula kulipa kodi na mambo mengine madogo madogo.

Sijui vizuri kuhusu Mwanza ila nalipenda hili jiji.
 
Yaan takriban nusu muongo Sasa sijasafir kwenda mkoa nilienda mkoa sio Siri naona pa kishamba sanaaaa pamekaa kishamba hakuna mzunguko wa pesa kabisa ukiwa police au mwalimu wa primary Au secondary unajiona umetusua maisha...

Dar ndio DUBAI ya Tanzania NDIO Washington DC ama New York City ndio Johannesburg ndio Amsterdam ya Tanzania dar es salaam [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]TANZANIA [emoji1241][emoji1241][emoji1241] [emoji1241] maisha ni rahisi MNO kutoboa kuliko sehemu yeyote TANZANIA

1. POPULATION ina fevor kutokana na population kua Caucasoid in nature.......

2. Government makao makuu haina ubishi dar ndio Tanzania na Dar es salaam TANZANIA [emoji1241][emoji1241][emoji1241]

3. Financially [emoji383][emoji857] haina ubishi kua Tanzania dar es salaam TANZANIA NDIO mkoa pekee unao changia Kwa kiwango kikubwa Pato la taifa Kwa kukusanya mapato....

4. Fursa nyingi sana sema tu watu wengi hawajui ndio maana Kuna mapolice , ma doctor na WALIMU wengi WALIO acha ajira na wapo hapa mjini dar es salaam

5. Ni ndoto za watu wengi wa mikoani kuishi Dar es salaam TANZANIA [emoji1241][emoji1241] na mtu akifa bila kufika dar es salaam lazima ajilaumu [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23]

Mkuu yapo mengi mkuu [emoji4][emoji851][emoji851][emoji851]
Mkoa gani huo ulio ona pakishamba? Inakufaa nn ww kuishi mkoa wenye maghorofa mengi barabar nzuri na mahotel ya kila aina wakati ww umepanga chumba kimoja, unapanda daladala na unakula wali wa 2000 kwa mama ntilie.

Hapa hatuangaliaa sehemu ya kishamba au ya kishua tunaangalia sehemu ambayo vijana wanaweza kuventure na kutengeneza pesa.

Kwangu mm inategemea na ntu na ntu, na biashara unayo taka kufanya. Mfano kmaa weww ni mtu wa kilimo/ufugaji njoo mikoa kama Morogoro utaona fursa zaidi kuliko ukiwa huko Dar
 
Dar utapata Hela za kula tu na kupanga chumba,ila kutoboa ni msala,

Kunamwanangu alienda dar tangu mwaka 98 ,alikua akilud mkoa ni mtu wa pamba sana ila maokoto Hana ,ana nauli tu ya kuludi

Mungu mkubwa akastuka akaludi bush,saivi anamisauzi mitatu,aisi Moja ,ng'ombe 20,shamba la urith kama heka 70,watoto kwa mwaka wanasoma private ada jumla Yao kama milioni 4.5

Watu wa dar(mjini) hua wanaona aibu kulud bush maana hua wanawaona waliowaacha wamewazid mbali akilud mtupu atawaambia Nini

Ndio mana hua wanaludi kusalimia tu na kuludi mjini
 
Oya weeeee oyaaa tuache na Dar yetu sisi tunajua tunaishije huku hatuna hela ila hatulali njaa wala hatushindi njaa, hatuna pakulala ila tuna lala na kuamka vyema kabisa hatuna kazi ila uhakika wavibarua tunao, hatuna uhakika wa chakula cha buku mbili lakini ukakika wa miguu ya kuku na mihogo ya kwa mama Mwajuma haitushindi
 
nimenunua ardhi Dsm, nimenunua ardhi mikoa kama mitatu pia. usijifariji. popote ulipo inategemeana na ardhi unanunua wapi, ila kwenye ordinary people hapo dsm ardhi ni bei ndogo kuliko mikoa kama mwanza, arusha, mbeya, dodoma na kwengine.
Mkuu kwanini unafananisha Dar nje ya mji na Mikoani mijini kwanini usifananishe Dar mjini na Mikoani mjini kwa Dar nje ya mji na Mikoani vijijini, kama hiyo Mikoa uliyotaja unaongelea maeneo ya mjini basi na Dar ongelea maeneo ya mjini kati siyo nje ya mji, mfano kwa Mbeya ukitaja maeneo kama Isyesye au Forest Mpya basi na Dar utaje maeneo kama Mikocheni au Kawe
 
nimenunua ardhi Dsm, nimenunua ardhi mikoa kama mitatu pia. usijifariji. popote ulipo inategemeana na ardhi unanunua wapi, ila kwenye ordinary people hapo dsm ardhi ni bei ndogo kuliko mikoa kama mwanza, arusha, mbeya, dodoma na kwengine.

Ukapimwe mkojo aisee!! Unaongelea Dar ya wapi? Aisee amka usingizini usije ukakojoa kitandani.
 
Back
Top Bottom