Dar: Flyover ya Mfugale yazinduliwa. Chang'ombe na Gerezani kujengwa flyover, Barabara njia 8 kujengwa Kimara hadi Kibaha

Dar: Flyover ya Mfugale yazinduliwa. Chang'ombe na Gerezani kujengwa flyover, Barabara njia 8 kujengwa Kimara hadi Kibaha

Mmh...wakati utasema kama kweli...
Sheria kandamizi, majina yasiyo reflect interest za taifa yatafutwa! Mfugalle ni kwa vile walikuwa maswahiba wanakula pamoja, watu wana kumbukumbu sahihi!
 
taratibu rafiki yangu si unajua tena nchi hii si salama! Naona sheikh wa Dar yupo, eti anye anasali, huyo Mungu simtaki, nitatafuta wa kwangu asiyehusiana na huyo Sheikh!
haahahhaahhaa
 
Mwangosi,mauaji Arusha, ulimboka, kibamba haya yalitokea China. Bora uwe MCHAWI KULIKO MNAFKI.
Hayakuwa sanctioned na JK! mind! haya yanakuwa sanctioned na yule baba yetu wa Mbinguni,everybody knows. KJ has necer been implicated in those killingsm but this one is implicated even by you, misuli!
 
"ENG MFUGALE - 1st degree India na Masters nchini Uingereza, ameshiriki kudesign madaraja mengi nchini."

Sijui tunajifunza nini hapa hasa kwenye hii dhana yetu ya Tanzania ya Viwanda na kuzalisha kizazi chenye tija kwa Taifa.
 
Mi nadhani Kikwete aliridhika na sifa alizopata ndio maana akaachia madaraka. Kama angekuwa anahitaji kuendelea kupta sifa basi angebadili katiba ili aendelee kuongoza. Hata kama Kikwete aliomba pesa na Magufuli akakamilisha huo mradi basi Magufuri anastahili pongezi zaidi, inawezekana ulikuwa mdogo huko nyuma kuna rais alipewa hela kwa ajri ya ujenzi wa daraja la Mkapa, hela zikaja wakati yeye ametoka madarakani na rais aliyeopo akazitumia zile hela kufanya uchaguzi wa serikari za mitaa. Sasa hapo nadhani utaelewa kwanini Magufuri anastahili pongezi
Kwanza kuna miradi kibao imekwama, ishu ingekua ni mkataba kusingekuwa na story za miradi kukwama.
 



Tulikotoka

Ujenzi wa daraja hilo lililopewa jina la Mfugale ulioanza miaka miwili iliyopita umegharimu Sh bilioni 92 hadi kukamilika kwake, huku Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (JICA) likichangia Sh bilioni 26. Jina la Mfugale limetokana na jina la Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads), Patrick Mfugale, ambaye Rais Magufuli alisema amekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu nchini na kumpa heshima ya kulitunuku daraja hilo jina lake.

Mkataba wa ujenzi wa daraja hilo, ulisainiwa Oktoba 15, mwaka 20 1 5 kati ya Wakala wa Taifa wa Barabara (Tanroads) na Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd. Juzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika kuanzia saa 2 asubuhi huku akiwataka wananchi, viongozi wa siasa kutoka vyama mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi huo wenye historia ya kipekee nchini.


View attachment 879144

Rais Magufuli amewasili katika eneo hilo zinapokutana barabara za Mandela na Nyerere na amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

RC Makonda

Makonda wakati anamkaribisha Rais amemsifu na kumwambia kuwa ujenzi wa fly-over hiyo utaondoa usumbufu wa msongamano wa barabarani na kusaidia watu kuwahi maofisini, majumbani na hata Airport

"Tumewaalika wabunge wote wa Dar katika Uzinduzi wa ‘Flyover’ ya Mfugale ila Wabunge wa Kawe, Ubungo na Kibamba hawajaja... aaah!

