Sheria kandamizi, majina yasiyo reflect interest za taifa yatafutwa! Mfugalle ni kwa vile walikuwa maswahiba wanakula pamoja, watu wana kumbukumbu sahihi!Mmh...wakati utasema kama kweli...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sheria kandamizi, majina yasiyo reflect interest za taifa yatafutwa! Mfugalle ni kwa vile walikuwa maswahiba wanakula pamoja, watu wana kumbukumbu sahihi!Mmh...wakati utasema kama kweli...
haahahhaahhaataratibu rafiki yangu si unajua tena nchi hii si salama! Naona sheikh wa Dar yupo, eti anye anasali, huyo Mungu simtaki, nitatafuta wa kwangu asiyehusiana na huyo Sheikh!
Hayakuwa sanctioned na JK! mind! haya yanakuwa sanctioned na yule baba yetu wa Mbinguni,everybody knows. KJ has necer been implicated in those killingsm but this one is implicated even by you, misuli!Mwangosi,mauaji Arusha, ulimboka, kibamba haya yalitokea China. Bora uwe MCHAWI KULIKO MNAFKI.
Kwanza kuna miradi kibao imekwama, ishu ingekua ni mkataba kusingekuwa na story za miradi kukwama.Mi nadhani Kikwete aliridhika na sifa alizopata ndio maana akaachia madaraka. Kama angekuwa anahitaji kuendelea kupta sifa basi angebadili katiba ili aendelee kuongoza. Hata kama Kikwete aliomba pesa na Magufuli akakamilisha huo mradi basi Magufuri anastahili pongezi zaidi, inawezekana ulikuwa mdogo huko nyuma kuna rais alipewa hela kwa ajri ya ujenzi wa daraja la Mkapa, hela zikaja wakati yeye ametoka madarakani na rais aliyeopo akazitumia zile hela kufanya uchaguzi wa serikari za mitaa. Sasa hapo nadhani utaelewa kwanini Magufuri anastahili pongezi
Tulikotoka
Ujenzi wa daraja hilo lililopewa jina la Mfugale ulioanza miaka miwili iliyopita umegharimu Sh bilioni 92 hadi kukamilika kwake, huku Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (JICA) likichangia Sh bilioni 26. Jina la Mfugale limetokana na jina la Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale, ambaye Rais Magufuli alisema amekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu nchini na kumpa heshima ya kulitunuku daraja hilo jina lake.
Mkataba wa ujenzi wa daraja hilo, ulisainiwa Oktoba 15, mwaka 20 1 5 kati ya Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads) na Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd. Juzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kuanzia saa 2 asubuhi huku akiwataka wananchi, viongozi wa siasa kutoka vyama mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi huo wenye historia ya kipekee nchini.
View attachment 879144
Rais Magufuli amewasili katika eneo hilo zinapokutana barabara za Mandela na Nyerere na amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda
RC Makonda
Makonda wakati anamkaribisha Rais amemsifu na kumwambia kuwa ujenzi wa fly-over hiyo utaondoa usumbufu wa msongamano wa barabarani na kusaidia watu kuwahi maofisini, majumbani na hata Airport
"Tumewaalika wabunge wote wa Dar katika Uzinduzi wa ‘Flyover’ ya Mfugale ila Wabunge wa Kawe, Ubungo na Kibamba hawajaja... aaah!
