Zillion
JF-Expert Member
- May 15, 2017
- 1,378
- 1,866
Hivi mtu akiteuliwa anatakiwa afanye kazi au awe kibaraka wa kujipendekeza kwa aliyemteua?Nimetokea kumfuatilia sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda kwamba kila anapojua kuwa kafanya tukio au tendo baya la Kumuudhi Mteule na Bosi wake Mkuu Rais Magufuli na ambalo linaudhi na kukera katika Jamii basi Yeye Kesho yake au wiki hiyo au ijayo atahakikisha anafanya tukio moja Kabambe sana la Kimaendeleo kisha anawaita Waandishi wa Habari walichukue na wahakikishe linasambaa ambapo humfikia kwa urahisi sana Bosi wake na kumfanya awe mzito sana Kutengua Uteuzi wake hivyo kujikuta akiendelea tu kumuacha huku wengi wetu tukinuna hadi mishipa ya Fizi inatukakamaa na Makonda anaendelea zake tu Kupeta madarakani.
Tukubali tukatae ukweli ni kwamba japo tunamcheka na kumdhihaki kuhusu Elimu yake na uwezo wake wa Kiupeo lakini kwa matendo yake na Ujanja wake anaoufanya nina uhakika anawazidi Wasomi wengi mno wenye sijui Degree, Masters na PhD's zao na kuna uwezekano mkubwa kwamba pengine wengi wetu tunaojiita Wasomi tungepata tu ujanja alionao Mkuu wa Mkoa Makonda basi huenda leo hii Tanzania ingekuwepo mbali sana Kimaendeleo.
Huyu Jamaa ni Mjanja sijapata kuona na acheni tu Rais Magufuli awe mzito Kumtengua kama RC. Tutanuna na Kukasirika sana ila Jamaa ndiyo Kwanza anachanja zake mbuga tu huku kila Kukicha Kujiamini Kwake kukiongezeka na akiendelea Kuaminika hali ambayo inamfanya Bosi wake azidi Kumuamini na Kumpenda.
Sent using Jamii Forums mobile app