Ndoa za wengi zilitetereka kutokana na foleni ya TAZARA, wengine walidanganya kumbe walikuwa ‘guest’ tu

Daraja la Nyerere la Kigamboni kwa sasa linaingiza takribani Tsh. Milioni 800 kwa mwezi"

Pia amemuomba Rais afanye ziara katika Mkoa wa Dar kwani wanahitaji sana ziara hiyo na wanaona wivu anapokuwa katika mikoa mingine na kupiga picha na wananchi

Mkurugenzi Mtendaji TANROADs

Mwaka 2008, Tanzania iliandaa ‘Master Plan’ ya kupunguza msongamano jijini Dar. 2013 Japan wakajitokeza kuwa watatusaidia kujenga daraja hili; 2014 ilitangazwa tenda! Wazabuni walikuja na gharama kubwa

Japan iliongeza ufadhili hadi Bilioni 103 mwaka 2015 Machi, Mkandarasi mmoja alikuja lakini gharama zake zilikuwa mara mbili zaidi. Tulifanya ‘Selective Tendering’ ambapo mkandarasi aliyejenga daraja hili alipatikana

Daraja hili limejengwa kwa nguzo kubwa 26; zimekaa juu ya Piles 133. Daraja lina urefu wa zaidi ya km 1. Linaweza kubeba tani 180 kwa wakati mmoja. Daraja hili linaweza kutumika kwa zaidi ya miaka 100. Limejengwa kwa jumla ya Sh. Bilioni 92

Tunao mkakati wa kujenga BRT ya kutoka mjini(CBD) hadi Gongo la Mboto katika awamu ya 3

Balozi wa Japan

Naamini watanzania wote wamefurahi kuona Flyover ya kwanza nchini Tanzania. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Nafarijika kuwa nikiwa narudi Japan nitatumia ‘Mfugale Flyover’

Eng. Ninatubu Lema(ERB)

Mhandisi Patrick Aaron Lipilima Mfugale ametumikia taaluma ya Uhandisi kwa miaka 41
- Alizaliwa Ifunda, Iringa na alikamaliza Sekondari mwaka 1975. Alipata 1st Degree nchini India, Masters nchini Uingereza
- Aliajiriwa Wizara ya Ujenzi 1977

Mfugale ametumia muda wake mwingi wa kazi kama Mtaalamu wa Madaraja. Alibuni daraja la Malagarasi; ameshiriki ktk ujenzi wa madaraja ya Mkapa, Umoja, Rusumo, Kikwete, Nyerere, Mto Sibiti, Kilombero na mengine mengi (zaidi ya 1,400 nchini)

Mhandisi Patrick Mfugale ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS; leo atapata heshima kubwa sana kwa Flyover ya kwanza Tanzania kupewa jina lake!

Elias J. Kwandikwa

Mradi huu jumla umegharimu Bilioni 106. Serikali ya Tanzania imegharimia kodi zote. Daraja hili litapunguza msongamano jijini Dar. Toka Flyover imeanza kutumika, msongamano eneo la TAZARA umepungua kwa kiwango kikubwa

Miradi inayotarajiwa jijini Dar kwa kushirikiana na JICA:
> Upanuzi wa barabara ya Morocco - Mwenge
> Ujenzi wa Daraja la Gerezani (Kariakoo)

Rais Magufuli

Natoa pole kwa familia zilizoondokewa na wapendwa wao kufuatia ajali ya #MVNyerere na kuwaombea majeruhi uponyaji wa haraka. Nawashukuru watanzania kwa mshikamano walioonyesha

Ajali hii ya #MVNyerere iwe funzo kwetu. Ajali kama hizi zinaepukika, na zikitokea basi madhara yake yanaweza kuwa madogo kama tukipata funzo kwa kilichotokea

Nawapongeza Wizara ya Ujenzi, TANROADS na Wahandisi washauri kwa kusimamia ujenzi wa #MfugaleFlyover. Daraja limegharimu Bilioni 106.65; Japan wamechangia kiwango kikubwa cha pesa hii, ni marafiki wa kweli kwenye masuala ya maendeleo

Nampongeza Mbarawa ambaye alikuwa Waziri wa Ujenzi wakati ujenzi wa #MfugaleFlyover unaanza

Nakumbuka wakati Daraja la Umoja linaandaliwa kujengwa, nilimwita Mfugale anisaidie design ya Daraja hilo; nilipoipeleka kwa marais wa Tanzania na Msumbiji, ikapitishwa. Wakati wa uzinduzi wala hakutambulishwa

Mwaka 2008 Mfugale na mwenzake walipewa maagizo wakayakataa, Katibu Mkuu wa wakati huo aliwaokoa; mwenzake (marehemu Mjungi) alijiua kwa kujipiga risasi lakini Mfugale alivumilia. Ndo gharama ya kusimamia maadili

Ujenzi wa Flyover ya Ubungo itagharimu Bilioni 247. Itakuwa flyover ya aina yake kwa hapa Dar es Salaam! Wazaramo watasema ‘Ina ghorofa 3’

Tunajenga barabara ya njia 6 kutoka Kimara kwenda Kibaha kwa Sh. Bilioni 140 na fedha zote zinatolewa na Serikali ya Tanzania. Kutakuwa pia na njia ndogo 2 (service road). Bomoabomoa ya Kimara ilizingatia sheria!

