Dar es Salaam nzima haijawahi kutokea Baa yenye sifa na mvuto kama Kwa Macheni

Dar es Salaam nzima haijawahi kutokea Baa yenye sifa na mvuto kama Kwa Macheni

Ukiwa mjanja hadi buku unakula mzigo fresh na sometimes unaulizwa vipi na uwani utaingia? Ukisema ndio unageuziwa vipara viwili umalizane navyo [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaaah
 
Nyapu za kumwaga, huduma za chap chap, mambo ya bolingo kina papaa buengee enzi hizo unawakuta hapo.

Wale wazee wa kuhemewa na kuhemea wenzao mgongoni nao hawakuwa nyuma. Nyama choma mpaka mishkaki ya bata mzinga unapata.
I mean ile sehemu ilikuwa ni ya aina yake nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaaah
 
Hahaha 🤣🤣🤣 Kweli mkuu, macheni imeondoka na watu wengi sana. Tulionusurika wengi wetu tulichinja mbuzi na kufanya sherehe.

Maana mshikemshike wa miaka ile ulikuwa sio wa kitoto.
Usinilize Mkuu nimezika Rafiki zangu wa Kiume 11 waliokuwa Wakilewa hapo na Rafiki zangu wa Kike 5 na Wote ni kwa Dally Kimoko Gitaa / UKIMWI Kipindi hicho hiyo Baa ikiwa ndiyo Talk of the Town hasa.
 
Ya mishoga iliuwa stem za watu sana enzi zile. Mtu umetulia mezani huku ukimsubiri mchumba kaenda msalani mara moja. Ghafla linakuja dume lenye midevu na kuomba likupe kampani ukija kulicheki miguuni limevaa vikuku na jina la dhahabu linakuchekea tu kama chizi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kumbe ushoga uko tangu zaman, sasa hizi kelele za nn?? As if n jambo jipyaa au geni??

Khaaaaah
 
Usinilize Mkuu nimezika Rafiki zangu wa Kiume 11 waliokuwa Wakilewa hapo na Rafiki zangu wa Kike 5 na Wote ni kwa Dally Kimoko Gitaa / UKIMWI Kipindi hicho hiyo Baa ikiwa ndiyo Talk of the Town hasa.
Dah pole sana mkuu kwa kupoteza vichwa 16 mfululizo. Tatizo la vijana wengi wa enzi zile walikuwa hawashauriki. Ukimshauri mtu asisahau kutumia kinga anapokuwa uvunguni, utasikia anakwambia kuwa yeye hawezi kula ndizi au pipi na ganda lake.

Au akijua jamaa yenu mmoja kaondoka na hiyo dally kimoko unasikia anakwambia ajali kazini au nzia kufia kwenye kidonda sio kesi.

Sasa siku ikifika upande wake ndo anaanza kutia huruma na kuwapa watu mzigo wasioweza kuubeba.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kumbe ushoga uko tangu zaman, sasa hizi kelele za nn?? As if n jambo jipyaa au geni??

Khaaaaah
Ushoga ulikuwepo, sema ulikuwa haujasambaa sana kama miaka hii. Miaka hiyo mashoga walikuwa wanaonekana zaidi maeneo kama hayo.
Sasa miaka hii wapo kila mahali, hawajifichi tena Bar kama miaka ile.
 
Habari zenu wana JF wenzangu.

Hivi ni Bar au maeneo gani ya starehe yanaweza kufikia sifa ilizokuwa nazo Bar ya Macheni enzi zake.

Hii Bar enzi za Prime Time yake iliweza kujibebea umaarufu hadi nje ya mipaka ya nchi yetu achilia mbali maeneo na mikoa mbali mbali ya Tanzania.

Mwaka 2003 wakati nipo ndani ya basi kutoka Lusaka kuelekea Harare nilikutana na mzambia fulani ambae tuliongea mengi kati ya tulioongea nilishangaa kuona jamaa aliifahamu hadi macheni Baa na alisema kwamba siku atakayofanikiwa kukanyaga Tanzania atajitahidi kufika katika Bar hiyo ili kujionea mwenyewe kwa macho yake yale yote aliyokuwa anahadithiwa na wazambia wenzake waliobahatika kukanyaga Dar na kwenda kula bata katika Bar hiyo.

Lakini pia nishakutana na watu kutoka katika nchi zingine za Congo, Burundi, Namibia na Kenya wakiizungumzia Bar hiyo kwa jinsi ilivyokuwa na mvuto kwa watu mbali mbali kutoka mataifa mbali mbali.

Sasa toka Bar hiyo ya macheni ilipoanguka sijawahi kusikia Bar zingine zenye sifa kubwa kama hiyo.

Je wewe ushawahi kuisikia nyingine yenye sifa zinazofanana na zile zile za kwa macheni? Kama ipo ni ipi? Najua kuna Bar na maeneo mengi yenye sifa na mvuto wa kiwango fulani ila sio kufikia viwango vya Bar ya Macheni.

Nyinyi au wewe unaonaje?

Karibuni tujadili.
Dah Nakumbuka hata marehemu alipatia ngwengwe kwa macheni
R.I.P Jackson M
 
Back
Top Bottom