Hukuelewa swali na umeshindwa kuuliza.
Mengine naomba nikujibu hapa chini japo hukuelewa swali langu.
Inaonekana unaishi kinadharia sana bila vitendo.
Hoja yako ya kuwa na maeneo chalinze au bagamoyo inaonyesha kabisa unaamini kwenye nadharia na hujui mambo vipi yanakwenda.Ingekuwa rahisi hivyo kuwa na wawekezaji na kiwanda kikajengwa bila shaka ungekuwa na viwanda vingi sana ukanda huo na ungekuwa mmoja wa mabilionea Tanzania maana huko maeneo bado ni bei rahisi sana kuliko maelezo na kama huna uwezo huo basi hukupaswa kuandika ulichoandika. Ingekuwa pia ni rahisi hivyo basi watanzania wengi sana tungekuwa matajiri maana unaamka tu unatafuta muwekezaji anakuja anakujengea kiwanda tayari rahisi tu kama hivyo maana eneo kubwa Tanzania liko wazi na marofa tu Tanzania wanamiliki maelfu ya maekari.
Hoja yako bado inaonyesha unaishi kinadharia na hujui mambo yanaendaje. Pia inaonyesha umesoma sana shule lakini huna exposure wala experience ya hicho ulichokariri, Recycling plant ya makaratasi unajua inauzwaje mpaka inaanza kazi na mtaji wa kukusanya hayo makaratasi harafu ulinganishe na faida yake that is business sio ndoto, Watanzania wangapi wanaweza kumudu??
Kupiga Soga JF ni vile tu hujui maisha ya kila unayemwita mpiga soga humu wakati wewe mwenyewe ni member humu.
Hayo mengine ya Fly over uko sawa upande wa nadharia maana hilo swali hata mtoto std seven anaweza kujibu vizuri mno.. Unachotakiwa kujua tu tunatakiwa tuwe nazo nyingi sana Dar hapo na kwenye miji mingine mikubwa na ile inayokua ndio tujipigie makofi sio kitu cha ajabu sana..
Usiwe mwepesi hivyo ndugu yangu, ongezea mawazo fikiri sana na upate wazo.
Yupo kijana mdogo wa kitanzania ambae ana-supply taka za karatasi kwenye recycling plant hapahapa Tanzania.
Hiyo Recycling Plant inapeleka material hayo kwenye kiwanda cha karatasi na hapo tunapata bahasha na mifuko inayotengenezwa Tanzania. bahasha nyingi ni za rangi ya khaki, unadhani zinatoka China?
Fuatilia hii kitu inaweza kukutoa kabisa kimaisha.
Anazikusanya kutoka sehemu mbalimbali nchini na ana compactors za kushindilia hizo malighafi na kuzipakia kwa uzuri.
Anaitwa Masawe kama sikosei na tayari ana tuzo ya uanamazingira bora kwa kusaidia kuondoak takataka mijini.
Fuatilia kipindi chaitwa Karakana kipo kila Jumatano kupitia Azam Two utajifunza mengi.
Halafu kwamba mimi naishi kinadharia ni kwamba hunifahamu tu mimi ni mjasiriamali wa kutupwa na nina mambo mengi mzuri kwa ustawi wa nchi yetu.
Kuhusu "Exposure" nakukaribisha sana kwa mawazo ya kujiendeleza kifikra na kiuchumi maana nina exposure ya kutosha kabisa kutoka sehemu nyingi duniani.
Tatizo la sisi waafrika ni kwamba wengi wetu tumefungwa akili na ukitaka kutoka kwenye hicho kifungo huna budi kupigana kwelikweli.
Na hapo ndipo wageni wanapotuchezea watakavyo.
Nimekupa wazo la bure kukutoa kwenye umaskini wewe unaleta masuala ya exposure!