DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Wanasema kuna maajabu ya dunia yanayopatikana katika nchi mbali mbali, ila Tanzania yenyewe ni ajabu miongoni Mwa maajabu,

Watu wanajitolea kukusanya vifaa kuwasaidia watanzania walioko katika shule zisizo na vifaa Alafu inafika bandarini eti viuzwe,??

Kama wanajali sana hela basi vinunuliwe na wizara ya elimu,

Tanzania ilivyonikatisha Tamaa mimi kuhusu michango ya kujitolea kuokoa majanga nadhani hata wengine wamekata tamaa,

Kuna rafiki yangu mtoto wa mtu mkubwa wa zamani anakaa Norwich nilipomtembelea juma lilee akanambia kuna vifaa vya hospital tuvikusanye tutume visaidie hospital za Tanzania, nisiwe mnafiki nilimjibu Tokea serikali imeleta zuruzunga kwenye Hela ya Tetemeko niliyochangia USD 400 nikidhani zitamfikia yule mama ambaye alitumika kukusanya Hela Mara matembezi masaki Mara changia bukoba, kumbe picha yake inatumika tu, sitakuja kuchangia Janga lolote Tanzania, acha wenye za kuchezea wachange,

Sasa Leo huyo jamaa yangu baada ya kusikia makontena ya makonda ya msaada yamezuiliwa ili yauzwe kanipigia moja kwa moja kwamba ulisema kweli, nami sivikusanyi

Mnakatisha wanaojitolea tamaa,
Ni bora ukatumia hela yako kuinua familia yako kuliko kuchangia Majanga ambayo serikali haithamini mchango wako,

Britanica
Kiherehere chako. Aliekuambia uchange nani? Sheria ni msumeno. Mnajiokotezea vitu vibovu huko mnaleta huku kwani ni dampo? Lipeni Kodi acheni kulia lia
 
Uungwana ni vitendo...Majuto ni mjukuu!!!!

Kumekuwepo na sakata la muda ninaoweza kusema ni mrefu juu ya uingizwaji wa makontena yenye vifaa mbalimbali vya kusaidia maendeleo jijini Dar.

Nampongeza mkuu wa mkoa kwa initiative zake kwa ajili ya kuhakikisha jiji la Dar linaboreka.

Hakuna doubt kwamba katika awamu hii mambo yote ni lazima yafuate taratibu zilizopo bila kujali ni mambo ya namna gani au ni ya nani.

Sakata la haya makontena limeanza kitambo sana ....limegusa wengi na mengi lakini kwa umuhimu limekugusa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni hardworking na inovative na influential.

Kwa sasa inaonekana kuna mkwamo kuhusu procedures vs intention za kuingizwa kwa Makontena haya.

Kwa sasa najionea 'stance' kati ya mamlaka za Serikali zinazotakiwa kufanya kazi kwa umoja....yaani breach of collective responsibilities!

Kuondoa utata,mkwamo na matokeo mabaya ni muhimu kufanya majadiliano ya kina na kuombana/kupeana misamaha ili mambo yasonge mbele kwa mustakabali wa wanaDAR na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa RC nenda TRA ukaoombe msamaha ikibidi au kuweka sawa procedures ili kufikia suluhisho.

CIAO!!
Ndio umeandiika nini? Makonda ndio mwenye uchungu na maendeleo ya Dar?. Unatukosea heshima mno, huyu kijana hana nidhamu ya uongozi! Mikwamo ishaanza na bado, umri wake bado mdogo sana ametengeneza kitu kibaya sana huko tuendako. Kimsingi procedure ilipaswa aulize kabla ya mzigp kupakiwa, alifanya maksudi akidhani jina lake likiwepo itakuwa rahisi kusamehewa kodi...., kumbe misamaha ya kodi iko kisheria. Anaendelea kulalamika as if anaonewa yeye nani? Mbona ambulance za wabunge tuliona zinapigwa kodi?. Ni kijana aliyepewa nafasi kashindwa kuitumia kwa nidhamu. Kampaka sana matope aliyemchagua pasipo kujua.sasa naona kastuka. Hutakiwi kumwamini Rais, Rais anatakiwa kukuamini, hamshei urais wake hata kama anakupenda vipi!
 
Hii series hii inaonyesha magu kashamchoka Bashite na ndio maana wateuliwa wa magu hawatishiki kwa sasa, na napata uhakika sasa kuwa ni kweli Bashite akili zake hazipo sawasawa maana mara ya kwanza aliyakana hayo makontena kuwa sio yake akaja tena akisema kuwa ni yake na anaomba msamaha wa kodi na sasa anawalaani wanaoyapiga mnada wakati ni yeye mwenyewe mwazo aliyakana kuwa sio yake

Alafu ukimkuta kule insta anavyopost mambo ya kilokole huwezi mshtukia kuwa ni shetani mkubwa huyu

Sent using Jamii Forums mobile app
"
Mi nahisi kuna issue hatuijui kama aliombea makontainer 36 na 20 ndo yqmelima kishoka bandaeini 16 yapo wapi na alimaqnisha nini
 
Cha kujiuliza hivi kwanini Magu amekaa kimya MTU anaonekana kukwepa kodi Mara akatae sio yake?

