DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Kwahiyo ni Mali yake binafsi?
Sikuwa nataka kufatilia, lakini kwa jinsi hizi habari zinavuokuja nashawishika kujua ni Nini hasa.
Kwanza huo mzigo umekaa bandarini muda mrefu, Hilo halina ubishi.
Pili mmiliki wa huo mzigo makonda inajulikana - halina ubishi
Tatu mmiliki wa mzigo aliukana - halina ubishi.
Nne mmiliki wa mzigo kaukubali na kutoa vitisho kwa atakaye ununua - halina ubishi

Sasa nijiulize Kuna Nini hapa.
Kama Nia yake haikuw ovu, kwa Nini aukane.
Kama Nia yake ilikuwa nyoofu na kweli kaleta msaada kwanini pawe na mikingamo huko bandari. - zingatia nafasi yake !! Ni mtu wa kukwama ??????

Naridhika kwamba kwenye mzigo huo Kuna Nia ovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nataka nje ya mada kidogo, ivi makontena 20 yanalipiwa kodi ya 1.2b ina maana kontena moja kodi ni 60m kwa mzigo wa fenicha tu???? Wataalam hebu tujuzeni manake mm naona kama ni nyingi sana kwa hivyo Viti.
 
Nimeota kwamba kuanzia leo tarehe 28 August hadi tarehe 2 September, kuna tukio kubwa la mabadiliko ya uongozi litatokea. Na naona anguko la RC likijongea kwa kasi ya mwanga...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We acha tu kuchangia; kwani kuna mtu kakulazimisha? We na rafiki yako mkiacha, sisi tunaopenda maendeleo ya nchi yetu tutachangia. Kwani unadhani ukiacha kuchangia ndo tanzania itaishia hapo? Mlizoea vya kunyonga, unaagiza makontena 20 ukidai ni ya misaada, unasamehewa kodi, mawili ndo unapeleka kwenye misaada, 18 unaweka kwapani. Damn, wabongo wamezoea wizi mpaka wanaona ni haki yao kuiba!
Kama vilikuwa vitu vya kusaidia mashule basi angevigawa kwa hayo mashule baada ya kufika tu, ili hizo shule ndo ziombe msamaha wa kodi serikalini. Kontena zimeandikwa mali ya mtu binafsi, zitasamehewaje kodi km mali ya shule?
Ama wewe usinziaye!
 
Kama una elimu ya kubangaiza huwezi kumwelewa Dr. Mpango. Hili ni suala ka kitaalamu (In Nape's voice).

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Mkuu TRA ndio wanahusika na masuala ya kodi sio TRC.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…