Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

Uchaguzi 2020 Dar: Jeshi la Polisi lasitisha wito wake kwa Tundu Lissu, lamtaka aendelee na Kampeni zake

kama nime elewa vizuri wito bado uko pale pale ila anatakiwa kuripoti mkoa wa kipolisi Kilimanjaro, na hii ni Zaidi ya ngonjera ya policcm
1. Kwa hiyo barua za wito zilikuwa mbili ya RPC K"njaro na Dsm kwa kosa moja?.
2. Sirro alivyodai aliongea na Mbowe naye alikuwa anasisitiza Lissu ashauriwe aitikie wito gani?.
3. Ni barua gani Lissu anayodai haijataja kosa kati ya hizo mbili?
4. Mambosasa anaposema aendelee tu na kampeni mpaka 28 Oct. ina maana amefuta hata wito wa RPC mwenzake wa Kilimanjaro?.
Nashauri maagizo, wito na maelekezo kwa ngazi ya wagombea Urais yakawa yanatolewa na Ofisi ya IGP tu hata kama mgombea atafanya kosa akiwa mkoa wowote. RPCs wawe wanapeleka malalamiko kwa IGP na kupokea maagizo ya kutekeleza toka kwake kutaepusha mkanganyiko huu.
 
Kwa hali ya kawaida Lissu huyu ana ratiba ya mikutano, Mahera anamumhitaji, polisi wamhitaji. Lengo ni kumtoa kwenye reli . Acheni uchaguzi ufanyike Watanzania waamue hatima yao.
 
mapungasese hayo,nashindwa ku attach video humu,yanasema yana imani na lissu atawavusha wapate kibali huru bongo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
download (2).jpeg
 
[emoji2]
Jamani narudia tena Lissu sio Slaa, Lissu sio Lowasa Lissu sio Mbowe,
Tundu Lissu is Another level..... ndio maana waliona namna pekee ni kumuua lkn kumbe mbeba maono wataifa anapitishwa tu kwenye tanuli la moto ili arudi akiwa imara zaidi
 
Ukiingia JF waweza kudhani Lissu atashinda kuwa Raisi. Ukweli ni kwamba Lissu hatakaa awe Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Sio 2020 ni kamwe(NEVER), hatakaa awe Raisi wa nchi hii. Ila kikatiba mnaruhusiwa kujitekenya na kucheka wenyewe mitandaoni masaa 24(24/7). Tarehe moja mwezi ujao ndo mtaelewa ninachomaanisha hapa.
 
"Kanda Maalum Ya Polisi Dar Es Salaam" inahusika vipi na uhalifu wa mkoa mwingine, swala la kosa aliloitiwa (Japo halijatajwa) Mh Tundu Lissu ni mkoa wa Mara na akatakiwa ku report Kilimanjaro. Mambosasa yanamhusu nini maswala ya mikoa mingine?.

Nchi yetu jeshi la polisi limekosa weredi kabisa, viongozi wanakurupuka na kujiamulia tu anachojisikia, hawajui "TERRITORIAL JURISDICTION/MAMLAKA YA KIENEO" yanakwenda vipi na yana nguvu gani kisheria na mipaka ya mamlaka hayo.

Mambosasa anatakiwa afanye kazi kulingana na "TERRITORIAL JURISDICTION" ya eneo lake, eneo lake na mamlaka aliopewa kisheria ni ya Kanda Maalum Ya Dar Es Salaam, hana mamlaka kisheria ya kuingilia maswala ya kikazi ya mikoa mingine. Aache kukurupuka kwani atalinajisi jeshi la polisi kuonekana halifuati sheria na mamlaka. Anapaswa arudishwe darasani na apelekwe kusoma upya sheria.

Barua ingekua imetokea "MAKAO MAKUU YA POLISI" raia tusingekua na pingamizi, na tungeiheshimu, kwasababu makao makuu ya polisi wana mamlaka ya mikoa yote kisheria. Ila barua inatoka "KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM". Kwa hilo watuache.

Acha lissu awanyooshe hawa vibwengo wenye vyeo vikubwa bila ya kuwa na elimu ya kukidhi matakwa ya kazi yao. Nchi inaendeshwa na kikundi cha watu wachache wanaojiamulia mambo bila kufuata sheria, wanatumia mamlaka na mabavu, ila sio sheria wala haki.

