DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Nimetokea kumfuatilia sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul C. Makonda kwamba kila anapojua kuwa kafanya tukio au tendo baya la Kumuudhi Mteule na Bosi wake Mkuu Rais Magufuli na ambalo linaudhi na kukera katika Jamii basi Yeye Kesho yake au wiki hiyo au ijayo atahakikisha anafanya tukio moja Kabambe sana la Kimaendeleo kisha anawaita Waandishi wa Habari walichukue na wahakikishe linasambaa ambapo humfikia kwa urahisi sana Bosi wake na kumfanya awe mzito sana Kutengua Uteuzi wake hivyo kujikuta akiendelea tu kumuacha huku wengi wetu tukinuna hadi mishipa ya Fizi inatukakamaa na Makonda anaendelea zake tu Kupeta madarakani.

Tukubali tukatae ukweli ni kwamba japo tunamcheka na kumdhihaki kuhusu Elimu yake na uwezo wake wa Kiupeo lakini kwa matendo yake na Ujanja wake anaoufanya nina uhakika anawazidi Wasomi wengi mno wenye sijui Degree, Masters na PhD's zao na kuna uwezekano mkubwa kwamba pengine wengi wetu tunaojiita Wasomi tungepata tu ujanja alionao Mkuu wa Mkoa Makonda basi huenda leo hii Tanzania ingekuwepo mbali sana Kimaendeleo.

Huyu Jamaa ni Mjanja sijapata kuona na acheni tu Rais Magufuli awe mzito Kumtengua kama RC. Tutanuna na Kukasirika sana ila Jamaa ndiyo Kwanza anachanja zake mbuga tu huku kila Kukicha Kujiamini Kwake kukiongezeka na akiendelea Kuaminika hali ambayo inamfanya Bosi wake azidi Kumuamini na Kumpenda.
Hivi mtu akiteuliwa anatakiwa afanye kazi au awe kibaraka wa kujipendekeza kwa aliyemteua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majibu yako ni kama ifuatavyo;

1: YALE NI MSAADA so yapite BURE, na atakayenunua atalaaniwa na Mungu wake yeye binafsi.
2: Ametumia utaratibu wa sheria mpya ambayo haijaundwa bado, ya kuagiza mizigo kwa jina lako binafsi na kuomba msamaha wa KODI
3; Aliyakana kwasababu hakusikia vizuri jina lake km limetamkwa, si unajua mara Daudi Bashite, mara Boy from Koromije, mara Paulo Makonda, yani majina mengi so yanachanganya sometime.
4: Watatunga na kutumia sheria mpya ambayo itaondoa vuguvugu lote hili, sheria mpya itaruhusu mtu binafsi kuingiza mizigo ya misaada na kuitoa free.
5: Waliandika makonda kwasababu Diaspora wanamfaham kama Makonda, wangeandika bashite yasingefika,

Subiri ujio wa sheria mpya,

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23] [emoji23] [emoji22] uko sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpango simamia sheria, kama mtu anaona anaonewa basi afuate utaratibu. tabia ya kiongozi kwenda kanisani kupayuka nakutoa vitisho wakati sehemu kubwa ya furnitures ni zake zinapelekwa kwenye hotel yake ya Mwanza ni upuuzi. Kwanza pesa ya kujenga hotel Mwanza kaitoa wapi kwa mda mfupi huu? SOMENI LINK CHINI

Mpango hints at resignation
Clip ipo, mnamlisha maneno. Rais alitajwa kwa kutoa elimu bure siyo kwa kuonesha nia ya kujiuzuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo? Siku za karibu hujapiga safari, niko Tijuana mpakani Mwa Mexico na USA kesho narudi makazini kwangu
week mbili zilizopita nilikuwa Antwerp Belgium
mwez wa tisa nitakuwa Manila Philippines na Melbourne, Canberra Australia,pia baadae Auckland newzeland
Niko na shirika LA kikatoliki
 
Angeshugulika na madawa ya kulevya kabla ya hili tungemwelewa. Je alimpima mweshimiwa Mbowe kuona kama alikuwa na chembe za madawa? Tuna mbao kibao zinauzwa na kuibiwa kwenda China kwa nini tuletewe toka US? Angeomba vitabu vya Maths, Science na vingine tungeelewa. Viti na meza?
 
Back
Top Bottom