DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Wanasema kuna maajabu ya dunia yanayopatikana katika nchi mbali mbali, ila Tanzania yenyewe ni ajabu miongoni Mwa maajabu,

Watu wanajitolea kukusanya vifaa kuwasaidia watanzania walioko katika shule zisizo na vifaa Alafu inafika bandarini eti viuzwe,??

Kama wanajali sana hela basi vinunuliwe na wizara ya elimu,

Tanzania ilivyonikatisha Tamaa mimi kuhusu michango ya kujitolea kuokoa majanga nadhani hata wengine wamekata tamaa,

Kuna rafiki yangu mtoto wa mtu mkubwa wa zamani anakaa Norwich nilipomtembelea juma lilee akanambia kuna vifaa vya hospital tuvikusanye tutume visaidie hospital za Tanzania, nisiwe mnafiki nilimjibu Tokea serikali imeleta zuruzunga kwenye Hela ya Tetemeko niliyochangia USD 400 nikidhani zitamfikia yule mama ambaye alitumika kukusanya Hela Mara matembezi masaki Mara changia bukoba, kumbe picha yake inatumika tu, sitakuja kuchangia Janga lolote Tanzania, acha wenye za kuchezea wachange,

Sasa Leo huyo jamaa yangu baada ya kusikia makontena ya makonda ya msaada yamezuiliwa ili yauzwe kanipigia moja kwa moja kwamba ulisema kweli, nami sivikusanyi

Mnakatisha wanaojitolea tamaa,
Ni bora ukatumia hela yako kuinua familia yako kuliko kuchangia Majanga ambayo serikali haithamini mchango wako,

Britanica
Pole kama umejua leo
 
Mwandishi yuko sawa Tanzania ni ngumu hata kuisaidia. Kwa wanaokaa TZ wengi hawawezi kuamini haya lakini sisi wa nje tunajua ndugu zetu. Tunaenda kwenye ma hospital na mashule kuombea vifaa mfano Ali ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Zanz ndiye aliyetuma hivyo vifaa cha ajabu akituma nchi nyingine hakuna hizi shida! Yuko seattle na watu wanajitolea kupakia kwenye makontena, watu wanachangia gharama za kutuma na storage halafu zikifika TZ eti tulipe kodi wakati vifaa ni vya watoto wanaokaa chini ndiyo wameomba. Sasa hiyo kodi ni ya nani kama haitasaidia watoto wanaokaa chini! Tulifikiri kodi ni kusaidia Watanzania.... Halafu watu hao hao wanasema sisi watu
Wa nje hatuna faida maana hatusaidii. Mna mkomoa nani Makonda yupo kwenye jumba la serikali, sisi tuko huku US anayepata shida ni yule mtoto. Sasa wazuri wakitucheka tutasema nini mlitaka watu wasaidiaje kutoa pesa tu ambazo zitaishia kwa wajanja..!
Fuateni utaratibu, sio kujiamlia tu serikali ishashtuka kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani, hao wachangiaji wangefuata utaratibu mambo yangeenda shwari namna ya kuchangia misaada shule za serikali.
 
Ilivyokuwa Makonda alienda kwenye nyombo vya habari akaomba watu wa nje tutume vifaa alisema kwenye media sio hata siri na akasema lini vitafika watu wa pale Washington state walijua vifaa vinaenda kusaidia watoto na mkuu wa mkoa aliomba viwe kwa jina lake ili asaidie sehemu ambayo haina vifaa lakini kosa lake lisije ku cost watoto wangemtafuta mtumaji ambaye ni Mtanzania ! Kabla ya mnada na angeweza kubadilisha jina
Kwani vifaa hivyo vya Makonda unadhani ndio vitamaliza shida ya vifaa kwenye mashule mpaka sheria ivunjwe?
Unadhani kila MTU akiwa na makontena bandarini anasema vifaa vya shule au hospitali Tandahimba basi TRA wanaweka sheria pembeni?
Kumbuka ambulance za mama Salma ilikuwaje? Alilipa kodi kwa mujibu Wa sheria na sio jambo geni.
Kwa Makonda mbona inakuwa issue kubwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaman naomba sana msimuhusishe Mhe. Rais Magufuli na Sakata la Makontena ya Paul Makonda.

Sheria ni msumeno hivyo utekelezaji wa Sheria hauangalii wewe ni nani na unacheo kipi kwenye jamii.

Note: Kodi ni lazima kila mtu alipiye anapopata huduma au anapotoa huduma.

Binafsi sina shaka na maamuzi ya Wazir aliyoyafanya vile vile tukumbuke kuwa ili nchi iweze kupiga hatua ni lazima Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria utumike vizur kwa manufaa ya Umma na siyo vinginevyo.



Sent using Jamii Forums mobile app
Sheria ingekuwa msumeno huyo Maknda angekuawa jela kwa kughushi vyeti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa jiji alikurupuka bila kumshirikisha Mwenye nchi yake...anaonekana kuizoea ikulu hivyo anajiamulia tuu.
Ndio maana anasema Mara nitamwambia baba mtaona, Mara msinunue hayo makotema mtalaanika na vizazi vyenu.
Huyu jamaa amemzoea Rais kiasi cha kumchezea ndevu, na anamuaibisha kweli kiasi kwamba maneno mbovu mbovu yanasemwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nI
Hivi Magufuli si ndo anashtumiwa kumbeba Makonda?
Tuna ushahidi wa kutosha wa marais waliofanya madudu ya kuwabeba ndugu na marafiki kwenye mizigo yao pale bandarini, je Magufuli angekuwa anambeba Makonda ,si angetuma memo tu?? Kwamba hayo makontena yaachiwe Mara moja?

Ninahisi Magufuli hajawahi kumbeba Makonda, ila hapendi kushinikizwa kuchukua hatua,

Naanza kupata mwanga wa mambo mbali mbali

Magufuli hajawahi kumbeba Makonda, si ambebe hata kwa hili??

Au kambeba kaona habebeki? Au kambeba kaona amechoka, au hajawahi kumbeba kabisa
NINA HAKIKA 100% KAMA ANGEKUWA MWINGINE ANGESHAPANGULIWA KITAMBO.
NA HII ISSUE YA MAKONTENA ITAPITA TU KAMA ZINGINE!
 
Na
Hakuwa na nia njema kama usemavyo,kwa nini aandike jina lake binafsi kama vifaa ni vya msaada katika taasisi husika,viuzwe tu next time aagize kupitia jina la taasisi husika
Pia kumbuka hilo sio jina lake, meenye jina lake akija kidai mzigo wake itakuaje wa wahusika wa bandarini?.
 
makonda anajua vizuri njia na taratibu sahihi za kufuata ili hii kodi ipate kusamehewa ikiwa ni pamoja na kusalander documents zote zisomeke si kwa jina lake na ihakikishwe kuwa linafanywa hivyo.
kwenda kulalamika kwenye vyombo vya habari hili ni tatizo zaidi na sio njia ya kulitatua.
sidhani kama ni njia sahihi ya kupeleka miemko kwa jambo la msingi kama hili.
afuate taratibu kama viliagizwa kwa ajili ya shule za dar es salaam si wana accaunt yao walipe wakati wakifuatilia jinsi ya kuasamehewa kwa kukata rufaa?
Wasiwasi wangu vilivyokuja vilishachukuliwa vilivyopo nivingine, hili ninaliamini 78%.
Haiwezekani muda wote wawe wanasubiri kusamehewa kitu kisichosameheka na wasitafute plan b.
 
RC Makonda anastahili kuungwa mkono kwa kazi kubwa aliyoifanya na anayoifanya ya kutatua kero la viti kwa ajili ya wanafunzi na waalimu ndani ya mkoa wa Dar.

Amewatafuta wafadhili, amepata hivyo viti na meza kwa ajili ya waalimu na wanafunzi. Kwanini visiingie bure nchini?.
Serikali inapoomba misaada ya vifaa ama mashine toka nchi za nje, inalipia kodi misaada hiyo?, sasa kwanini RC Makonda alipe kodi wakati mzigo huo si wake binafsi bali ni kwa ajili ya mashule ya serikali ndani ya mkoa wake wa Dar?

Wanaosema mzigo huo ni wa Makonda, hivi kweli mnaamini kwamba Makonda ana njaa mpaka auze viti kama hivyo?.

Jamani hata kama watu wanamchukia RC Makonda kwa utendaji wake ama kwa sababu binafsi, lakini kwenye hili naona ni hekima kumuunga mkono. Kazi aliyoifanya RC Makonda kwenye hili suala limeokoa pesa nyingi za serikali ambazo zingetumika katika kununua ama kutengeneza viti na meza kwa ajili ya waalimu na wanafunzi.
 
Back
Top Bottom