G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Mambosasa: Polisi tumesitisha kumuita Tundu Lissu, tunamtaka aendelee na Kampeni zake
Baada ya mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, kukataa kuitikia wito uliotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, uliotolewa jana ukimtaka aripoti kituo cha Polisi Kilimanjaro.
Lissu kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika kuwa ataendelea na ratiba zake ikiwemo kikao cha mabalozi kinachofanyika leo.
“Wito wa polisi sio barua ya kirafiki ni amri kisheria, wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama, huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria, nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho” ameandika Lissu kupitia kaunti yake ya Twitter.
Kwa mujibu ya barua iliyotumwa kwa Mwenyekiti wake wa Chama, Freeman Mbowe, Lissu alitakiwa kuripoti polisi 02/10/2020 kwa ajili ya mahojiano kufuatia kauli na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwenye mikutano yake ya kampeni dhidi ya maafisa wa polisi.
Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi