DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Wapambe wa Bashite mtapata tabu sana. Hizi ni dalili kwamba mwanzo wa mwisho wake umewadia. Endeleeni kutumika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusafirisha container moja toka US mpaka Dar ni silingi karibia milioni saba.
Containers 20 ni milioni karibia 140. Hapo hujaweka gharama za hizo furnitures.
Je, ingekuwa vizuri kutoa dola laki moja(100,000$) ili utengeneze furnitures Dar (keko) na kutoa ajira kwa vijana wa Dar, kuweka hizo hela (za kigeni) kwenye mzunguko wa fedha mitaani Dar.
Au ni bora, kulipa kampuni za meli za nje fedha za kigeni kusafirisha fenicha kutoka nje, zilizotengeneza ajira nje?

Tuwe tunafikiria kichumi zaidi ili tupate faida kwa kidogo tulicho nacho. Some decisions huwa hazina faida sana, making you wonder .....
 
Tanzania ya viwanda jamaawanataka iwe US ya viwanda Wakati tayari ni ya viwanda. Ningekuwa Mimi ningesema letini hiyo misaada katika Hali ya cash ili wale madogo wa jkt keko watutengenezee fanicha. Badala yake wanakamata watupa taka.
 
Mkitaka kuchanga mchange kama Kwa ajili kusaidia taasisi sio ifike Kwa jina binafsi, Sheria za msamaha wa kodi utambua taasisi, na lazima wajiridhishe ili kuzuia michezo isiyofaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao ni wabinafsi sana na mpaka leo hii siamini kama kweli hizo Furniture ni Kwa ajili ya Walimu,huo ni mradi wake binafsi ila Kwa kuwa Walimu wa Bongo ni daraja la watu kujinufaisha na kupata madaraka ndio hivyo tena wanatumika vibaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbushia na ule mtambo wa kuprosesi taka meya wa kinondoni alivyolalamika kuhujumiwa .
Alitakiwa kulipa Kodi hata kama ulikuwa na faida kwa wote na zoezi likafeli. Meya Yakobo.
Bother ...two wrongs make a right...
Hata JPM walimhujumu wakati akiwa Waziri wa Uvuvi pale alipokamata meli ya wavuvi haramu.
Wanasheria wa serikali kupitia ofisi ya DPP walipeleka shitaka weak, inturn serikali ikashindwa kesi... wakati wavivu walikuwa haramu na walikamatwa ready handed
 
Waziri Mpango ajitayarishe kuachia uwaziri very soon. Hata pona na hili kama yalivyo mkuta Nape.
 

"two wrongs don't make aright"
 
makonda ni mwizi tu, vipi analeta makontena yote hayo kwa jina lake binafsi tena jina lenyewe mpaka leo lina utata, kulikuwa na ugumu gani kuiomba serikali kutoa msamaha wa kodi kabla ya hizo bidhaa kusafirishwa? Huyu alijua mzigo utapita bandarini kwa kumuogopa yeye lakini kitu imebuma. Na Raisi akikalia kimya hili jambo basi na yeye atakua amejijafua.
 
Brother... tayari fanicha ziko bandarini. Walimu hawana fanicha.
Misaada mingapi ya mahindi inakuja toka Marekani inapita bila kodi wakati kuna mahindi Iringa, Katavi na Ruvuma yanaharibika?

Tukiamua kuijenga nchi tuijenge. Tukiamua kufuata sheria sawa tutakuwa sawa pia. Ila suuala je tunapiga hatua au tunarejea nyuma?
...Coming together is a beginning; keeping together is progress; working together is success...
 
Sheria ifuate mkondo wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Go go go! Mpango....asikuyumbishe mtu......we huna hofu ya ajira kama hela unayo.
Simamia sheria....usiskilize maneno ya watu
 
Taja misaada iliyotoka marekani ya mahindi, wakati kuna mahindi mengi Tanzania.
Usipende kuongea vitu visivyo na ukweli ili kuthibitisha vitu ambavyo havina ukweli.
Try another argument.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…