Katika #MfugaleFlyover, nataka zifungwe kamera kote! Kazi hii ianze mara moja. Hatutaki watu wajiue hapa. Na madaraja mengine yote yatakayojengwa yawekewe kamera

Kwa kazi alizozifanya Eng. Mfugale, Flyover hii ilistahili kuitwa jina lake. Hakupendelewa, ni haki yake. Wataalamu wengine wamuige!

Gharama za umeme hapa nchini ni kubwa mno. Ni kikwazo katika ushindani wa viwanda. Bila umeme wa uhakika, viwanda ni ndoto!

Naomba flyover ya Gerezani ifanyiwe kazi ambayo tayari hadi tenda yake imeshatangazwa

Nawaomba Japan pia waikumbuke barabara ya Morocco-Mwenge waliyoahidi, imechukua muda mrefu!

Baadhi ya mikwamo hapa nchini imeletwa na wataalam ambao ni watanzania wenzetu! Wataalam wetu walipendekeza vyoo vya mradi wa Stiegler's Gorge vijengwe kilomita 10 toka eneo la mradi...

Miradi hii inaumiza baadhi ya watu. Tusitumike kukwamisha maendeleo ya watanzania. Yapo mengi tunayaweza kwa fedha zetu. Fedha za kujenga Stiegler's Gorge zipo!

Hatuwezi kuingia Uchumi wa Kati wakati tuna umeme unaokatikakatika. Hatuwezi kwenda huko bila kuwa na Flyovers, miundombinu ya Reli n.k. Maendeleo hayana chama!

Rais Magufuli kuzindua Flyover ya TAZARA. Yamaliza Foleni iliyokuwa ikisababisha hasara ya Tsh. Bilioni 400 kwa Mwezi - JamiiForums

Hivi Mkazi wa Bunju au Mapinga ananufaikaje na hii flyover?
 
"ENG MFUGALE - 1st degree India na Masters nchini India, ameshirii kudesign madaraja mengi nchini."

Sijui tunajifunza nini hapa hasa kwenye hii dhana yetu ya Tanzania ya Viwanda na kuzalisha kizazi chenye tija kwa Taifa.

Usipende kuwa mwongo na mpotoshaji.

Mhandisi Patrick Mfugale masters yake amesomea Uingereza.

Kule ndiko khasa amejifunza kujenga madaraja kama hili la Mfugale.

Amejenga madaraja 1400 nchi nzima.
 
Hayakuwa sanctioned na JK! mind! haya yanakuwa sanctioned na yule baba yetu wa Mbinguni,everybody knows. KJ has necer been implicated in those killingsm but this one is implicated even by you, misuli!
Hahahahahahah kwa akili hii ccm itawale milele.Kama kiongoz wa nchi alichukua hatua gani kwa mauaji ya Arusha?Kamanda wa polisi alifukuzwa kazi au alipandishwa cheo?Unafki unawatesa sana,yaani mabaya yote enzi za jk mnamtenga nayo ila kwa jpm lzm yamhusu.Tumepigwa sana mabomu chuo kikuu, nyumba zimebolewa sana lkn mtu anaibuka leo anakuambia haya yote sio jk.
 
Usipende kuwa mwongo na mpotoshaji.

Mhandisi Patrick Mfugale masters yake amesomea Uingereza.

Kule ndiko khasa amejifunza kujenga madaraja kama hili la Mfugale.

Amejenga madaraja 1400 nchi nzima.

Samahani ni makosa ya kiuandishi uko sahihi, swali langu watanzania tunajifunza nini hasa kwenye dhana hii ya Tanzania ya viwanda?
 
