Wanasema kuna maajabu ya dunia yanayopatikana katika nchi mbali mbali, ila Tanzania yenyewe ni ajabu miongoni Mwa maajabu,
Watu wanajitolea kukusanya vifaa kuwasaidia watanzania walioko katika shule zisizo na vifaa Alafu inafika bandarini eti viuzwe,??
Kama wanajali sana hela basi vinunuliwe na wizara ya elimu,
Tanzania ilivyonikatisha Tamaa mimi kuhusu michango ya kujitolea kuokoa majanga nadhani hata wengine wamekata tamaa,
Kuna rafiki yangu mtoto wa mtu mkubwa wa zamani anakaa Norwich nilipomtembelea juma lilee akanambia kuna vifaa vya hospital tuvikusanye tutume visaidie hospital za Tanzania, nisiwe mnafiki nilimjibu Tokea serikali imeleta zuruzunga kwenye Hela ya Tetemeko niliyochangia USD 400 nikidhani zitamfikia yule mama ambaye alitumika kukusanya Hela Mara matembezi masaki Mara changia bukoba, kumbe picha yake inatumika tu, sitakuja kuchangia Janga lolote Tanzania, acha wenye za kuchezea wachange,
Sasa Leo huyo jamaa yangu baada ya kusikia makontena ya makonda ya msaada yamezuiliwa ili yauzwe kanipigia moja kwa moja kwamba ulisema kweli, nami sivikusanyi
Mnakatisha wanaojitolea tamaa,
Ni bora ukatumia hela yako kuinua familia yako kuliko kuchangia Majanga ambayo serikali haithamini mchango wako,
Britanica