Ndoa za wengi zilitetereka kutokana na foleni ya TAZARA, wengine walidanganya kumbe walikuwa ‘guest’ tu
Daraja la Nyerere la Kigamboni kwa sasa linaingiza takribani Tsh. Milioni 800 kwa mwezi"
Pia amemuomba Rais afanye ziara katika Mkoa wa Dar kwani wanahitaji sana ziara hiyo na wanaona wivu anapokuwa katika mikoa mingine na kupiga picha na wananchi
Mkurugenzi Mtendaji TANROADs
Mwaka 2008, Tanzania iliandaa ‘Master Plan’ ya kupunguza msongamano jijini Dar. 2013 Japan wakajitokeza kuwa watatusaidia kujenga daraja hili; 2014 ilitangazwa tenda! Wazabuni walikuja na gharama kubwa
Japan iliongeza ufadhili hadi Bilioni 103 mwaka 2015 Machi, Mkandarasi mmoja alikuja lakini gharama zake zilikuwa mara mbili zaidi. Tulifanya ‘Selective Tendering’ ambapo mkandarasi aliyejenga daraja hili alipatikana
Daraja hili limejengwa kwa nguzo kubwa 26; zimekaa juu ya Piles 133. Daraja lina urefu wa zaidi ya km 1. Linaweza kubeba tani 180 kwa wakati mmoja. Daraja hili linaweza kutumika kwa zaidi ya miaka 100. Limejengwa kwa jumla ya Sh. Bilioni 92
Tunao mkakati wa kujenga BRT ya kutoka mjini(CBD) hadi Gongo la Mboto katika awamu ya 3
Balozi wa Japan
Naamini watanzania wote wamefurahi kuona Flyover ya kwanza nchini Tanzania. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Nafarijika kuwa nikiwa narudi Japan nitatumia ‘Mfugale Flyover’
Eng. Ninatubu Lema(ERB)
Mhandisi Patrick Aaron Lipilima Mfugale ametumikia taaluma ya Uhandisi kwa miaka 41
- Alizaliwa Ifunda, Iringa na alikamaliza Sekondari mwaka 1975. Alipata 1st Degree nchini India, Masters nchini Uingereza
- Aliajiriwa Wizara ya Ujenzi 1977
Mfugale ametumia muda wake mwingi wa kazi kama Mtaalamu wa Madaraja. Alibuni daraja la Malagarasi; ameshiriki ktk ujenzi wa madaraja ya Mkapa, Umoja, Rusumo, Kikwete, Nyerere, Mto Sibiti, Kilombero na mengine mengi (zaidi ya 1,400 nchini)
Mhandisi Patrick Mfugale ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS; leo atapata heshima kubwa sana kwa Flyover ya kwanza Tanzania kupewa jina lake!
Elias J. Kwandikwa
Mradi huu jumla umegharimu Bilioni 106. Serikali ya Tanzania imegharimia kodi zote. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Toka Flyover imeanza kutumika, msongamano eneo la TAZARA umepungua kwa kiwango kikubwa
Miradi inayotarajiwa jijini Dar kwa kushirikiana na JICA:
> Upanuzi wa barabara ya Morocco - Mwenge
> Ujenzi wa Daraja la Gerezani (Kariakoo)
Rais Magufuli
Natoa pole kwa familia zilizoondokewa na wapendwa wao kufuatia ajali ya #MVNyerere na kuwaombea majeruhi uponyaji wa haraka. Nawashukuru watanzania kwa mshikamano walioonyesha
Ajali hii ya #MVNyerere iwe funzo kwetu. Ajali kama hizi zinaepukika, na zikitokea basi madhara yake yanaweza kuwa madogo kama tukipata funzo kwa kilichotokea
Nawapongeza Wizara ya Ujenzi, TANROADS na Wahandisi washauri kwa kusimamia ujenzi wa #MfugaleFlyover. Daraja limegharimu Bilioni 106.65; Japan wamechangia kiwango kikubwa cha pesa hii, ni marafiki wa kweli kwenye masuala ya maendeleo
Nampongeza Mbarawa ambaye alikuwa Waziri wa Ujenzi wakati ujenzi wa #MfugaleFlyover unaanza
Nakumbuka wakati Daraja la Umoja linaandaliwa kujengwa, nilimwita Mfugale anisaidie design ya Daraja hilo; nilipoipeleka kwa marais wa Tanzania na Msumbiji, ikapitishwa. Wakati wa uzinduzi wala hakutambulishwa
Mwaka 2008 Mfugale na mwenzake walipewa maagizo wakayakataa, Katibu Mkuu wa wakati huo aliwaokoa; mwenzake (marehemu Mjungi) alijiua kwa kujipiga risasi lakini Mfugale alivumilia. Ndo gharama ya kusimamia maadili
Ujenzi wa Flyover ya Ubungo itagharimu Bilioni 247. Itakuwa flyover ya aina yake kwa hapa Dar es Salaam! Wazaramo watasema ‘Ina ghorofa 3’
Tunajenga barabara ya njia 6 kutoka Kimara kwenda Kibaha kwa Sh. Bilioni 140 na fedha zote zinatolewa na Serikali ya Tanzania. Kutakuwa pia na njia ndogo 2 (service road). Bomoabomoa ya Kimara ilizingatia sheria!
Katika #MfugaleFlyover, nataka zifungwe kamera kote! Kazi hii ianze mara moja. Hatutaki watu wajiue hapa. Na madaraja mengine yote yatakayojengwa yawekewe kamera
Kwa kazi alizozifanya Eng. Mfugale, Flyover hii ilistahili kuitwa jina lake. Hakupendelewa, ni haki yake. Wataalamu wengine wamuige!
