Dar: Flyover ya Mfugale yazinduliwa. Chang'ombe na Gerezani kujengwa flyover, Barabara njia 8 kujengwa Kimara hadi Kibaha

Kule Zanzibar Flyover itajengwa lini? Au nchi ziliungana wapelekewe majeshi tu siku uchaguzi inatosha
 
Pesa za ndani MBONA wanasema za msaada wa Japan
ahaa kasema Japan wametoa bill 26
lakini kugusia miradi mingine ya stigler gorge kuwa N pesa za Ndani mara hizo reli nk
in short hotuba yake ni hile ile ya SIKU zote haijabadilika kitu
 

Hivi kaka yangu Misuli kweli umeaandika paragraph nzima umeshindwa kusema Japan katoa kiasi gani na Tanzania kiasi gani kaka yangu!? Sasa nimegundua kwanini hata rais alipofikia kwenye kutaja nani kachangia nini hakutaka kutaja kiwango kwani kilichokuwa kinasakwa ni sifa binafsi kwa Magufuli, ilionekana kingetajwa kiasi wajinga wangeona kumbe wanasifia bure bali sifa zilipaswa ziwaendee Wajapan. Hapa ndio pale tunapowaambia Magufuli anasema huu sio wakati wa siasa bali kazi, yeye ndio anayeendekeza siasa.

Sipingi maelezo yako mazuri, lakini lengo langu ni kukuambia yale tunayoambiwa Magufuli anayofanya ni mageni sio kweli maana hata watangulizi wake walikuwa wanategemea misaada na mikopo. Taswira inayojengwa ni kwamba miradi hii tunatekeleza kwa pesa zetu za ndani kitu ambacho sio kweli. Ukweli ni kwamba bado tunategemea misaada na sasa kuna mikopo mingi sana inayoendelea nyuma ya pazia ili kuaminisha umma kwamba uchumi wetu ni mzuri sana. Kama kweli wewe au rais wetu ni muungwani kipi kilimshinda kutaja mchango wa japani kwa figure na waTanzania wakati ameweza kutaja mradi mzima ulikuwa wa Bilioni 112? Tukifika hapo ndio huwa naamini kwamba taarifa nyingi toka serekalini hupikwa ili kuonyesha hali ni nzuri wakati ni kinyume chake.
 


Akanyage kwenye nyao, asishangae siku statement ikigeuzwa daraja likanyang'anywa jina
 
tunaanza lini kulipishwa kuvuka kama kile kivuko/daraja cha kigamboni...? this time punguzeni bei maana mnakamua sana malipo kwa hivi vivuko[emoji61]
nikitoka hom napitia daraja la kivukoni nalipa 2000 kwenda tu na hili jipya sijui mtaweka shingapi kuvuka... tufanye 1500 mpakaafika shambani kwangu jumla kwenda kurudi ni buks7 per day.. hebu jumlisha mwenyewe upate jibu la mwezi[emoji574] [emoji574] [emoji574] [emoji574] [emoji90]
 
Mkuu sema unataka siasa nyepesi.Soma mwanzoni mwa hii thread wameeleza ni kiasi gan.
 
Mbona kikwete hasifiwi katika, hizi salamu kama mwanzilishi wa mradi?
MISULI said:
Mnatapatapa sana. Mradi umeanza kujengwa 2016 na serikali inayoongozwa na jpm.jpm alikua na uwezo wa kupiga chini mipango yote ya jk lkn hana upumbavu ambao mnauonesha humu.Kama kaachana na mradi wa gesi na kaingia wa maji alishindwa nn kuachana na flyover?
 
Taa za kumulika meli iliyozama ili uokoaji uendelee wamekosa!
Na watu wamekufa kibudu!
Hizo barabara mnajenga mnataka wapite punda?
 
Tanzania hiyooooo.....Yes,tunalo dume bwana.Hongera Magufuli,nani kama wewe?
 
Taa za kumulika meli iliyozama ili uokoaji uendelee wamekosa!
Na watu wamekufa kibudu!
Hizo barabara mnajenga mnataka wapite punda?
Kivuko kilichopinduka saa nane mchana nani wa kufika saa 2 usiku akawa bado hai uko chini ya maji?
 

