Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

mkuu wangehariri barua ungesema kawafundisha.

wameamua kuwa madogo ili kuepusha vurugu mnawazomea,lakini wote tunajua kwamba wakiamua kufanya ujinga huwa wanaufanya ujinga uliokomaa.

tufurahi maana amani ndicho kitu tunachoulizia.
Ndio maana tunasema jeshi limekosa weledi!Wanaumbuka na kujidhalilisha kwa vitu vya hovyo hovyo tu visivyo na kichwa wala miguu!
 
kama nime elewa vizuri wito bado uko pale pale ila anatakiwa kuripoti mkoa wa kipolisi Kilimanjaro, na hii ni Zaidi ya ngonjera ya policcm
 
PoliCCM wamekubali Mpira Uishe tu.
Wanakula mabanzi kutoka kila kona ya dunia hii!
1601623583_1601623583-picsay.jpg
 
"Kanda Maalum Ya Polisi Dar Es Salaam" inahusika vipi na uhalifu wa mkoa mwingine, swala la kosa aliloitiwa (Japo halijatajwa) Mh Tundu Lissu ni mkoa wa Mara na akatakiwa ku report Kilimanjaro.

Nchi yetu jeshi la polisi limekosa weredi kabisa, viongozi wanakurupuka na kujiamulia tu anachojisikia, hawajui "TERRITORIAL JURISDICTION/MAMLAKA YA KIENEO" yanakwenda vipi na yana nguvu gani kisheria.

Mambosasa anatakiwa afanye kazi kulingana na "TERRITORIAL JURISDICTION" ya eneo lake, eneo lake na mamlaka aliopewa kisheria ni ya Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam, hana mamlaka kisheria ya kuingilia maswala ya kikazi ya mikoa mingine. Aache kukurupuka kwani atalinajisi jeshi la polisi kuonekana halifuati sheria na mamlaka.

Barua ingekua imetokea "MAKAO MAKUU YA POLISI" raia tusingekua na pingamizi, kwasababu makao makuu ya polisi wana mamlaka ya mikoa yote kisheria. Ila barua inatoka "KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM". Kwa hilo watuache.

Acha lissu awanyooshe hawa vibwengo wenye vyeo vikubwa bila ya kuwa na elimu ya kukidhi matakwa ya kazi yao.

Au lasivyo wakiachiwa, kesho tutasikia Mhalifu amefanya kosa la Kubaka Morogoro halafu Jeshi La Polisi Mkoa Wa Kigoma limetoa barua ya kuachiliwa mara moja mhalifu huyo.
Anafokea Polisi,kwenye kanda maalumu.mbalimbali,kwahiyo kanda ya Dar,wamekasirika sana
 
Ndio maana tunasema jeshi limekosa weledi!Wanaumbuka na kujidhalilisha kwa vitu vya hovyo hovyo tu visivyo na kichwa wala miguu!

jeshi ambalo wanachi waliishalichukulia ni la hovyo halijali hizi filimbi.

wewe ndio utaona unaliabisha,wakati wenyewe hata habari hawana.
 
Back
Top Bottom