Gharama za umeme hapa nchini ni kubwa mno. Ni kikwazo katika ushindani wa viwanda. Bila umeme wa uhakika, viwanda ni ndoto!
Naomba flyover ya Gerezani ifanyiwe kazi ambayo tayari hadi tenda yake imeshatangazwa
Nawaomba Japan pia waikumbuke barabara ya Morocco-Mwenge waliyoahidi, imechukua muda mrefu!
Baadhi ya mikwamo hapa nchini imeletwa na wataalam ambao ni watanzania wenzetu! Wataalam wetu walipendekeza vyoo vya mradi wa Stiegler's Gorge vijengwe kilomita 10 toka eneo la mradi...
Miradi hii inaumiza baadhi ya watu. Tusitumike kukwamisha maendeleo ya watanzania. Yapo mengi tunayaweza kwa fedha zetu. Fedha za kujenga Stiegler's Gorge zipo!
Hatuwezi kuingia Uchumi wa Kati wakati tuna umeme unaokatikakatika. Hatuwezi kwenda huko bila kuwa na Flyovers, miundombinu ya Reli n.k. Maendeleo hayana chama!
Rais Magufuli kuzindua Flyover ya TAZARA. Yamaliza Foleni iliyokuwa ikisababisha hasara ya Tsh. Bilioni 400 kwa Mwezi - JamiiForums
"ENG MFUGALE - 1st degree India na Masters nchini India, ameshirii kudesign madaraja mengi nchini."
Sijui tunajifunza nini hapa hasa kwenye hii dhana yetu ya Tanzania ya Viwanda na kuzalisha kizazi chenye tija kwa Taifa.
Hahahahahahah kwa akili hii ccm itawale milele.Kama kiongoz wa nchi alichukua hatua gani kwa mauaji ya Arusha?Kamanda wa polisi alifukuzwa kazi au alipandishwa cheo?Unafki unawatesa sana,yaani mabaya yote enzi za jk mnamtenga nayo ila kwa jpm lzm yamhusu.Tumepigwa sana mabomu chuo kikuu, nyumba zimebolewa sana lkn mtu anaibuka leo anakuambia haya yote sio jk.Hayakuwa sanctioned na JK! mind! haya yanakuwa sanctioned na yule baba yetu wa Mbinguni,everybody knows. KJ has necer been implicated in those killingsm but this one is implicated even by you, misuli!
Wewe ni great SINKER. Kwa akili hii ccm itawale milele.Hivi Mkazi wa Bunju au Mapinga ananufaikaje na hii flyover?
Usipende kuwa mwongo na mpotoshaji.
Mhandisi Patrick Mfugale masters yake amesomea Uingereza.
Kule ndiko khasa amejifunza kujenga madaraja kama hili la Mfugale.
Amejenga madaraja 1400 nchi nzima.
Ni mwanamama huyoHahahaha ni wa kike au wa kiume. Huyo dc maana yule mama terry wa tcra aliambiwaga na hao madanga kwamba ata mume wake naye wanaruka naye tena anazungushiwa kiuno mpaka naniliu ulihisi inacharangwa charangwa kama kachumbari. Chezea madanga wa town. Wakituma polis, polis wanakopeshwa kesho madang yanarudi mtaani.
Ila sishangai jiwe anachakuaga vichaa kama yeye
Mkuu hayajafanyika..!Uzinduzi huendana na utenguzi,tusubiri.
Hicho kizungu cha ugoko peleka kulee.Of course he was as you have described, but there are some issues to comprehend! alikuwa dhaifu sana, tena sana... lakini hakuwa dictator, hakuua watu, hakuna miili iliyookotwa Coco beach, Hakuna Ben Saanane, hakuna Mawazo etc.
mjomba pokea kama ulivyoelezwa ubishi wa nini sasa ?Tuwekewe sawa jamani hiyo figure ya 400 Billion inafikiwaje?
Astaghafillulah !taratibu rafiki yangu si unajua tena nchi hii si salama! Naona sheikh wa Dar yupo, eti anye anasali, huyo Mungu simtaki, nitatafuta wa kwangu asiyehusiana na huyo Sheikh!
Samahani ni makosa ya kiuandishi uko sahihi, swali langu watanzania tunajifunza nini hasa kwenye dhana hii ya Tanzania ya viwanda?