Hukuelewa swali na umeshindwa kuuliza.

Mengine naomba nikujibu hapa chini japo hukuelewa swali langu.
Inaonekana unaishi kinadharia sana bila vitendo.

Hoja yako ya kuwa na maeneo chalinze au bagamoyo inaonyesha kabisa unaamini kwenye nadharia na hujui mambo vipi yanakwenda.Ingekuwa rahisi hivyo kuwa na wawekezaji na kiwanda kikajengwa bila shaka ungekuwa na viwanda vingi sana ukanda huo na ungekuwa mmoja wa mabilionea Tanzania maana huko maeneo bado ni bei rahisi sana kuliko maelezo na kama huna uwezo huo basi hukupaswa kuandika ulichoandika. Ingekuwa pia ni rahisi hivyo basi watanzania wengi sana tungekuwa matajiri maana unaamka tu unatafuta muwekezaji anakuja anakujengea kiwanda tayari rahisi tu kama hivyo maana eneo kubwa Tanzania liko wazi na marofa tu Tanzania wanamiliki maelfu ya maekari.

Hoja yako bado inaonyesha unaishi kinadharia na hujui mambo yanaendaje. Pia inaonyesha umesoma sana shule lakini huna exposure wala experience ya hicho ulichokariri, Recycling plant ya makaratasi unajua inauzwaje mpaka inaanza kazi na mtaji wa kukusanya hayo makaratasi harafu ulinganishe na faida yake that is business sio ndoto, Watanzania wangapi wanaweza kumudu??

Kupiga Soga JF ni vile tu hujui maisha ya kila unayemwita mpiga soga humu wakati wewe mwenyewe ni member humu.

Hayo mengine ya Fly over uko sawa upande wa nadharia maana hilo swali hata mtoto std seven anaweza kujibu vizuri mno.. Unachotakiwa kujua tu tunatakiwa tuwe nazo nyingi sana Dar hapo na kwenye miji mingine mikubwa na ile inayokua ndio tujipigie makofi sio kitu cha ajabu sana..
 
Kivuko kilichopinduka saa nane mchana nani wa kufika saa 2 usiku akawa bado hai uko chini ya maji?
Mtu amewahi kukaa kwenye tumbo la samaki kwa siku tatu na hakufa! Wewe sijui ukoje!!!
 
Mkuu sema unataka siasa nyepesi.Soma mwanzoni mwa hii thread wameeleza ni kiasi gan.

Mkuu ninafahamu ninachouliza. Aliyeleta huu uzi anatumia ID fake yeye kasema mradi ni wa 92b, rais anasema mradi ni 110b+. Sasa hapo tushike lipi? Jana umenzishwa uzi mwingine unasema flyover hiyo imesaidia kwani taifa lilikuwa linapoteza 400b@month, leo rais anasema ni 400b@year. Sasa katika mazingira haya tumsikilize rais au tuamini hizi id fake humu ndani?
 
Huyo aliyesema 400b kwa mwezi nafikir alikosea tu ila usahihi ni kwa mwaka na hii ni kwa Dar nzima.mwanzo umesema Rais hajataja kiwango saiz unasema kasema 110+.Nikianza nawewe, usahihi wa arguments zako ni upi?
 
Kwa mujibu wa maelezo ya mtoa mada,Mkurugenzi mtendaji wa Tanroads anadai gharama za daraja ni bilion 92,kwenye maelezo ya Rais ametaja gharama ni bilioni 106 ndugu mtoa mada hebu hakiki taarifa zako kwanza au ni mimi nimeshindwa kuelewa.
 
Huyo aliyesema 400b kwa mwezi nafikir alikosea tu ila usahihi ni kwa mwaka na hii ni kwa Dar nzima.mwanzo umesema Rais hajataja kiwango saiz unasema kasema 110+.Nikianza nawewe, usahihi wa arguments zako ni upi?

Misuli pitia post yangu vizuri, nimesema rais kataja mradi mzima ni kiasi gani, lakini sio Japan kiasi gani au Tanzania kiasi gani. Unasema niangalie post namba moja. Angalia kiwango anachotaja huyo Elias Kuandikwa anataja kiasi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…