Dar: Hafla ya BAWACHA Mikocheni yazingirwa na Polisi, wapewa dakika 30 tu

Jana Lissu alisema Mwendazake amekufa lakini waliokua wakimsaidia kutesa na kuumiza watu hawajafa. Bado wapo. Wanaweza kuwa wameficha makucha tu kwa muda lakini wakishamsoma mama, watarudi tu.

Na hiki ndicho kilichotokea. Polisi wenye silaha wamezingira ukumbi wa Hekima Garden, Mikocheni kuzuia hafla ya chakula cha jioni iliyoandiwa na Baraza la wanawake la Chadema (BAWACHA).

Iko hivi, Bawacha wameandaa hafla ya kuwakutanisha wanawake wa Chadema kubadilishana mawazo na kuzungumza mambo yao kama akina mama.

Wakaandika barua kwa Mkurugenzi kumpa taarifa. Lakini Mkurugenzi akasema wapeleke maombi yao kwa DC. Wakapeleka barua kwa DC Gondwe. Katika hali ya kushangaza Gondwe eti nae akaagiza barua ipelekwe kwa RC. Yani danadana zisizo na ulazima wowote. Yani akina mama kukaa na kula kuku zao hadi RC atoe ruhusa?

Anyway, barua ikapelekwa kwa RC lakini Makalla akaingia mitini. Hataki kujibu. Baada ya kusumbuliwa sana akaagiza waende kwa RPC Kinondoni. RPC kaagiza waende kwa OCD Oysterbay. OCD akaruhusu hafla ifanyike kwa masharti yafuatayo;

1. Pasiwepo na mziki.
2. Pasiwepo na pombe.
3. Hafla ifanyike kwa dakika 30 tu.
4. Askari waingie ukumbini kusikiliza wanachojadili.
5. Wakimaliza kula watawanyike haraka.

Wanawake wa BAWACHA wamegomea masharti hayo, wanataka wawe huru kufanya mambo yao.

#MyTake;
Mama kemea hawa watu watakuharibia sasa hivi. Hawa akina mama ni wanawake wenzako. Wameamua kukaa, kula na kujadili mambo yao. Kwanini wananyanyaswa? Mwendazake aliwabagua watu kwa vyama vyao. Wapinzani wakawa mistreated kama vile magaidi. Wakapigwa, wakateswa na kunyanyaswa bila sababu.

Wewe ulianza vizuri kwa kuliunganisha taifa. Ukaahidi kuganga makovu yetu. Ukasema tusahau yaliyopita na tufute machozi. Lakini badala ya kutufuta machozi, mbona watu wako wameanza kutuletea machozi tena? Tafadhali wakemee. Jana tumefanya kongamano zuri la Katiba, na dunia imekupongeza kwa sababu polisi hawakutusumbua. Lakini leo hawa akina mama wanasumbuliwa? What happened?
Hapa siyo mahala pake kwa maana mama yahuko hapa. Pili mahakama ziko pelekeni kesi mahakamani.
 
Kama hii ni kweli kama inavyoripotiwa hapa basi nitajua ni wazi kabisa kwamba viongozi wa CCM ni kizazi cha nyoka.

Tutakuwa taifa ambalo watu wake ni wa mwisho duniani kwa kukosa uhuru. Na nitasema heri hata wakati wa mkoloni wa Kiingereza. Ukoloni wa CCM ni ukoloni wa kutisha, kuteka, kubambikia makesi na kuua?

Mama unanihuzunisha sana. Just when we thought we were getting to the top we find that we have hit bottom!!!!!
Hama nchi, nye nye nye mob, actions zero. Hameni basi
 
Hapa siyo mahala pake kwa maana mama yahuko hapa. Pili mahakama ziko pelekeni kesi mahakamani.
Nakuona ukiwa kazini kwa kujipatia mkate wako wa kila siku
JamiiForums1992601550.jpg
 
Jana Lissu alisema Mwendazake amekufa lakini waliokua wakimsaidia kutesa na kuumiza watu hawajafa. Bado wapo. Wanaweza kuwa wameficha makucha tu kwa muda lakini wakishamsoma mama, watarudi tu.