Au lasivyo wakiachiwa, kesho tutasikia Mhalifu amefanya kosa la Kubaka Morogoro halafu Jeshi La Polisi Mkoa Wa Kigoma limetoa barua ya kuachiliwa mara moja mhalifu huyo.

#KUFICHA AIBU, kesho utasikia Mambosasa anaongea na vyombo vya habari na kusema barua hio inayozunguka mitandaoni imeandikwa na watu "WASIOJULIKANA", wananchi tunaombwa tuipuuze.[emoji38][emoji16]
Sasa tume kama kuwatuwengine wanatuchanganya kutoka nyie tume ni police tafadhalini msituharibie nchi yetu sasa nyie mmekosea na police pia wamekosea naniawajibike hapo?
 
Kama ni kweli wamechukua hayo maamuzi basi wametumia Busara.
 
Mh Tundu Lissu & Wafuasi wako
mnayo kila sababu kusherehekea "USHINDI" huu wa kishindo!

Hongereni sana Makamanda kwani Jeshi la Polisi "LIMEWAOGOPA" nyie na Mgombea wenu ambaye ni Mwanasheria Mbobezi!

Sisi tumekubali kushindwa kwenye mechi hii na nyinginezo zote zitakazochezwa KABLA YA OKTOBA 28, 2020!
 
Ninyi mna utundio wa ubongo,inawezekana vipi watu ambao ndiyo huwa mnawategemea katika huduma za maji,umeme,afya,barabara,etc mnawakejeli kuwa ni mabeberu?!Yaani budget ya nchi zaidi ya asilimia 60 inategemea misaada kutoka kwa wazungu halafu mnawaita ni mabeberu!

Yaani wazungu wakiamua kusema leo kuwa waache kuisaidia Tanzania maana yake ni hakuna maji,umeme,barabara,afya,etc.Sasa hebu leo niambie watu wa namna hiyo inawezekana vipi mnawakejeli kuwa ni mabeberu?!Huu kama siyo mtindio wa ubongo ni nini?
Sasa tutaacha lini kuwategemea kama kila tukitaka kujikwamua tuache kuwategemea, kina Lisu wanakuja na kauli kwamba hatuwezi kuishi bila wao mabeberu? Na huyo mtu kumbuka anataka kuwa rais lakini ana akili za nama hiyo,!
Ndio unaona sasa hadi hao beberu wake wamejitokeza hadharani kabisa wanampigania awe rais ili sasa rasmi tusifanye chochote bila wao kuamua!

Nakwambia hivi, oktoba hii Tutampiga yeye Lisu na huyo bebru wake,
 
Ni kazi yao kulinda raia na mali zao!Sasa hawa wa kwetu wanageuka kituko baada ya wao kuwa waanzilishi wa fujo na taharuki kwa kupiga mabomu hovyo au risasi!
Akwilina amgekuwa hai leo kama jeshi lingekuwa linatumia weledi wakati wote!Lakini hiyo go ahead waliyopewa na Magufuli ndio chanzo cha wao kujitoa ufahamu!Yaani mpaka Rais anaongea kwa jazba "i wish i could be IGP",nadhani wale wanakwaya wa Gwajima waliokuwa wanaimba nje ya kituo cha polisi kuna ambao wangekuwa na vilema!Nguvu tembo huku tatizo ni saizi ya siafu!

mwenye mpira ndiye anachagua nani na nani wacheze.
 
Wananchi wenye busara wamewashauri polisi kuachana na Lisu kwakua uu uchaguzi amesha shindwa kwaiyo anatafuta pa kuangushia lawama.
Ameshashindwa!!!! Kwani tumeshapiga kura, kura zimeshahesabiwa na matokeo yameshatangazwa?
 
Wananchi wenye busara wamewashauri polisi kuachana na Lisu kwakua uu uchaguzi amesha shindwa kwaiyo anatafuta pa kuangushia lawama.
Kweli huu mwaka mtaimba hadi kichina kura zinepigwa wapi na zimehesabiwa wapi mkiambiwa mambulula mnavimba na badoo
 
Back
Top Bottom