Hahahaha ni wa kike au wa kiume. Huyo dc maana yule mama terry wa tcra aliambiwaga na hao madanga kwamba ata mume wake naye wanaruka naye tena anazungushiwa kiuno mpaka naniliu ulihisi inacharangwa charangwa kama kachumbari. Chezea madanga wa town. Wakituma polis, polis wanakopeshwa kesho madang yanarudi mtaani.

Ila sishangai jiwe anachakuaga vichaa kama yeye
Ni mwanamama huyo
 
Of course he was as you have described, but there are some issues to comprehend! alikuwa dhaifu sana, tena sana... lakini hakuwa dictator, hakuua watu, hakuna miili iliyookotwa Coco beach, Hakuna Ben Saanane, hakuna Mawazo etc.
Hicho kizungu cha ugoko peleka kulee.
 
RC Makonda

Makonda wakati anamkaribisha Rais amemsifu na kumwambia kuwa ujenzi wa fly-over hiyo utaondoa usumbufu wa msongamano wa barabarani na kusaidia watu kuwahi maofisini, majumbani na hata Airport

"Tumewaalika wabunge wote wa Dar katika Uzinduzi wa ‘Flyover’ ya Mfugale ila Wabunge wa Kawe, Ubungo na Kibamba hawajaja... aaah!

Ndoa za wengi zilitetereka kutokana na foleni ya TAZARA, wengine walidanganya kumbe walikuwa ‘guest’ tu

Daraja la Nyerere la Kigamboni kwa sasa linaingiza takribani Tsh. Milioni 800 kwa mwezi"

Pia amemuomba Rais afanye ziara katika Mkoa wa Dar kwani wanahitaji sana ziara hiyo na wanaona wivu anapokuwa katika mikoa mingine na kupiga picha na wananchi

Wakuu mliokuwepo au kufuatilia tafadhali mseme. Maana…….
 
Samahani ni makosa ya kiuandishi uko sahihi, swali langu watanzania tunajifunza nini hasa kwenye dhana hii ya Tanzania ya viwanda?

Haina shida mkuu kuwekana sawa ni moja ya mambo ya msingi wa JF.

Ukiwa na barabara za juu kama hizi na za kutosha basi unafungua njia nyingi za kusafirisha bishaa za viwandani na kukurahisisha biashara zingine nyingi tu.

Kwa mfano huko Uingereza alikosomea hayo mambo, wao wakati wa usiku ndo utaona malori na magari mengine maarufu kwa jina la Van ndo yanasafirisha bidhaa mbalimbali kati ya miji mingi nchini humo.

Hii inasaidia kuondoa kelele katika barabara za kawaida na kuleta misongamano.

Ikikamilika hiyo Ubungo Interchange basi bidhaa za viwandani, mashambani na za kutoka sehemu zingine kama bandarini zitakuwa zikisafirishwa kwa muda mfupi na pembezoni mwa barabara hizo watanzania wanaweza kujenga viwanda vyao vya aina mbalimbali.

Urahisi huo ni wa kufikisha bidhaa zhizo sokoni pameoma kutoka mashambani au kwenye mabohari.

Ukiangalia viwanda vya barabara ya Nyerere ni mfano wa viwanda vitakavyojengwa pembezoni mwa hiyo Ubungo Interchange.

Uchumi unatagemea sana barabara na viwanda vinatagemea barabara.

Nikupe wazo, tafuta eneo kubwa la ardhi kuelekea Chalinze na uikilipata basi tengeneza wazo la kuwa na kiwanda hata kidogo tu.

Ukiishafanya hivyo basi tafuta mwekezaji wa ndani au wa nje ambae atakujengea kiwanda chako na mtaanza kula faida pamoja baada ya hapo uzalishaji utakaanza kushika kasi..

Kwasababu mwekezaji wa kigeni haruhusiwi kumiliki ardhi lakini anaweza kushirikiana na mzawa kujenga kiwanda hicho.

Nakupa wazo la kujenga kiwanda cha urejereshaji au Recycling na takataka zote za aina ya karatasi unakuwa ukizitoa mikoa yote ya Tanzania je utaweza kufanya hivyo?

Ukifanya hivyo utaajiri watanzania na utalipa kodi na pia utawezesha uchumi wa viwanda.

Unaweza kuja kujikuta wewe ni mmoja wa matajiri fulani hivi ndani ya miaka 5.

Usishinde JF kupiga soga tu.
 
Back
Top Bottom