DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Hizi sarakasi za makonda na makontena ni "Agenda Settings" wazee tusiingizwe kwenye 18 za WAKOLOMIJE.
 
Hivi kwani kodi anayotakiwa kulipa mh RC kwa hayo makontena ni shilingi ngapi kwanza ?
Si tuliambiwa ana hela sana huyu mtu...!
Yeye si ana marafiki kibao wenye uwezo....!
Pengine alistahili kuandika barua ya kuomba msamaha Wa kodi kweli, lakini baada ya kukataliwa sidhani kama alipaswa "kulialia" namna hii....
 
Acha utoto wewe
Huyo mpango kaacha ofisi dodoma kaenda bandarini kushindilia container za Makonda tu?
Mimi ni mpenzi wa somo la sheria,sishabikii sheria kupindishwa
Sheria ya kodi imempa waziri wa fedha maguvu ya kusamehe kodi
Post ya kwanza unamponda Mpango post ya pili unatetea sheria ambazo Mpango anazitumia, yaani vijana wa CCM wameshindwa watetee kipi Makonda anayelazimisha kuvunja sheria au Mpango anayefuata sheria.

Anaandika Malisa GJ

#JumapiliAugust26
"Makontena yenye vifaa vya elimu hayatapigwa mnada. Na anayetaka kuyanunua, Mungu atamlaani" Paul Makonda, RC DSM.

#VijanawaCCM: Hureee. Hongera sana mheshimiwa. Wewe ni mtetezi wa wanyonge. Tupo pamoja nawe katika kupigania maslahi ya wanyonge. Wapinzani walifanya fitina ili makontena yapigwe mnada, sasa wameumbuka.

#JumatatuAugust27
"Nimeapa kulinda na kusimamia sheria za nchi, sitishwi na mikwara ya mwanasiasa yeyote. Mpuuzeni huyo anayesema atakayenunua haya makontena atalaaniwa. Mungu hasikilizi maombi ya aina hiyo" Dr.Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na uchumi.

#VijanawaCCM: Hureee. Hongera sana Mheshimiwa Waziri. Serikali makini ni inayoweza kukusanya kodi. Endelea kusimamia sheria ili mapato yaongezeke na uchumi ukue. Tupo pamoja nawe mheshimiwa waziri.

#MyTake:
Najaribu kufikiria aina ya zamadamu waitwao CCM nakosa majibu.!
 
Jana nilisikia ni 1.2b waache wapambane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alichoomba huyo Makonda kanisani ni kosa la jinai.

Upigaji minada ni jambo la kisheria katika kukusanya kodi.

Ina maana hapo anapiga Serikali isikusanye kodi iliyo halali kisheria kwa vitisho kwa wahusika wa zoezi. Hilo ni kosa kubwa sana katika sheria za kodi. Angekuwa ni raia wa kawaida kasema hizo kauli sasa hivi angekuwa lupango akisubiri mashtaka pale Kisutu na tena Makonda huyo huyo angetoa kauli kali..kwanye "MKOA WANGU" sitaki wasiolipa kodi.

Pia anachofanya si sawa...hii ni ya mkuki kwa nguruwe...Serikali imeshapiga mnada mali za watu wengi na kuwafilisi kwa minada ya madeni ya kodi. Mbona hakutoa laana? Na yeye ni sehemu ya serikali, mteule wa Rais, halafu anapinga sheria isifuate mkondo wake kwa vitisho vya laana?

Hilo ni kosa kubwa sana. Tena sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna fumbo kubwa sana katika hili sakata la makontena...Serikali sio taahira kusema haijui umuhimu wa samani hizo kwenye mashule...behind the scene kuna mchezo mchafu sana Makonda alitaka kuucheza...na Serikali imemshtukia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara pap!! BREAKING NEEWZ!!!!,badiliko la baraza la mawaziri,mpango nje!!!!
Ofsini kwetu mabango ya baraza la mawaziri tulishayachana maana kila tukinunua hili,kesho linakuja jipya!!!
 
pole sana makonda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…