Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

"Kanda Maalum Ya Polisi Dar Es Salaam" inahusika vipi na uhalifu wa mkoa mwingine, swala la kosa aliloitiwa (Japo halijatajwa) Mh Tundu Lissu ni mkoa wa Mara na akatakiwa ku report Kilimanjaro.

Nchi yetu jeshi la polisi limekosa weredi kabisa, viongozi wanakurupuka na kujiamulia tu anachojisikia, hawajui "TERRITORIAL JURISDICTION/MAMLAKA YA KIENEO" yanakwenda vipi na yana nguvu gani kisheria.

Mambosasa anatakiwa afanye kazi kulingana na "TERRITORIAL JURISDICTION" ya eneo lake, eneo lake na mamlaka aliopewa kisheria ni ya Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam, hana mamlaka kisheria ya kuingilia maswala ya kikazi ya mikoa mingine. Aache kukurupuka kwani atalinajisi jeshi la polisi kuonekana halifuati sheria na mamlaka.

Barua ingekua imetokea "MAKAO MAKUU YA POLISI" raia tusingekua na pingamizi, kwasababu makao makuu ya polisi wana mamlaka ya mikoa yote kisheria. Ila barua inatoka "KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM". Kwa hilo watuache.

Acha lissu awanyooshe hawa vibwengo wenye vyeo vikubwa bila ya kuwa na elimu ya kukidhi matakwa ya kazi yao. Nchi inaendeshwa na kikundi cha watu wachache wanaojiamulia mambo bila kufuata sheria, wanatumia mamlaka na mabavu, ila sio sheria wala haki.

Au lasivyo wakiachiwa, kesho tutasikia Mhalifu amefanya kosa la Kubaka Morogoro halafu Jeshi La Polisi Mkoa Wa Kigoma limetoa barua ya kuachiliwa mara moja mhalifu huyo.
Kwani RPC wa Kilimanjaro alimuandikia Lisu barua? IGP Siro na hao wa Kanda maalum ndiyo walijitia kimbelembele.
 
Navalny alikuwa mpinga rushwa na mtaka taratibu zifuatwe...Lakini baadaye ikaja kugundulika yupo kwenye orodha ya wanaolipwa na " magenge ya wafadhili vurugu ndani ya nchi" ulimwenguni kote!!! Mara kama mbili iligundulika alipokea maagizo kutoka kwenye genge hilo!!! Navalny mwanzoni alionekana shujaa wa wapenda haki na mwenye 'Akili kubwa'. Navalny ni binadamu pia Lissu ni mtu!
Kura kwa Lissu!
 
Hii ni picha halisi ya jinsi ambavyo taasisi hii muhimu ya kimabavu (polisi) kuwa wana mapungufu mkubwa ya kisheria katika kushughulikia issues zinazohitaji weledi wa kisheria...

Hii ni ishara kuwa watu wengi wameonewa na polisi kwa kuwa tu polisi wao wenyewe hawazijui sheria zinazoongoza utendaji kazi wao....!!

Hii ni crisis inayohitaji kushughulikiwa haraka ili kufikia maendeleo ya haraka na ustawi wa jamii ya watanzania...
 
Sasa asingeipokea haya madubwasha tungeyaona wapi?
Imagine barua muhimu kama hii anaandika secretary halafu hakuna mtu mwingine anaeipitia kuangalia kama ina makosa!Yaani barua anaandika msaidizi wa ofisi halafu anapelekewa boss kusaini halafu boss anasaini tu bila hata ya kuisoma yaani!Jeshi la polisi linatakiwa likaguliwe vyeti
 
Jeshi la polisi hapo nawapongeza sana kwa kuweka busara mbele. IGP Sirro acha kumtetea Magufuli anayevunja sheria ovyo kwa kutukana na kutishia wananchi kuwa hatawaletea maendeleo wakimchagua mtu asiye wa CCM. Hivi NEC hamuoni hili kama ni kosa???? NALIPONGEZA JESHI LA POLISI KWA BUSARA MLIYOONYESHA. Bado huyo DPP anayefungwa watu wasio na makosa kwa sababu ya chuki aliyonayo juu ya CHADEMA.
 
jeshi ambalo wanachi waliishalichukulia ni la hovyo halijali hizi filimbi.

wewe ndio utaona unaliabisha,wakati wenyewe hata habari hawana.
Linazidi kukosa thamani na heshima mbele ya watanzania!
Yaani mpaka watu wakiwaona polisi wanajua ni watu wa mabavu wasio na akili!
 
Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Warumi 12:19

Naamini kwa moyo wangu wote kwamba Mungu anaenda kukupa nafasi ya kuongoza nchi yetu ya Tanzania. Hakuna aliyejua kuwa Daudi angeweza kumwangusha shujaa Goliathi, ila Mungu alimsaidia Daudi.

Kati ya mambo makubwa aliyofanya Daudi ni kutokulipa kisasi kwa watesi wake. NAKUPA ONYO KALI, Usije kulipa kisasi kwa watesi wako, Jitahidi utakapoingia madarakani umweshimu mzee Magufuli wala usiwaze kumtendea baya lolote. Hata ikiwezekana mwachie ndege moja ili awe anaenda nayo kwenye uwanja wa Chato. Usimnyanyase wala kumtenda vibaya.

Hata hao jesi la polisi usiwafanyie chochote kibaya, kwa ghadhabu, wewe tengeneza mfumo mzuri wa jeshi la polisi la kisasa ambalo halijihusishi na siasa wala ukandamizaji wa raia.

Maendeleo yana chama kwa mujibu wa JPM
 
Back
Top Bottom