Na hiki ndicho kilichotokea. Polisi wenye silaha wamezingira ukumbi wa Hekima Garden, Mikocheni kuzuia hafla ya chakula cha jioni iliyoandiwa na Baraza la wanawake la Chadema (BAWACHA).

Iko hivi, Bawacha wameandaa hafla ya kuwakutanisha wanawake wa Chadema kubadilishana mawazo na kuzungumza mambo yao kama akina mama.

Wakaandika barua kwa Mkurugenzi kumpa taarifa. Lakini Mkurugenzi akasema wapeleke maombi yao kwa DC. Wakapeleka barua kwa DC Gondwe. Katika hali ya kushangaza Gondwe eti nae akaagiza barua ipelekwe kwa RC. Yani danadana zisizo na ulazima wowote. Yani akina mama kukaa na kula kuku zao hadi RC atoe ruhusa?

Anyway, barua ikapelekwa kwa RC lakini Makalla akaingia mitini. Hataki kujibu. Baada ya kusumbuliwa sana akaagiza waende kwa RPC Kinondoni. RPC kaagiza waende kwa OCD Oysterbay. OCD akaruhusu hafla ifanyike kwa masharti yafuatayo;

1. Pasiwepo na mziki.
2. Pasiwepo na pombe.
3. Hafla ifanyike kwa dakika 30 tu.
4. Askari waingie ukumbini kusikiliza wanachojadili.
5. Wakimaliza kula watawanyike haraka.

Wanawake wa BAWACHA wamegomea masharti hayo, wanataka wawe huru kufanya mambo yao.

#MyTake;
Mama kemea hawa watu watakuharibia sasa hivi. Hawa akina mama ni wanawake wenzako. Wameamua kukaa, kula na kujadili mambo yao. Kwanini wananyanyaswa? Mwendazake aliwabagua watu kwa vyama vyao. Wapinzani wakawa mistreated kama vile magaidi. Wakapigwa, wakateswa na kunyanyaswa bila sababu.

Wewe ulianza vizuri kwa kuliunganisha taifa. Ukaahidi kuganga makovu yetu. Ukasema tusahau yaliyopita na tufute machozi. Lakini badala ya kutufuta machozi, mbona watu wako wameanza kutuletea machozi tena? Tafadhali wakemee. Jana tumefanya kongamano zuri la Katiba, na dunia imekupongeza kwa sababu polisi hawakutusumbua. Lakini leo hawa akina mama wanasumbuliwa? What happened?
Ningeishangaa intellejensia ya Polisi Kanda Maalumu kama ingeruhusu jana kile walichokiita "Chakula cha usiku cha BAWACHA"

Wanatishia usalama wa Taifa kwa kauli za ajabu ajabu, wanamsakama na kumbeza Rais SSH hadharani.

Hawastahili tena kuachiwa uhuru wa kukutana.

KUIJENGA nchi unaweza tumia damu na muda mrefu ILA kauli moja tu ya kwenye majukwaa au mtandao wa kijamii inatosha kabisa KUIBOMOA nchi.

Bila kujali umaarufu wala hadhi ya fulani Nchi lazima ilindwe kwa nguvu zote, mahatarisho yazimwe na waasi wafutwe.
 
Wazee wa SIASA za matukio tena.

Kuna wakati mnawalaumu tu POLISI.

Kuna kitu leo nishee hapa.

Hivi mnajua kuwa KUIJENGA NCHI NA KUISIMAMISHA NI KAZI SANA ZAIDI YA KUIBOMOA?!!!

Nchi inasimamiwa na Serikali iliyoko madarakani.

Na Serikali yoyote ile duniani Ni lazima IOGOPE machafuko/mapinduzi kwa FAIDA YA NCHI ,watu wake na VIONGOZI WA HIYO SERIKALI.

Sasa huwa tunawalaumu sana Polisi wa hizi nchi zetu za Afrika wakati mwingine KIHISIA tu.

Hebu tufikiri hivi..

