DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Wanasema kuna maajabu ya dunia yanayopatikana katika nchi mbali mbali, ila Tanzania yenyewe ni ajabu miongoni Mwa maajabu,

Watu wanajitolea kukusanya vifaa kuwasaidia watanzania walioko katika shule zisizo na vifaa Alafu inafika bandarini eti viuzwe,??

Kama wanajali sana hela basi vinunuliwe na wizara ya elimu,

Tanzania ilivyonikatisha Tamaa mimi kuhusu michango ya kujitolea kuokoa majanga nadhani hata wengine wamekata tamaa,

Kuna rafiki yangu mtoto wa mtu mkubwa wa zamani anakaa Norwich nilipomtembelea juma lilee akanambia kuna vifaa vya hospital tuvikusanye tutume visaidie hospital za Tanzania, nisiwe mnafiki nilimjibu Tokea serikali imeleta zuruzunga kwenye Hela ya Tetemeko niliyochangia USD 400 nikidhani zitamfikia yule mama ambaye alitumika kukusanya Hela Mara matembezi masaki Mara changia bukoba, kumbe picha yake inatumika tu, sitakuja kuchangia Janga lolote Tanzania, acha wenye za kuchezea wachange,

Sasa Leo huyo jamaa yangu baada ya kusikia makontena ya makonda ya msaada yamezuiliwa ili yauzwe kanipigia moja kwa moja kwamba ulisema kweli, nami sivikusanyi

Mnakatisha wanaojitolea tamaa,
Ni bora ukatumia hela yako kuinua familia yako kuliko kuchangia Majanga ambayo serikali haithamini mchango wako,

Britanica

Wewe ndo Bashite? au tumsubirie mwingine?
 
Tehe tehe labda kama hatuhitaji elimu bure
Kila siku Rais anasema kuna viongozi hawamuelewi,wanabishana wao kwa wao kwa ajili ya kazi ya serikali.
Sheria imempa nguvu waziri wa fedha kusamehe kodi kwa kutoa Government notice na kuichapisha katika gazeti la serikali
Mpango anaudanganya moyo wake kwamba hizo container 20 ni za Makonda zikitoka zitaenda kuuzwa congo,huku akili yake inajua kabisa makonda aliomba msaada kwa niaba ya serikali
Watu warasimu kama akina Mpango hawatufai kwa sasa
Sasa mbona alikataa kuwa makontena hana habari nayo.
 
Ngoja niaze kuagiza magari ya kusaidia walimu na mazagazaga kibao kutoka kwa jamaa zangu wa Canada na USA halafu nione mtu aniulize kodi.
Mbona wengi tunaweza kutumia hili chaka kuagiza kwa kisingizio cha kusaidia, hebu fikiria kila mwanakijiji mwenye access ya kuagiza kutoka kwa marafiki zake afanye hivyo unafikiri nini kitatokea pale bandarini kwetu?
Mtu unatoka kusikojulikana unaagiza kwa jina lako kwa kisingizio cha kusaidia taasisi iliyopo eneo lako huoni mwisho wa siku itakuwa vurugu tu?
Tufate utaratibu, umepata mazagazaga huko kwa rafiki zako itaarifu mamlaka husika ikusaidie kuingiza huo mzigo ili kuepusha siasa za kujikuza badala ya nia ya kusaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha utoto wewe
Huyo mpango kaacha ofisi dodoma kaenda bandarini kushindilia container za Makonda tu?Basi hata kutumia ziara hiyo kuamuru na mizigo mingine yote inadiwe,lakini kwa kua anaongozwa kwa chuki mizigo mingine kwake si lolote hata ikikaa miaka 10
Atakuwa kapigiwa simu aende bandarini na atamke maneno hayo, Dr. Mpango nwenyewe asingefanya hivyo.
 
things are falling apart it seeems the son of a women is no longer at easy thus it might be......the devil is on the cross ......ups down !!!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hapa shida ni hofu na kutokujua au kotokutazama mbali. Ukitizama karibu - short sight kama viongozi hawa wanadai sheria - in long range utakosea. Mangalizo ni mawili au matatu:
1. Consignment ikiwa katika jina la binafsi - RC kisha kuomba msamaha wa kodi kwa msingi ni sahihi sana hasa ikiwa kwamba nia ya matumizi iko wazi na tayari ana zoezi la kuboresha ofisi za walimu na tayari ameshajenga majengo kadhaa, zahanati, maabara etc kwa kuchangisha watu wa ndani wafanya biashara nk. Je kodi kiasi gani ilikusanywa kama capital gain kwa michango hiyo? Ni swali tu anyhow hakuna sheria duniani bila exception. Kila mtanzania alipe kodi na hapo hapo unakuta kuna watu wamekuwa exempted. Mathalani - Watu wote endesha gari kushoto lakini tunaona watu kadhaa na ving'ora wakiendesha kulia bila kujali mwendokasi mtoroko. Hizi ni exception. Sasa hapa ni hekima tu ingetumika zaidi ya kutunishiana misuli na kuleteana stress.