Nadhani kuna siri nzito kati ya rais na Bashite
 
MAkonda alifanikiwa kuingilia sana wizara ya mambo ya ndani kupitia uenyekiti wa kamati ya ulinzi alivuka mipaka na kuingilia kazi za Mwigulu!

Leo kaingia cha Kike! Kakutana na Mpango kakaziwa; ajue tu pale wizarani yupo mtoto mpendwa kuliko yeye (Doto):
Msikie mpango akimpa za uso hapa!

Siku zimekaribia za gavana kuondoka habebeki!

Makonda fahamu kuwa Dr. mpango siyo mwigulu au ummy mwalimu ambao ulikuwa unawaingilia majukumu yao! Nasubili laana
 
Nakubaliana kabisa na Wewe! Haiwezekani Mhe. Waziri uende hadharani ukapingane na RC kwa kurejerea magazeti. Hii ni laana! RC yeye kaongea na anayemwamini Kanisani na kaomba kwa atakayenunua alaaniwe na sio Serikali ilaaniwe. Sasa nini kilichomtuma Waziri kulumbana? Ama kweli naamini Vita ya Dawa za kulevya alivyoanzisha RC ni vikubwa.
Waziri mzima katoka dodoma,kaja Dar kuyashindilia makontena yapigwe mnada.
Hakutembea makinikia,hakutembelea LW9,huko kuna mali ya mabilioni Tra wanauziana kienyeji na ku refer kuwa huyu alishinda katika mnada fulani
 
Makonda fahamu kuwa Dr. mpango siyo mwigulu au ummy mwalimu ambao ulikuwa unawaingilia majukumu yao! Nasubili laana
Acha utoto wewe
Huyo mpango kaacha ofisi dodoma kaenda bandarini kushindilia container za Makonda tu?Basi hata kutumia ziara hiyo kuamuru na mizigo mingine yote inadiwe,lakini kwa kua anaongozwa kwa chuki mizigo mingine kwake si lolote hata ikikaa miaka 10
 
Acha utoto wewe
Huyo mpango kaacha ofisi dodoma kaenda bandarini kushindilia container za Makonda tu?Basi hata kutumia ziara hiyo kuamuru na mizigo mingine yote inadiwe,lakini kwa kua anaongozwa kwa chuki mizigo mingine kwake si lolote hata ikikaa miaka 10
Acha porojo wewe punguani,chuki gani hiyo? Ndiyo ninyi mnao promote sheria ziwe na macho ! Sheria ni msumeno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mheshimiwa RC nenda TRA ukaoombe msamaha ikibidi au kuweka sawa procedures ili kufikia suluhisho.
Hilo limeshafanyika kazi ipo kwa mpango
Mpango anaamani kwa dhati kabisa ya moyo wake kuwa samani hizo kuukuu ni za Makonda,hivyo basi azilipie ushuru.
Mpango kwa chuki yake kaenda kuyashindilia yauzwe,badala ya kuyataifisha basi yapelekwe shule za serikali nchi nzima
 
Acha porojo wewe punguani,chuki gani hiyo? Ndiyo ninyi mnao promote sheria ziwe na macho ! Sheria ni msumeno

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni mpenzi wa somo la sheria,sishabikii sheria kupindishwa
Sheria ya kodi imempa waziri wa fedha maguvu ya kusamehe kodi bila hata kuliarifu bunge,ndio maana kuna mawaziri waliwahi kudondoka kwa kuitumia sheria hiyo vibaya
Hapa huwezi kumuona mtu kama Zitto,yeye anasubiri magufuli tu ,aweze kutweet
 
Sheria si mnatunga wenyewe na kuzipitisha kwa kusema ndioooo!!Sasa hapo unashangaa nini?!

Alafu jiulize ni kwanini mwanzoni aliakana alafu baadae akayakubali?

We jua tu hilo ni dili limebumbuluka.
unaijua vizuri sheria ya kodi wewe au unabwabwaja tu
 
Kwann jina lake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilivyokuwa Makonda alienda kwenye nyombo vya habari akaomba watu wa nje tutume vifaa alisema kwenye media sio hata siri na akasema lini vitafika watu wa pale Washington state walijua vifaa vinaenda kusaidia watoto na mkuu wa mkoa aliomba viwe kwa jina lake ili asaidie sehemu ambayo haina vifaa lakini kosa lake lisije ku cost watoto wangemtafuta mtumaji ambaye ni Mtanzania ! Kabla ya mnada na angeweza kubadilisha jina
 
Back
Top Bottom