Ni juzi tu mh.Mbowe AMENG'AKA MNO.....aliyoyaongea jukwaani ni "alarming point" kwa SERIKALI yoyote hata ingekuwa ni ya CHADEMA.

Baada ya "kung'aka kwake" yakafuata matamko ndani na nje ya nchi....haswa kutoka kwa mh.Tundu Lissu kuwa ,kuhusu KATIBA MPYA ni lazima ipatikane kwa HERI AMA KWA SHARI ....so put yourself in that position....would you let things going without putting your nose on it?!!!

TUTAFAKARI JAMA.....

POLISI WAKO SAHIHI NANYI BAWACHA....2 months ago ,BAWACHA from LAKE ZONE wanted to demonstrate in Dodoma against Speaker's decision on "Covid-19 members of parliament's" before cancelling their gathering following Police's ban.....

Jamani jama ,NCHI HA ZIENDESHWI KILIBERALI eti tu kwa kuwa Kuna UHURU WA VYAMA VYA UPINZANI...UHURU WA KUKUSANYIKA.....

#KaziIendelee
Kwani kupeleka Polisi kuwalinda ingegharimu nini? Wakati mwingine watawala wanawapa wapinzani umaarufu wa bure.
 
Siasa za Chadema ni siasa zembe. Mtu anayetaka nchi isitawalike sio wa kumchekea hata kidogo. Mkulima wa mahindi amchekeae nyani, huvuna mabua! Hata USA wanajua walichokivuna January 6, 2021 baada ya kuingia mtego wa kumchekea nyani.
 
Hivi polisi wanakuwaga na akili saa zingine??!! Yani unaamuru watu wale, wanywe, wazungumze mambo yao kwa dakika 30 tu kisha watawanyike!!
 
Si kweli kwamba serikali zote zinafanya hivyo. Nimeishi nchi 6 tofauti, na ni moja tu kati hizo niliona serikali ni onevu kama hii ya CCM. Watu wengi wanaishi kwenye mazingira huru. Tanzania kwenyewe utawala wa Mwalimu na wa Mwinyi ulikuwa hauna uozo huu wa uonevu.

Nilidhani Mama ni mcha Mungu wa kweli anayechukia uonevu na dhuluma, ila kwa hali hii naanza kuona labda hata yeye kaoza tu kama viongozi wengine wa CCM. Hiki Chama ni ukoma kwa taifa letu. Mimi sina chama but I can smell rubbish a mile away.
Kulikuwa na RPC akiitwa Tibaigana. Huyu Wapinzani wakitaka kuandamana anaita viongozi wao na kukaa mezani kuchora njia watakazopitia kisha siku ya maandamano hutoa askari wayalinde maandamano yafike Jangwani au Mnazi 1 wahutubie muda waliokubaliana ukiisha watawanyike kwa amani.

RPC waliofuatia walikuwa wanatumia mabomu na vurungu na maji ya washawasha kuzuia maandamano. Matokeo ni vurugu mtindo mmoja. Watu kama Lipumba alinjwa mkono. Kuongoza ni kutumia tu hekima na maarifa. Watu wanapofurukutwa ndani, wanata kusema, JK alisema, "Waacheni waseme kwa kuwa kwa njia watapumulia nje hilo fukuto ndani yao kisha wataenda nyumbani kulala. Vilio vya chura gavimzuii ng'ombe kunywa maji"

You can kill a rat in the kitchen silently by using a poisoned carrot or by using a big rungu. Although the choice is yours, but check the consequences.
 
Barakoa mbona hawajavaa Hawa vibaraka wa mabeberu??

Kila siku si wanatishia wananchi juu ya Corona..mbona wao hawachukui tahadhari?
 
Na wao ndo wamemlazimisha kufanya hivyo. Alidhani ni wastaarabu

Naye havimtoshi hivyo viatu alivyovalishwa na Katiba! Amekuwa sehemu ya top brass kwa miaka zaidi ya mitano na bado alikuwa hajui kuwa sio wastaarabu?
 
Back
Top Bottom