Swali jengine - naljiuliza sasa akiisha RC kulipia kodi je? mtatamani aendelee kugawa bure kwa shule za Dar au mtamshitaki akiuza samani hizi? Najiuliza tu. Aibu kweli kwa hawa wapinzani wetu wa maendeleo.

2. Consignment ikiwa katika jina la taasisi say Ofisi ya RC - hapa sasa ndiyo penye mkanganyo kwa kuwa sasa je serikali ingetumia kodi iliyokusanywa kulipa kodi? Huu ni upuuzi na upotevu wa hesabu za serikali. Anyhow I stand to be corrected BUT kuhusu hili suala la madawati na social service needs nadhani hekima imekosekana au ulevi wa madaraka. Viongozi wakikosa hekima katika madogo huleta fedheha.

3. Double taxation - Nchi yetu ina tatizo kubwa la double taxation yaani usipoangalia unaweza lipa hadi 60% 70% 80% 100% 110% hata 200% kodi na ukaishia kubaki hauna chochote. Hii inadidimiza pia maendeleo kwa kuwa inakuwa illogical to do business

Anyway kupenda vya bure hizi ndiyo gharama zake. Tutamlaumu nani sasa kwa umaskini wetu? Serikali iweke mahitaji ya elimu yakidhi haja, hii itakuwa suluhu ya kudumu kwani ni aibu sana kusema elimu bure ikiwa huwezi kuhudumia kwa kiwango cha ubora na inakuwa bora elimu bure badala ya elimu bora na bure.

FINDINGS:
Huyu RC hata kama hana PhD asiitafute kwa kuwa imeonyesha hawa wenye hizi degree wameshindwa hata kusababisha maendeleo si tu kwa maandiko ya PhD zao bali hata kwao wenyewe. Sasa mfano mkubwa ni PhD holder anapokimbilia siasa katika nchi changa kama Tanzania na kuacha job creation, inaonesha hamna creativity and so big failure. Kuwa kiongozi wa kisiasa sio professionalism, it is about moral judgement and ethics. Hawa wasomi wetu hawana moral judgement and ethics. Example: Samani zipite, zitanufaisha wengi na tutapata leverage ya kodi. Kimsingi nchi ilipasa kupamtia RC comission kwa kufanya jambo kama hili na siyo kuhitaji tena kitu kidogo kuotka kwake. Yeye alishafanya homework yake. Sasa kila mtanzania akifanya jambo creative la kimaendeleo baada ya mwaka mmoja sisi ni first world ikiwa viongozi wote wangekuwa kama huyu RC na siyo kama hawa wengine..

Naomba kuwasilisha
 
Hivi Magufuli si ndo anashtumiwa kumbeba Makonda?
Tuna ushahidi wa kutosha wa marais waliofanya madudu ya kuwabeba ndugu na marafiki kwenye mizigo yao pale bandarini, je Magufuli angekuwa anambeba Makonda ,si angetuma memo tu?? Kwamba hayo makontena yaachiwe Mara moja?

Ninahisi Magufuli hajawahi kumbeba Makonda, ila hapendi kushinikizwa kuchukua hatua,

Naanza kupata mwanga wa mambo mbali mbali

Magufuli hajawahi kumbeba Makonda, si ambebe hata kwa hili??

Au kambeba kaona habebeki? Au kambeba kaona amechoka, au hajawahi kumbeba kabisa
 
#MwananchiNukuu Wengine hugawa watu katika mafungu. Mtu fulani akifanya kosa hata liwe kubwa, hasemwi lakini mwingine akifanya kosa japo dogo hukuzwa likawa kama Mlima Kilimanjaro" Hayati Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere #MwananchiLeo


Sasa huyu bashite kafanya bonge la kosa lakini baba yake anamlinda tu hapo ndo utajua jiwe alivyombaguzi.
Nilivyosikia makontena ya Makonda kutolipiwa ushuru nikajua kumekucha!

Kumbe ni vifaa vya msaada wa taasisi za umma!

Wafafhili wameleta misaada kwa ajili ya mashule, lkn isue inakuzwa utadhani kulikuwa na bidhaa za kibiashara binafsi!

Hii ninashindwa kuuelewa mnyororo wa serikali unavyofanya kazi!

Makonda kabuni hadi kupatiwa hivyo vifaa, kwanini wasimsapoti kuikwamua hiyo misaada kwa walengwa?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom